content
stringlengths
1k
24.2k
category
stringclasses
6 values
Mashabiki wa timu hizo wamekuwa wakitam- biana kuanzia mitaani, nyumbani, katika vyombo vya usafi ri, sokoni, vijiweni na kila mahali, ambapo kila mmoja akitamba kuibuka na ushindi leo.UPINZANI MKALIUpinzani mkali kwa timu hizo unaonekana kuongezeka baada ya Yanga kumchukua mshambuliaji hatari wa watani wao wa jadi Si...
michezo
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo amesema, anatilia mkazo suala la elimu na kuongeza wigo wa vyanzo vya uchumi kwa wananchi ili hata akiondoka huko wananchi wamkumbuke kwa hayo.Ameieleza timu ya wafanyakazi kutoka Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) kuwa, wapo kwenye mchakato wa kuweka historia kwa kujenga ...
uchumi
PASIPOTI mpya ya Tanzania ya kielektroniki, imetunukiwa Tuzo ya kuwa pasipoti bora katika Ukanda wa Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika, kwa kukidhi viwango vya ubora wa kiusalama.Viwango hivyo vinapendekezwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia Usafiri wa Anga (ICAO).Akiwasilisha Bajeti ya Wizara ya Mambo ya N...
kitaifa
KOCHA Mkuu wa Taifa Stars Emmanuel Amunike amefurahishwa na kiwango kilichooneshwa na wachezaji wake dhidi ya timu ya taifa ya Uganda jana.Amunike alipewa jukumu la kuinoa Taifa Stars mwezi mmoja uliopita akichukua nafasi ya kocha Salum Mayanga huo ulikuwa mchezo wake wa kwanza ambapo walitoka sare ya bila kufungana d...
michezo
BAADA ya kutolewa mapema katika michuano ya Kombe la Mapinduzi iliyomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita, Yanga inahamishia hasira zote kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mwadui ya Shinyanga utakaochezwa leo.Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kuanzia saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Kati...
michezo
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), imeanza kupokea rufaa za mikopo kwa mwaka wa masomo 2018/2019 kuanzia juzi. Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa na bodi hiyo juzi kwa vyombo vya habari, wanafunzi wote wa taasisi za elimu ya juu, wanatakiwa kutuma rufaa zao kwa njia ya mtandao.HESLB ilisema kuwa dirish...
kitaifa
HALMASHAURI mbalimbali za mkoa wa Dodoma, zimetakiwa kuhakikisha zinapima na kulinda ardhi inayofaa kwa kilimo cha zabibu.Hayo yameelezwa na Ofisa Kilimo Mkoa, Bernard Abraham alipokuwa akiwasilisha mada ya namna ya kuongeza uzalishaji wa zao la zabibu na alizeti kwenye kikoa cha Baraza la Biashara Mkoa wa Dodoma.Alis...
kitaifa
ROBERTO Oliveira amewapongeza wachezaji wake wa Rayon Sports baada ya kuifunga Kirehe mabao 4-0 na kutwaa taji la Ligi Kuu ya Rwanda ya Azam msimu wa mwaka 2018-19.Rayon Sports ambayo imeivua ubingwa APR, imetwaa taji hilo huku ikiwa na mchezo mmoja mkononi kabla ya kumalizika kwa ligi hiyo inayoshirikisha timu 16. Hi...
michezo
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu kifungo cha miaka miwili jela au faini ya Sh 500,000 aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Katibu wake, Celestine Mwesigwa.Vigogo hao wa TFF walihukumiwa kifungo hicho au kulipa faini baada ya kutiwa hatiani kwa mashitaka ya kughushi muhtasari...
michezo
SERIKALI imesema mpaka sasa zaidi ya asilimia 59 ya wakulima wa korosho wamelipwa fedha zao, lakini wabunge wamehoji deni la fedha za ushuru kwa halmashauri.Pia, wametaka kujua hatua zilizochukuliwa kwa watendaji wa serikali, waliobainika kufanya ubadhirifu wakati wa uhakiki wa wakulima. Aidha, tani 213 za korosho zim...
kitaifa
SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limetia saini mkataba wa mauziano ya gesi asilia na kampuni ya Shreeji Silicate Tz Ltd kwa miaka 10 inayoweza kuongezeka kulingana na makubaliano.Meneja wa Biashara za Gesi, Dora Ernest alisema amesema TPDC itauza gesi asilia futi za ujazo milioni 0.4408 kwa siku kwa mia...
kitaifa
POLISI jijini Mwanza imemkamata askari magereza Kibemba Warioba (27) mwenye namba za usajili B.9205 WDR, akiwa na simu tano za aina tofauti na mitandao tofauti akijihusisha na makosa ya kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro amesema kuwa tukio hilo limetokea juzi saa nn...
kitaifa
SERIKALI ya Tanzania imekubaliana na serikali ya Sudan Kusini kuimarisha ushirikiano katika sekta ya usafirishaji ili nchi hiyo ipitishe mizigo kwenye bandari ya Dar es Salaam.Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi amewaeleza waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa,...
uchumi
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla, amesema ili kukuza utalii wameanza mazungumzo na klabu ya KRC Genk anayochezea Mbwana Samatta ili kutangaza utalii nchini Ubelgiji.Akizungumza jana Dk Kigwangalla alisema wapo kwenye kuandaa mkakati mahsusi, kwa ajili ya kujitangaza kwenye nchi hiyo. “Tayari pia tu...
michezo
['Wachezaji nyota wa Arsenal Mesut Ozil na Sead Kolasinac wameripotiwa kuvamiwa na genge la majambazi katika jaribio la wizi wa gari katika barabara za mji wa London.', 'Klabu ya Arsenal imethibitisha kuwa wachezaji wake Mesut Ozil na Sead Kolasinac walilengwa na majambazi hao waliokua wamejihami lakini hawakujeruhiwa...
michezo
Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Pwani utafikishwa kwenye balozi za Tanzania nje ya nchi ili watu wa huko wazifahamu fursa zilizopo waje kuwekeza.Mkuu wa mkoa huo, mhandisi Evarist Ndikilo ameiagiza sekretarieti ya mkoa kuwasiliana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ili mwongozo huo ufikishwe kw...
uchumi
RAIS wa Marekani, Donald Trump amepokea barua kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa Korea Kaskazini (DPRK), Kim Jong Un ambayo pamoja na mambo mengine imeelezwa kuwa viongozi hao wanatarajia kukutana hivi karibuni kwa mkutano wao wa pili.Trump aliwathibitishia waandishi wa habari Ikulu ya Marekani kuwa ni kweli amepok...
kimataifa
["Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amesema kuwa Paul Pogba ''hajawahi kuwa tatizo'' na kuwa kuna ''ajenda'' dhidi ya kiungo huyo mfaransa.", "Wakala wa Pogba, Mino Riola amesema mchezaji huyo, 26, anataka kuondoka united na ana matumaini kuwa ''kutakuwa na suluhu lenye kuridhisha kwa pande zote''.", "Pog...
michezo
.Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Inmi Patterson amekabidhi vifaa mbalimbali vyenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 18 (Tsh bilioni 41.6) kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kama sehemu ya Kikosi Maalumu cha Kulinda Amani cha Afrika (African Peacekeeping Rapid Reaction Program – APRRP).Ubia wa ...
kitaifa
Hii ni wiki ya pili sasa Simba imepiga kambi nchini humo, ikijifua kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara, huku lengo kubwa la kocha huyo raia wa Cameroon, kutwa taji ambalo linashikiliwa na mahasimu wao Yanga.Akizungumza na gazeti hili kutoka Johanesburg, kocha Omog alisema mechi hizo mbili nd...
michezo
RAIS wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein ametoa pongezi kwa wachezaji wa timu ya taifa, Zanzibar Heroes na viongozi wao kwa kuiwakilisha kwa nidhamu Zanzibar katika Michuano ya Kombe la Chalenji mjini Kampla, Uganda.Michuano hiyo inatarajiwa kufikia tamati kesho kwa fainali kati ya wenyeji Uganda na Eritrea. Zanzibar il...
michezo
TIMU ya taifa ya netiboli ya Tanzania, Taifa Queens, leo inatarajia kuanza mazoezi rasmi kujiandaa na mashindano ya Afrika yatakayofanyika Pretoria, Afrika Kusini kuanzia kesho, Oktoba 16 hadi 23, imeelezwa.Kocha wa timu hiyo, Argentina Daud alithibitisha jana kuwa leo anatarajia kukutana kwa mara ya kwanza na wacheza...
michezo
Kaimu Mtendaji Mkuu wa RwandAir, Chance Ndagano amesema shirika hilo litafanya safari nne kwa wiki kutoka Kigali kuelekea Cape Town na Harare, Zimbabwe.Hawakutangaza siku maalumu ya kuanza safari hizo lakini alisisitiza kuwa haitachukua muda mrefu.Amesema, usafiri huo wa Abuja nao unatarajia kufanya safari zake mara n...
uchumi
KILIMANJARO Queens imekuwa timu ya kwanza kutinga nusu fainali ya michuano ya Wanawake ya CECAFA inayoendelea kwenye uwanja wa Chamazi Complex Dar es Salaam.Hiyo inatokana na vipigo inavyoendelea kuvitoa katika kundi A, ambapo hadi sasa wameweza kushinda mechi zote mbili na kufunga mabao 13. Kilimanjaro Queens ambao n...
michezo
KOCHA wa Gor Mahia, Hassan Oktay huenda akawa kocha wa kwanza kuiongoza klabu hiyo kwenye hatua ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kama atakwepa kipigo Nigeria Ijumaa ya wiki hii.Shirikisho la Soka Afrika (CAF) lilibadilisha michuano hiyo kutoka kwenye Kombe la Mabingwa Afrika kati ya mwaka 1964 na 1996...
michezo
KOCHA wa Simba, Patrick Aussems amesema mipango yake ni kutumia vema uwanja wa nyumbani ili kuhakikisha wanashinda mchezo mmoja uliobaki dhidi ya AS Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.Simba baada ya juzi kuifunga Al Alhly kwa bao 1-0, imebakisha mechi mbili, moja ugenini dhidi ya AS Saoura ya Algeria na ile...
michezo
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo amesema kuondolewa kwa kodi ya majengo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na kuwekwa kwenye mfuko wa Serikali Kuu umesaidia mamlaka hizo kupata fedha za kutekeleza miradi zaidi ya mapato waliyokuwa wanakusanya.Aidha, amekeme...
kitaifa
WIZARA ya Nishati imewasilisha makisio ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ikiwa na ongezeko la asilimia 26.6, huku kiasi kikubwa kikielekezwa katika miradi mitatu ya kimkakati, ukiwamo wa Rufiji (Stigler) uliotengewa Sh trilioni 1.443.Aidha, mafanikio kadhaa yamepatikana tangu Serikali ya Awamu ya Tano kuingia mad...
kitaifa
WIZARA ya Maliasili na Utalii imeunda kamati yenye jukumu la kutatua changamoto zinazoikabilia sekta ya utalii ikiwa ni pamoja na kuja na mapendekezo ya kuiendeleza sekta hiyo.Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Adolf Mkenda wakati akizungumza na gazeti hili kuhusiana na mikakati ya Wizara katika...
kitaifa
['Aston Villa kumsajili mshambuliaji wa Genk na Tanzania kwa dau la £10m', 'Aston Villa inatumai kukamilisha makubaliano ya dau la £10m kumsajili mshambuliaji wa Genk Mbwana Samatta huku mkufunzi Dean Smith akilenga kuimarisha safu yake ya mashambulizi.', 'Dean anahitaji kuimarisha safu hiyo baada ya kumpoteza mshamb...
michezo
UMOJA wa Wafanyabiashara kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (BCI) umepokea kwa faraja mazungumzo kati ya Rais John Magufuli na Rais wa Congo Felix Tshisekedi, huku ukiamini kuwa ziara ya Rais huyo hapa nchini itazidi kufungua fursa za kibiashara baina ya nchi hizo.Aidha, Umoja huo umeiomba Serikali ya Tanzania k...
uchumi
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Humphrey Polepole amewataka wabunge wa CCM nchini, kuacha kulala usingizi au kutafuta kiki ya kisiasa kwa mgongo wa Rais John Magufuli.Badala yake, amewataka kuwatumikia wananchi katika majimbo yao na kuiga mfano uliofanywa na mbunge wa jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama wa ku...
kitaifa
Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) imesema Jukwaa la Fursa za Biashara Tabora ni sehemu muhimu kwa mkoa huo kuzitangaza fursa zilizopo na kujiuliza kwa nini upo ulipo na utafikaje unapotaka kufika.Kaimu Mhariri Mtendaji wa kampuni hiyo, Tuma Abdallah amesema mjini Tabora kuwa, jukwaa hilo linatoa fursa kwa wajumbe ...
uchumi
HIFADHI ya Taifa ya Ruaha imejipenyenza katika vyuo vikuu 20 nchini na itafanya hivyo katika vyuo vingine vyote vilivyobaki; ukiwa ni mmoja wa mkakati wake wa kuwatumia wanazuoni kukuza utalii wa ndani.Viongozi zaidi ya 40 wa Serikali za wanafunzi wa vyuo hivyo vilivyopo katika mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya, Iringa, D...
uchumi
SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) limepania kurahisisha usafirishaji wa mizigo katika ukanda wa Afrika Mashariki na nchi nyingine za karibu.Wiki iliyopita TRC ilirejesha safari za treni za mizigo kutoka Tanzania mpaka Kampala Uganda kupitia Tabora, Isaka, Mwanza na Ziwa Victoria kwa kutumia bandari ya Mwanza na Port Bell...
uchumi
TAKRIBANI wajasiriamali wadogo 8,000 wanatarajiwa kupewa vitambulisho katika wilaya za Muheza na Lushoto mkoani Tanga, vilivyotolewa na Rais John Magufuli. Kazi ya utoaji vitambulisho hivyo kwa wajasiriamali hao ilizinduliwa na wakuu wa wilaya hizo juzi Alhamisi.Wilayani Muheza, kwa mujibu wa Idara ya Biashara ya Halm...
kitaifa
JAJI Mkuu mstaafu, Mohamed Chande Othman ameagwa rasmi kimahakama baada ya kustaafu utumishi wa umma.Jaji Othman alikuwa Jaji Mkuu tangu mwaka 2010 hadi mwaka 2017.Sherehe ya kumuaga imefanyika katika Mahakama Kuu, Dar es Salaam.Jaji Chande ameushukuru uongozi wa serikali kuanzia Awamu ya Tatu chini ya Benjamin Mkapa ...
kitaifa
MJUMBE wa Marekani katika Afrika, Tibor Nagy anakwenda Sudan ambako kuna hali tete kutokana na mgogoro wa kisiasa unaoendelea.Nagy ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika, anakwenda kuomba kusitishwa mashambulio dhidi ya raia. Kutokana na mgogoro huo, kumekuwa na mgomo wa kitaifa wa wafanyakazi ulioanza Jumap...
kitaifa
MABINGWA wa Tanzania Bara Simba, wamebanwa mbavu na timu ya Namungo itakayoshiriki Ligi daraja la kwanza msimu huu.Timu hiyo ya Mkoani Lindi ilimenyana na Simba jana katika Uwanja wa Majaliwa na kutoka suluhu katika mchezo huo ambao ulikuwa rasmi kwa ajili ya kuuzindua uwanja huo. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alikuwa m...
michezo
Juhudi za karibuni kuimarisha uhusiano huo, zimeshuhudiwa wiki hii ambapo wawakilishi wa wafanyabiashara kutoka nchi hiyo kubwa kiuchumi Afrika walitembelea nchini kwa mazungumzo zaidi.Ujumbe huo ulihudhuria semina kuhusu biashara kati ya nchi hizo iliyofanyika juzi jijini Dar es Salaam, ambayo ilitayarishwa na Kituo ...
uchumi
Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa NBS, Ephrahim Kwesigabo alisema hiyo inamaanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Februari 2015 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia Januari mwaka huu.Alisemaa fahirisi za bei zimeongezeka hadi 154.83 k...
uchumi
BALOZI wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa, Modest Mero amesema Tanzania inatarajiwa kuwasilisha taarifa yake katika vikao vya Umoja wa Mataifa (UN) Julai mwaka huu, ikiwa ni miongoni mwa nchi wanachama 92 wa mwanzo kupewa nafasi hiyo.Balozi Mero alisema hayo wakati alipokutana na Makamu wa Pili wa Rais, Bal...
kitaifa
MSHAMBULIAJI wa Paris-St-Germain (PSG), Neymar atakuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki 10 baada ya kuumia mifupa ya miguuni, itakayomfanya kuukosa mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya dhidi ya Manchester United.Mshambuliaji huyo Mbrazili aliumia wakati timu yake ikishinda mabao 2-0 katika mchezo wa Kombe la Ufaransa d...
michezo
MIPAKA ya Tanzania na nchi za Kenya, Uganda na Burundi imeanza kuimarishwa katika hatua mbalimbali ili kufikia lengo la serikali kuhakikisha ifikapo mwaka 2022 uimarishaji wa mipaka hiyo kuwa imekamilika.Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alibainisha hayo katika hotuba yake ya bajeti aliyoi...
kitaifa
Yanga imeangukia kwenye michuano ya Caf, baada ya kutolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na timu ya Township Rollers ya Botswana kwa jumla ya mabao 2-1.Akizungumza na gazeti hili Lwandamina, alisema kurejea kwa wachezaji hao kumeongeza matumaini ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo ambao amepania kupata us...
michezo
VIGOGO tisa wa taasisi za serikali ikiwamo Mahakama, Ofi si ya Mwanasheria wa Serikali, Jeshi la Polisi na Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Arusha, kwa tuhuma za kughushi na kumtorosha mtuhumiwa wa kesi ya ujangili.Mbali ya kufanya hivyo, pia watuhumiwa hao wanatuhumiwa kuch...
kitaifa
Makamu wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal amesema hayo mjini Kigoma jana wakati akifungua kongamano la uwekezaji ukanda wa Ziwa Tanganyika linalohusisha mikoa ya Kigoma, Katavi na Rukwa.Dk Bilal alisema kwa sasa uwekezaji mkubwa umekuwa ukifanywa katika sekta za kilimo, madini na umeme na kwamba kuimarishwa kwa uwekeza...
uchumi
WAKATI Wizara ya Viwanda na Biashara ikisimamia ujenzi wa viwanda 100 kwa kila mkoa, pia imeanza mikakati ya kutumia rasilimali zilizopo katika kila kijiji nchini kujenga viwanda kwa kushirikiana na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO).Hatua hiyo, itasaidia kila kijiji kuzalisha bidhaa itakayouzwa kwenye vijiji ...
uchumi
BAADA ya vuta nikuvute na subira ya muda mrefu, hatimaye leo Yanga wanatarajia kufanya uchaguzi na kupata viongozi wapya watakaoiongoza timu hiyo kwa miaka minne ijayo.Kwa mujibu wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) chini ya mwenyeikiti wake, Ally Mchungahela na Kamati Maalumu ya Yanga ya kusimam...
michezo
TIMU ya Azam FC imewapa zawadi ya mwaka mpya mashabiki wake baada ya kuifunga Singida United kwa mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Shekh Amri Abeid jana.Katika mchezo huo ambao ulihudhuriwa na mashabiki wachache, Azam FC walianza kupata bao dakika ya 26 likifungwa na Brayson Rafael...
michezo
WABUNGE wameiomba serikali iweke kituo kimoja cha utoaji huduma za vibali, ili kupunguza mlolongo na urasimu katika utoaji vibali vya biashara kwa wawekezaji.Wabunge walitoa ushauri huo wakati wakichangia bajeti ya wizara ya viwanda na Biashara, iliyowasilishwa bungeni hapo na Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kak...
kitaifa
TIMU ya Taifa ya Soka ya Wanawake chini ya umri wa miaka 17, leo inashuka uwanjani kucheza mchezo wa marudioano kufuzu Kombe la Dunia 2020 nchini India dhidi ya Burundi, utakaochezwa Bujumbura katika Uwanja wa Intwari, (zamani Prince Louis Rwagasore).Timu hiyo ambayo iliondoka juzi kwa ndege ya Shirika la Ndege la Tan...
michezo
['Mchezaji nyota wa Liverpool Sadio Mane ameisaidia Senegal kutinga robo fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) baada ya kuilaza Uganda bao 1-0.', 'Bao hilo la ufunguzi lilitiwa wavuni na Mane katika dakika za mwanzo wa kipindi cha kwanza liliashiria mwanzo mzuri kwa Senegal katika kampeini yake kuel...
michezo
LIGI Kuu ya soka ya wanawake inatarajiwa kuendelea leo baada ya kusimama kwa mwezi mmoja kupisha michuano ya kombe la Chalenji iliyofanyika nchini mwezi uliopita. Ligi hiyo ambayo inaingia katika mzunguko wa tatu leo itachezwa michezo sita katika viwanja vya miji tofauti.Bingwa mtetezi JKT Queens itacheza na Simba Que...
michezo
MKUU wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme amesema kufungwa kwa Benki ya Wananchi ya Mbinga mkoani humo kumeathiri kiasi kikubwa uchumi wa wakulima na jamii.Mndeme amesema hayo jana kwenye ufunguzi wa Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Maendeleo ya mkoa wa Ruvuma (RCC) mjini Songea.Amesema kufungwa benki hiyo kumesababisha ...
uchumi
SIMBA jana ilitoka suluhu na Azam katika mechi ya Ligi Kuu Bara na hivyo kuifanya kusubiri zaidi kabla ya kupata pointi za kutosha kutetea taji lake. Mechi hiyo iliyofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam ilikuwa ya kuvutia huku timu zote zikishambuliana kwa zamu.Matokeo hayo yanaifanya Simba iendelee kukaa kile...
michezo
Ametaka Manispaa ifanye hivyo kabla ya kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho. Alitoa kauli hiyo kupitia taarifa yake, aliyotuma kwa vyombo vya habari.Aliongeza kuwa hatua hiyo itaondoa migogoro baina ya wamachinga hao na uongozi wa manispaa, unaojitokeza mara kwa mara kutokana na uongozi huo kutochukua hatua mapema.Mbu...
uchumi
UGANDA imefanikiwa kupiga hatua kubwa katika kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Ukimwi kutokana na kushuka kutoka asilimia 18 mwaka 1990 hadi asilimia sita mwaka huu.Ripoti ya Tume ya Ukimwi ya Uganda (UAC) inasema, baadhi ya mbinu zilizotumiwa na serikali ya Uganda kufanikisha mafanikio hayo ni pamoja na kuharak...
kitaifa
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein amewataka wadau wa sekta binafsi kutoa huduma bora kukidhi viwango na ubora kukidhi malengo na matarajio ya jamii. Alisema hayo jana ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni alipofungua Jukwaa la Biashara la tisa, Zanzibar.Jukwaa hilo lil...
kitaifa
MFANYABIASHARA maarufu mkoani hapa, Hans Paul amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani hapa kwa kosa la kuajiri raia watatu wa kigeni bila ya kuwa na vibali vya kufanya kazi nchini.Mfanyabiashara huyo anamiliki kampuni tatu jijini hapa ambazo ni Dharam Singh Hans Paul & Sons LTD, Hans Paul Ltd na ...
kitaifa
Utaratibu mzuri wa kuhudumia wawekezaji na juhudi za viongozi vimekuwa na mvuto kwa wawekezaji, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Asumpta Mshama amesema mjini humo.Ameieleza timu kutoka Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) kuwa, huduma kwa wawekezaji zinafanywa kwa haraka Kibaha kiasi cha kuwavutia wengi kuwekeza.Wafanyakazi...
uchumi
YANGA leo inashuka kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya kucheza dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.Mabingwa hao wazamani wa Ligi Kuu Tanzania Bara, wanasaka ushindi mwingine ugenini leo ili kujiongezea pointi baada ya hivi kartibuni kuifunga Mwadui ya Shinyanga kwa mabao 2-...
michezo
MTAFITI binafsi nchini amebuni kanuni inayoweza kutumika kubadilisha gesi asili inayopatikana nchini kuwa kwenye mfumo wa LPG na kujazwa kwenye mitungi kwa ajili ya matumizi ya kupikia majumbani.Akizungumza kwenye Jukwaa la Mabadiliko ya Tabia Nchi, lililofanywa kwenye Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es...
uchumi
Rais John Magufuli amekabidhi vitambulisho 670,000 kwa wakuu wa mikoa yote nchini kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo wadogo.Amekabidhi vitambulisho 25,000 kwa kila mkuu wa mkoa hapa nchini ambao wamepewa jukumu la kuvigawa kwa wafanyabiashara hao kwa kigezo kuwa biashara zao ni lazima ziwe chini ya mtaji wa Sh mil 4/...
kitaifa
MAKUBALIANO ya kimataifa yakiwemo yanayotaka Serikali kutoa kipaumbele kwa sekta kadhaa kwa kutenga kiwango fulani katika bajeti, yamebainika ni vigumu kutekelezwa ipasavyo kutokana na uhaba wa fedha zinazopaswa kugawanywa.Serikali imekiri kuhusu hilo ikisema kazi inayotakiwa kufanyika, ni kujielekeza kuwezesha ukusan...
kitaifa
['Atletico Madrid imeanzisha mchakato wa kumuadhibu mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann, 28, ambaye anatarajiwa kuhamia Barcelona kwa dau la £107.5m . (Guardian)', 'Real Madrid inafikiri kumuuza mshambuliaji wake raia wa Colombia James Rodriguez, 27, ili kukusanya £150m kumnunua kiungo wa kati wa Manchester Unit...
michezo
Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Ole Nasha aliyasema hayo bungeni jana wakati akijibu swali la Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara (Chadema) aliyetaka kujua mpango wa serikali wa kuzuia uingizaji wa mayai kutoka nje kutokana na mayai hayo kuharibu soko la ndani.Naibu Waziri alisema kuanzia mwaka 2006, serik...
uchumi
WAFANYAKAZI sekta rasmi Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wanatarajia kuwa na uwezo wa kuhamisha michango yao ya pensheni na mafao katika mfuko mwingine kwenye ukanda huu wa EAC.Hatua hiyo imelenga kuwezesha utekelezaji wa itifaki ya soko la pamoja na kuwezesha utoaji pensheni katika ukanda huo ambao kwa sasa inakadir...
kitaifa
WATAFITI kutoka Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT) wamewashauri wafanyabiashara ndogo mkoani Dodoma wapewe mafunzo ili waondokane na changamoto ya namna ya kukuza mitaji na kufi kia hatua ya kuwa wafanyabiashara wa kati.Hayo yalielezwa na Dk Wambuka Rangi kutoka OUT wakati alipokuwa akiwasilisha utafiti kwenye warsha ya ...
uchumi
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa wakuu wa taasisi za serikali, wanaohusika na udhibiti wa mizigo katika maeneo hayo na wadau wa sekta binafsi, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Charles Kichere amesema lengo la kuwashirikisha wakuu hao ni kujenga uelewa wa pamoja wa utekelezaji wa mf...
uchumi
SERIKALI imetoa kanuni mpya za usimamizi wa mazingira katika kutekeleza agizo la kutotumika kwa mifuko ya plastiki nchini ambapo faini zake zimo za kifungo cha siku saba jela na faini ya hadi Sh bilioni moja.Chini ya kanuni hizo mpya, atakayekutwa na mfuko wa plastiki atatozwa faini ya kati ya Sh 30,000 hadi Sh 200,00...
kitaifa
MICHUANO ya kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati kwa wanaume inatarajiwa kutimua vumbi leo mjini Kampala kwa timu za kundi A, wenyeji Uganda wakitarajiwa kuchuana na Burundi na Somalia dhidi ya Djibouti.Michuano hiyo itakayofanyika kwenye uwanja wa Startimes jijini Kampala imeandaliwa na Baraza la so...
michezo
Hayo yalibainishwa na Meneja Mkuu wa mgodi huo wa Biharamulo, Dennis Sebugwao katika hafla ya kusherehekea mwaka mmoja kwa kampuni hiyo.Aidha kutokana na kipato hicho mgodi huo umeilipa Halmashauri ya Wilaya hiyo ushuru wa Sh milioni 40.9 ikiwa ni asilimia 0.3 ya mauzo yake kwa mwaka mmoja. Sebugwao alisema kuwa dhaha...
uchumi
MAJANGILI na wafanyabiashara wanaojihusisha na ujangili wa meno ya tembo na nyara za serikali katika mbuga za wanyama nchini, sasa watasakwa kwa kushirikiana na askari wa kimataifa (Interpol).Wizara ya Maliasili na Utalii nchini imewataka wale wote wanaojihusisha na uhalifu huo kujisalimisha mara moja, vinginevyo wata...
kitaifa
HATIMAYE Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Simba, Zakaria Hanspope ameweka kitanzini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) saa chache baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.Pope aliwasili nchini saa 7 usiku wa kuamkia jana na ndege ya KQ akitokea Marekani alikokuwa ak...
michezo
KATIKA kuongeza kasi ya kuchapisha vitambulisho vya Taifa, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inakamilisha mchakato wa kununua mashine mbili zenye uwezo wa kuchapa vitambulisho 9,000 kwa saa.Akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka ujao wa fedha bungeni, Waziri K...
kitaifa
MABAO sita aliyoyafunga mpaka sasa mshambuliaji wa Klabu ya Simba, Mnyarwanda, Meddie Kagere kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika yamemfanya avunje rekodi katika michuano hiyo iliyodumu kwa miaka mitano.Kagere kwa sasa anashika nafasi ya pili katika orodha ya ufungaji akiwa nyuma ya Moataz Al Mahd wa Al Nasr mwe...
michezo
TEZIDUME ni kiungo kidogo alichonacho kila mwanaume na huweza kukua na kuwasababishia maradhi hususani anapokuwa amefi kisha miaka 45 na kuendelea.Mbali na umri kuongezeka, sababu nyingine ya kukua kwa tezidume na kusababisha maradhi katika kiungo hicho ni pamoja na eneo hilo kushambuliwa kwa bakteria ama kupatwa na u...
kitaifa
JOZI milioni 40 za viatu zimekuwa zikiingizwa kila mwaka nchini huku uzalishaji wa ndani ukiwa ni jozi milioni 1.3 kiwango ambacho kinatakiwa kuongezeka ili kudhibiti soko la nje.Hayo yalibainishwa na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Bidhaa za Mifugo, Usalama wa Chakula na Lishe kutoka Wizara ya Mifugo, Gabriel Bura akifu...
kitaifa
KAMATI ya kuhamasisha uchangiaji Yanga imesema maandalizi kuelekea tamasha lao la kubwa kuliko Jumamosi yameiva na kuhimiza Wanayanga kufanya mchakato wa manunuzi ya tiketi mapema.Wakizungumza jana Dar es Salaam baadhi ya viongozi wa Kamati hiyo walisema tiketi zimeanza kuuzwa klabuni Yanga, Dar Live, Total Petrol Azi...
michezo
SERIKALI imeokoa Sh bilioni 9.01 katika kipindi cha mwaka 2018/19 ambazo zingelipwa kwa mawakili binafsi, waliokuwa wakitumiwa na ama wizara au taasisi za umma katika kuendesha kesi mbalimbali nchini.Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dk Augustine Mahiga (pichani) aliliambia Bunge jana kuwa hatua hiyo imekuja baada ya...
kitaifa
RAIS John Magufuli na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, wamewataka watumishi wa vituo vya mpakani, kufanya kazi zao kwa weledi na kujiepusha na rushwa.Walisema hayo walipozindua kituo cha forodha cha pamoja (OSBP) kilichopo Namanga mpakani mwa Tanzania na Kenya, huku wakibainisha kuwa hatua hiyo imelenga kuyainua kiuchumi...
kitaifa
WAKULIMA wa zao la alizeti nchini wameshauriwa kutumia mbinu za asili ili kukidhi vigezo vya kufi kia soko la kimataifa katika nchi za Ulaya na India.Ushauri huo ulitolewa jana na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Happines Mgalula, wakati wa ufunguzi wa warsha ya tathimini ya athari za mabadiliko ya tabianchi katika...
kitaifa
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Heritier Makambo amesema hajawahi kufi kiria tuzo ya ufungaji bora msimu huu, zaidi anawaza kuisadia timu yake kutwaa ubingwa.Makambo alisema kila anachokifanya uwanjani ni kwa ajili ya timu yake na atajituma ili kuisaidia kutwaa ubingwa msimu huu, kwani hajawahi kuwaza mafanikio binafsi kama ku...
michezo
SERIKALI mkoani Kilimanjaro imeelezea kukerwa kwake na Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, kupoteza hadhi yake ya kuwa kinara wa usafi miongoni mwa manispaa nchini kote kwa miaka 10 mfululizo.Katika hatua nyingine, serikali imemtaka Meya wa Manispaa ya Moshi, Raymond Mboya kuacha kuchanganya siasa na masuala ya utendaji...
kitaifa
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana, Igogo aliipongeza Serikali kwa kusikiliza kilio cha wafanyabiashara lakini alisema kuna haja ya Wizara ya Fedha kuunga mkono hatua hiyo.“Waziri wa Viwanda na Biashara hana mamlaka kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), bali Wizara ya Fedha hivyo uamuzi wa Dk Kigoda unapaswa...
uchumi
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameutaka uongozi wa mkoa wa Ruvuma uendelee kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo na kuondoa vikwazo vyote ili kuvutia wawekezaji zaidi.“Mkoa wa Ruvuma kama ilivyo mikoa mingine, unazo fursa ambazo zikiendelezwa, zitaleta tija na kusaidia kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi wa Taifa letu. Ni...
kitaifa
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia wakati wa ziara ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii waliokuwa wakitembelea miradi ya vikundi vilivyonufaika na fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya kuinua vijana.Miradi iliyokaguliwa juzi ni ya vikundi vitatu...
uchumi
Akizungumza na HabariLeo, Kaimu Msajli wa Michezo Ibrahim Mkwawa alikiri kumfungia Matuzya baada ya kushindwa kuwasilisha ripoti ya fedha ya Tasma licha ya kutakiwa kufanya hivyo mara kadhaa.Katika barua yenye kumbukumbu namba BMT/C.3/44/vol.3/21 iliyoandikwa Februari 15 na kusainiwa na Mkwawa na nakala kwa mwenyekiti...
michezo
Gama aliyasema hayo jana wakati akizungumza na wananchi wa mji mdogo wa Himo, kuhusu uwekezaji mkubwa utaofanyika katika eneo lao, hivyo kuwataka wawe tayari kukabiliana na maendeleo ya kisasa, kwa kutumia fursa hiyo bila kuzubaa.Alisema lengo la kuwataka wajiandae kisaikolojia, ni kutokana na miradi hiyo kuwa mikubwa...
uchumi
WACHEZAJI John Bocco, Meddie Kagere na Clatous Chama jana waliipa Simba ushindi muhimu wa mabao 4-1 dhidi ya Mbabane Swallows katika mechi ya kwanza ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.Matokeo hayo yanaiweka Simba kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele kwenye michuano ...
michezo
YANGA imekubali kipigo cha pili mfufulizo baada ya kufungwa na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana.Bao pekee katika mchezo huo lilifungwa dakika ya 26 baada ya kipa wa Yanga, Farouk Shikhalo kupangua kona iliyopigwa na Bruce Kangwa na mpira kuanguka miguuni mw...
michezo
BAADA ya kuisaidia Simba kufuzu hatua ya robo fainali, kiungo mchezeshaji Haruna Niyonzima ametoa hisia zake na kuahidi kuipigania timu hiyo ili kucheza fainali za Ligi ya Mabingwa Afrika.Katika mchezo wa mwisho wa makundi kwenye michuano hiyo ya Simba dhidi ya AS Vita uliochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita Dar es Sal...
michezo
Wajawazito zaidi ya milioni mbili walihudhuria na kuandikishwa kliniki katika kipindi cha mwaka jana, ikilinganishwa na wajawazito milioni mbili mwaka 2017.Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amewaeleza waandishi wa habari kuwa, mwongozo wa utoaji huduma za afya ya uzazi na mtoto,...
kitaifa
['Manchester United wanapenda kupata saini ya mshambuliaji wa Wolves Raul Jimenez, 28 na pia wanamtazama kwa karibu mshambuliaji wa Lyon Moussa Dembele, 23.(Sky Sports)', "Chelsea na Manchester United huenda wakakutana na kinyang'anyiro kikali kutoka kwa Juventus katika kumuwania Dembele. (Calciomercato - in Italian)",...
michezo
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeanzisha Kampeni ya Mtaa kwa Mtaa kuwafikia wananchi ili kutoa elimu ya matumizi ya mitandao na visimbuzi, ikiwa ni mkakati wa kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya kiteknolojia yanayotokea ili kuwe na upatikanaji wa huduma zisizo na matatizo kwa wananchi.Meneja wa TCRA Ka...
kitaifa
VIONGOZI wa vyama 10 vya upinzani wamevitaka vyama vingine vya upinzani kikiwamo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuheshimu sheria za nchi na kutokuwa na hofu na muswada wa vyama vya siasa kwani una lengo la kudhibiti fedha za ruzuku na fedha chafu zinazoingizwa nchini kwa kisingizio cha kusaidia upinzani....
kitaifa
SERIKALI imeongeza fedha za miradi ya maendeleo kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kutoka Sh trilioni 4.2 kwa mwaka 2018/2019 hadi Sh trilioni 4.8 kwa mwaka wa fedha 2019/2020.Hayo yalibainika wakati wa uwasilishaji wa bajeti ya wizara hiyo kulikofanywa na waziri mwenye dhamana, Isack Kamwelwe (pichani), bu...
kitaifa
Msanii huyo ambaye aliteka nyoyo za waamini wengi alipotea miaka ya hivi karibuni baada ya kukumbwa na misukosuko ikiwemo kashfa mbalimbali za utapeli, mbali na kuzindua albamu yake atapamba tamasha hilo ambalo linawahusisha wasanii mbalimbali wa muziki wa injili kutoka ndani na nje ya Tanzania.Mkurugenzi wa Msama Pro...
michezo
Pamoja na kuwahakikishia kuwepo kwa soko hilo, pia Serikali kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), kuanzia mwaka huu imetenga fedha za kununua mpunga tani 10,000, ikiwa ni hatua ya awali.Rais Kikwete alisema hayo wakati wa mkutano wa hadhara, uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mwaya kata ya Mw...
uchumi