content
stringlengths
1k
24.2k
category
stringclasses
6 values
CHAMA cha Wataalamu Wasaidizi wa Tiba na Afya ya Mifugo Tanzania (TAVEPA), kimebainisha kuwa Tanzania ndio nchi inayouza nyama kwa wingi katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa sasa.Kimeshauri kuwa kutokana na wingi wa soko hilo, ni wakati sasa sekta ya mifugo iboreshwe ili kuwawezesha wafugaji kujikwamua...
uchumi
MAMLAKA ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) imefafanua kuhusu vikokotoo vya pensheni ikisema vimeanza kutumika tangu 2014, kuwa kuunganishwa kwa mifuko ya hifadhi ya jamii hakujapunguza vikokotoo hivyo.Imesema kilichobadilika ni kiwango cha mkupuo kwa kundi dogo la wanachama takribani asilimia 20 ya wanac...
kitaifa
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ameridhishwa na ukarabati wa viwanja vitakavyotumika kwa mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika ‘Afcon’ kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi mwishoni mwa wiki hii.Mwakyembe alielezea kuridhishwa kwake baada ya jana k...
michezo
WAKATI sheria ikikataza utoaji mimba holela, imeripotiwa kuwa jumla ya mimba 405,000 zinatolewa nchini kila mwaka huku asilimia 40 kati ya hizo ikitolewa katika mazingira yasiyo salama.Kwa mujibu wa ripoti ya utafiti ya mwaka 2016 iliyotolewa na Taasisi ya Guttmatcher ya Marekani kwa kushirikiana na Taasisi ya Taifa y...
kitaifa
Benki ya CRDB imetangaza kuwa itakuwa mdhamini Mkuu wa Maonesho ya Pili ya Viwanda Mkoa wa Pwani.Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela ameushukuru uongozi wa mkoa huo kwa kuishirikisha benki hiyo, na kwamba, mwaka jana ilikuwa mdhamini mkuu wa maonesho ya kwanza ya viwanda mkoani humo.Mkuu wa Mkoa wa P...
uchumi
WAZIRI  wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Seleman Jafo ametoa siku sita  kupata taarifa ya kina kuhusu mradi wa kituo cha mabasi cha Mbezi Luis.Jafo aliyasema hayo leo akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa ofisi yake Magogoni Jijini Dar es Salaam na kudai kuwa iwapo h...
kitaifa
Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage wakati wa ufunguzi wa Mkutano na Maonesho ya Kibiashara ya Kimataifa ya Mauritius, yakilenga kujenga mahusiano na kutazama fursa za kibiashara baina ya mataifa haya mawili jijini Dar es Salaam jana.Alisema moja kati ya jitihada zinazofanywa na serika...
uchumi
SERIKALI mkoani Lindi imesema wakulima wote wa korosho ambao hawajalipwa pesa zao zilizosalia Sh bilioni 222.7, watalipwa fedha hizo ifikapo mwishoni mwa mwezi huu.Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amesema hayo mjini Lindi alipozungumza na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya kilimo na maji, wakulima na wataalamu wa kilimo, bo...
uchumi
WATOTO wenye umri wa kati ya miaka minne na 16 wanaoishi na kufanya kazi katika Mitaa ya Mji wa Sumbawanga mkoani Rukwa wamekuwa tishio kwa wakazi wa mji huo wakituhumiwa kwa uhalifu.Inadaiwa kuwa watoto hao wa kike na kiume katika umri huo mdogo ambao baadhi yao wameishi na kufanya kazi katika mitaa ya mji huo ambao ...
kitaifa
MSHAMBULIAJI wa Simba, John Bocco amekiri kuwa kushindwa kutumia nafasi za kufunga walizozipata katika eneo lao la ushambuliaji ni moja ya sababu iliyowafanya kushindwa kuondoka na pointi tatu katika mechi yao dhidi ya Lipuli juzi.Simba ilishindwa kutakata katika mechi hiyo iliyopigwa juzi Uwanja wa Taifa, Dar es Sala...
michezo
KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema ni bahati mbaya kumkosa mlinzi wake, Erasto Nyoni kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika dhidi ya JS Souara unaotarajiwa kuchezwa keshokutwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Akizungumza baada ya kurejea Dar es Salaam jana, Aussems alisema ni pigo kumkosa kiraka huyo, amb...
kitaifa
Akikabidhi hundi hiyo mjini Dodoma jana kwa Waziri wa Fedha, Saada Mkuya, Ofisa Mkuu wa Fedha wa NMB, Waziri Barnabas alisema gawio hilo ni ongezeko la asilimia 16 ukilinganisha na mwaka jana.Alisema mwaka huu benki hiyo imepata faida ya Sh bilioni 155.6 ambapo kila mwanahisa amepata gawio la Sh 104 kwa kila hisa tofa...
uchumi
SERIKALI imeweka mkakati wa kupanda miti milioni 280 kati ya mwaka 2016/20 katika maeneo mbalimbali nchini. Kauli hiyo aliitoa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Costantino Kanyasu wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Same, Magharibi, Nagenjwa Kaboyoka (Chadema).Mbunge huyo alitaka kujua kama serikali inawe...
kitaifa
SERIKALI imeteua Wilaya za Kongwa na Dodoma kuwa vituo vikuu vya kumbukumbu za ukombozi wa nchi, ambako miundombinu ya uhifadhi wa kihistoria itajengwa na kuhifadhiwa kumbukumbu mbalimbali zikiwemo kazi adhimu za Baba wa Taifa, Julius Nyerere.Aidha, serikali kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sa...
kitaifa
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta ‘Samagoal’ ameshinda tuzo ya mchezaji Bora Mwafrika katika Ligi ya Ubelgiji maarufu ‘Jupiler Pro League’.Samatta anayecheza katika klabu ya KRC Genk nchini humo alishinda tuzo hiyo iitwayo Kiatu cha Ebony katika sherehe za tuzo za Jupiler Pro League zilizofanyika u...
michezo
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) inakusudia kuanzisha sera ya viwango ambayo miongoni mwa majukumu yake makubwa ni kuweka viwango vitakavyokubalika kwa bidhaa zinazoingia nchini na zile zinazozalishwa ndani.Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda, Hassan Khamis Hafidh amesema hatua hiyo ni muhimu itakayodhibiti uin...
uchumi
Wakizungumza jana kwa nyakati tofauti, baadhi ya maofisa wa migodi ya madini nchini walisema kuna changamoto kadhaa ambazo zimechangia wawekezaji katika sekta ya madini kutowekeza kwenye utafutaji wa madini jambo ambalo linaweza kuifanya sekta hiyo kufa au kudumaa.Mwenyekiti wa Chama cha Madini na Nishati, Balozi Ami ...
uchumi
\SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema utaratibu wa utoaji wa vitambulisho vya taifa ni muhimu kwa sababu pamoja na mambo mengine utasaidia kupambana na kudhibiti uhalifu nchini.Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Khalid Salum Mohamed wakati akifungua Jengo la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ...
kitaifa
SHULE 11 zenye upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, zimetakiwa kukamilisha ujenzi wa madarasa ili wanafunzi wa awamu ya pili waanze masomo Februari 2, mwaka huu.Akipokea taarifa ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma iliyosomwa na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, Hidaya Maeda, Mkuu wa Mkoa h...
kitaifa
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Ephraim Mafuru alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akizindua shindano la kuwazawadia Watanzania kwa kuwapa fursa mbalimbali na zawadi ambazo zinagharimu Sh bilioni 1.2.Katika kuendesha shindano hilo, kampuni hiyo imeshirikiana na wataalamu wa teknolojia Bpesa, am...
uchumi
KOCHA wa Simba, Patrick Aussems ameanza kuwahofi a wapinzani wake katika mchezo ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Mbabane Swallows akisema hautakuwa mchezo rahisi.Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Novemba 27, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na ule wa marudiano utachezwa Desemba 4, nchini eSwatini. Akizun...
michezo
KOCHA wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila amesema baada ya kungo’olewa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), hasira zao wanahamishia kwenye michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara. Mtibwa ambao ni mabingwa wapya wa Kombe la Mapinduzi kwa mwaka 2020, walitolewa kwa mikwaju ya Penalti 2-3 dhidi ya Sahare All Star...
michezo
KOCHA wa Lipuli FC, Selemani Matola amejipanga vya kutosha, akijinadi kuwa anafahamu afanye vipi ili aondoke na pointi tatu ugenini leo dhidi ya Azam FC iliyo chini ya Mdachi, Hans van Der Pluijm.Lipuli inayotokea Iringa inatarajia kucheza mechi hiyo ya pili mfululizo jijini Dar es Salaam baada ya juzi kucheza dhidi y...
michezo
SPIKA wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Zubeir Ali Maulid amesema michezo ni moja ya sehemu ya afya zao na kitendo cha kutoka na kucheza michezo ni kwamba wanahamasisha kuimarisha afya zao.Zubeir aliyasema hayo katika hafla ya kukabidhiwa vifaa vya michezo na Benki ya NMB huko katika ukumbi wa mikutano wa Baraza la W...
michezo
WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika anatarajia kuzindua mkutano wa siku mbili leo Jijini Arusha, utakaojumuisha makatibu mahsusi zaidi ya 2,300 wa nchini.Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini hapa, Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) Zuhura ...
kitaifa
Balozi Eralp alisema juzi mjini hapa kuwa, sekta ya utalii ni kipaumbele chake cha kwanza, hivyo atakahikisha fursa za uwekezaji katika utalii zinafahamika kwa watu wa nchi yake, ili ‘wazichangamkie’ kwa kuwekeza. Alisema hayo wakati alipokutana na viongozi wa Shirika la Hifadhi ya Taifa (TANAPA), alipotembelea makao ...
uchumi
SERIKALI imetaka wakuu wa shule za sekondari na vyuo vikuu mkoani Kilimanjaro, kuandaa utaratibu maalumu ambapo wahitimu wa taaluma mbalimbali, hawatatunukiwa vyeti vyao bila kwanza kupanda Mlima Kilimanjaro.Mpango huo umelenga kuhamasisha utalii wa ndani lakini pia kuongeza mapato, jambo ambalo litasaidia uimarishwaj...
kitaifa
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara Simba wanatarajiwa kushuka dimbani leo kuwakaribisha Alliance ya Mwanza kwenye uwanja wa Taifa.Simba imetoka kupata ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo uliopita dhidi ya Stand United huku Alliance ikitoka kupata kichapo kama hicho kutoka kwa Yanga. Mchezo wa leo una umuh...
michezo
WAZIRI wa Maji, Profesa Makame Mbarawa amemsimamisha kazi Mhandisi wa Maji Mkoa wa Rukwa, Emmy George baada ya kutofurahishwa na maendeleo ya Mradi wa Maji wa Isale wilayani Nkasi.Wakati huo huo, Profesa Mbarawa ameagiza mkandarasi wa Kampuni ya Enterprises akamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya dola kwa kosa la uda...
kitaifa
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewaonya wananchi kutosajili laini zao kwa mfumo mpya wa alama za vidole kwa kutumia maduka ya mtandaoni (Application), bali wahakikishe wanasajiliwa na mtoa huduma wa mawasiliano.Imewataka pia kutumia fursa ya Kampeni ya Mnada kwa Mnada ili kupata huduma ya utatuzi wa matatizo ...
kitaifa
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, leo anatarajiwa kufungua Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji mkoani Tabora. Hii ni mara ya kwanza Jukwaa hilo kupata hadhi ya kufunguliwa na Waziri Mkuu Majaliwa.Waziri Mkuu Majaliwa anatarajia kuwasili leo mjini Tabora na kwenda moja kwa moja kufungua Jukwaa hilo litakalofanyika kat...
kitaifa
Mkutano huo utakaofanyika Bagamoyo, unalenga kujadili ni namna gani nchi za Afrika zitaondokana na kuuza nje bidhaa ghafi ambazo zinazipatia nchi hizo fedha kidogo za kigeni.Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kukuza na Kuchochea Ushindani wa Maendeleo Barani Afrika (PACF) Profesa Burton Mwamila, alisema mkutano huo umeandaliwa ...
uchumi
MKUU wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi amesema wameweza kuokoa takribani Sh milioni 400 zilizokuwa kwenye msingi wa udanganyifu katika ulipaji wa fi dia maeneo mbalimbali.Katambi alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari na kusisitiza kuwa katika ulipaji wa fidia maeneo mbalimbali katika jiji la Dodoma, im...
kitaifa
JANA umati mkubwa wa wananchi ulilipuka kwa shangwe na chereko wakati Rais John Magufuli alipowasili katika uwanja wa michezo wa Loftus Versfeld jijini Pretoria kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa 5 wa Afrika ya Kusini, Cyril Ramaphosa.Sherehe hizo ambazo zilijaa mbwembwe za aina yake na kurushwa na televishen...
kitaifa
KLABU ya Yanga imewatuliza mashabiki wake kufuatia kutolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikisema kazi haijaisha wanajipanga upya kwa ajili ya Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho Afrika. Yanga imetolewa na Zesco United ya Zambia kwa jumla ya mabao 3-2, wakitoka sare nyumbani ya bao 1-1 na kufungwa ugenin...
michezo
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameweka jiwe la msingi mradi wa maji wa Imalabupina/ Ichwankima wilayani Chato, ambao una thamani ya Sh bilioni 8.28 na amewaagiza viongozi wa wilaya hiyo wahakikishe unakamilika kwa wakati.Amesema serikali kupitia kampeni ya Rais John Magufuli ya kumtua mama ndoo kichwani, itahakikisha wa...
kitaifa
*JANA sehemu ya kwanza ya makala haya ilieleza mbinu zinazotumiwa na baadhi ya wafanyabiashara  kukwepa kodi sambamba na madhara yaliyowakumba baadhi ya wateja waliochukua bidhaa kwa wafanyabiashara hao. Endelea.Ikumbukwe, katika taarifa iliyosoma Oktoba Mosi mwaka huu na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania...
uchumi
KOCHA wa timu ya Simba, Patrick Aussems amesema wapinzani wao TP Mazembe kutoka Congo DR walikuwa bora miaka mitatu iliyopita hivyo kikosi chake bado kinanafasi ya kuendelea kuwashangaza watu kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.Aussems ametoa kauli hiyo baada ya droo ya hatua ya robo fainali ya michuano hiyo il...
michezo
WAZIRI wa Nchi Ofi si ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, vijana na walemavu Antony Mavunde amesema vijana 700 kutoka wilaya saba za mkoa wa Dodoma watapatiwa mafunzo juu ya kutengeneza kitalu nyumba (green house).Alisema hayo mwishoni mwa wiki katika kijiji cha Nzali Kata ya Chilonwa Wilaya ya Chamwino wakati w...
kitaifa
Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Kilimo na Maliasili, Mtumwa Mbarouk wakati akijibu na kutoa ufafanuzi wa baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliotaka kujua ubora wa miche ya mikarafuu inayozalishwa katika kituo cha Kizimbani.Alisema miche hiyo kwanza inafanyiwa utafiti katika maabara ...
uchumi
MHADHIRI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kutoka Idara ya Sayansi ya bahari na teknolojia ya uvuvi, Samwel Limbu kwa miaka miwili ya masomo nchini China, amekuwa mwanafunzi bora wa kimataifa katika Chuo cha East China Normal University (ECNU).Limbu amekuwa mwanafunzi bora wa kimataifa kwa mwaka wa masomo 2015/16...
kitaifa
SIMBA ipo tayari kulipa faini ya dola za Marekani 500 ili kuinasa saini ya mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi.Okwi anayefanya vizuri kwenye michuano ya Mataifa ya Afrika, Afcon 2019, akiwa na timu yake ya Taifa, mjini hapa, anamaliza mkataba Simba na hakutaka kuongeza mwingine akidai kutaka kutafuta ch...
michezo
BUNGE limelisifia Jeshi la Polisi kutokana na kufanya vizuri katika makusanyo ya maduhuli kwa asilimia 131.6 ya lengo, huku Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ikikusanya maduhuli kwa asilimia 78.6 ya lengo ililopangiwa.Mafanikio hayo yamo kwenye Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati kwa kipindi cha Februari mwaka jana ...
kitaifa
Taarifa iliyotolewa jana ilisema kuzinduliwa kwa tawi hilo, kumeongeza wigo wa matawi yanayoendelea kusambaa nchi nzima kwa lengo la kurahisisha huduma kwa wateja wao.Taarifa hiyo ilisema NMB inajivunia kuongoza kwa kuwa na matawi megi zaidi nchini na mashine za kutolea fedha (ATM) zaidi ya 500, zilizosambaa nchi nzim...
uchumi
.Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula,  ameitaka halmashauri ya wilaya ya Mafia mkoani Pwani kuandaa mazingira ya  kupokeaWawekezaji katika sekta ya utalii kwa kupanga na kupima maeneo yake.Dkt Mabula ametoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti, baada ya kusikiliza kero za migogoro ya ardh...
uchumi
KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa, Taifa Stars, Emmanuel Amunike amesema leo Tanzania inafungua ukurasa mpya dhidi ya Algeria katika mechi yao ya mwisho ya Kundi C kwenye michuano ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, Afcon 2019.Stars inamenyana na Algeria katika mechi ya kukamilisha ratiba kwani haina nafasi ya...
michezo
Washindi waliokabidhiwa magari ni pamoja na Hamim Yoyo mfanyakazi wa saluni kutoka Korogwe mkoani Tanga, Edson Mwansasu mkulima kutoka Kyela, Ester Mashauri muuguzi wa Hospitali ya Bugando jijini Mwanza na Sakina Libwana mamalishe kutoka jijini Dar es Salaam.Hafla ya kuwakabidhi magari hayo kila mmoja ilifanyika jana ...
uchumi
MTENDAJI Mkuu mpya wa Simba, Senzo Mazingiza ametambulishwa rasmi jana na kuahidi kuifanya klabu hiyo kuwa kubwa zaidi Afrika na duniani. Mazingiza anatarajiwa kuanza kazi mara moja baada ya kukamilika kwa kibali cha kuishi nchini, huku akiwa tayari amekamilisha kibali cha kufanya kazi nchini akichukua nafasi ya aliye...
michezo
Hayo yalisemwa na Mwakilishi wa Chumbuni, Machano Othman Said wakati akichangia bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017 na kusema kufuatia udanganyifu unaofanywa na wanunuzi wa zao hilo umepelekea kushuka bei ya mwani kwa kiwango kikubwa.Alisema bei ya mwani imeshuka kwa kiwango kikubwa kutoka Sh 700 hadi kufi...
uchumi
MRAKIBU Mwandamizi wa Polisi, Gerald Ngiichi ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa aliamuru askari kupiga mabomu ya moshi na risasi za moto hewani kwa ajili ya kusambaratisha maandamano ya viongozi na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).Alidai katika maandamano hayo yaliyofanyika Februari 1...
kitaifa
Watumiaji hao katika mikoa mitatu ya Mwanza, Tabora na Shinyanga waliyasema hayo kwa nyakati tofauti walipozungumza na mwandishi wa habari hizi baada ya kuelimishwa na mabalozi wa M-Pawa namna ya kunufaika na huduma hiyo. Aidha wananchi wa Morogoro pia wamefikiwa na huduma hiyo.Mara baada ya uzinduzi wa kampeni hiyo a...
uchumi
['Kiungo wa kati wa Real Madrid na Ujerumani Toni Kroos, 29, huenda akahamia Manchester United kama sehemu ya mkataba wa kumpeleka Paul Pogba, 26, katika klabu hiyo ya Uhispania. (Sun)', 'Juventus inapani akumpatia kiungo wa Ufaransa Adrien Rabiot, 24, katika makubaliano ya kubadilishana wachezaji na pesa kwa mchezaji ...
michezo
BENKI ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) imewataka wakulima na wafugaji nchini kutumia muda Maonesho ya Nanenane ambayo yanafanyika kitaifa ya mkoani Simiyu, kujifunza na kuchangamkia fursa za mikopo na inayotolewa na benki hiyo kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao kilimo.Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, mba...
uchumi
SERIKALI imesema kampuni 22 kutoka nchini Misri zimewekeza nchini zaidi ya Dola za Marekani milioni 900 sawa na Sh trilioni 2.068 hali iliyosaidia kuongeza ukuaji wa biashara na uchumi.Aidha, biashara kati ya Tanzania na Misri imekua kwa asilimia 75 baada ya Misri kuingiza nchini, bidhaa mbalimbali zenye thamani ya Do...
uchumi
JESHI la Polisi mkoani Pwani limetakiwa kumkamata mtu anayejiita Nabii Eliya ambaye jina lake ni Hamza Issa anayetuhumiwa kufanya mahubiri ambayo yanaweza kuhatarisha amani kwa jamii.Aidha, Nabii Eliya ambaye anadaiwa kuwa anawafanyia maombi watu wenye matatizo amewakusanya wanawake wengi ambao ndiyo waumini wake waku...
kitaifa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Uledi Mussa amesema usajili huo mpya, utachochea na kurahisisha shughuli za biashara. Alisema hayo jana wakati akifungua mkutano wa wadau wa Brela juu ya usajili wa jina la kampuni kwa njia ya mtandao.“Tumeamua kuboresha huduma zetu kwa kuanzisha mradi huu ili kusaidia wat...
uchumi
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amekamata jumla ya kilo 26,295 za bidhaa za nyama na maziwa zikiwa zimeingizwa nchini kutoka nje ya nchi bila kuwa na vibali, kulipiwa ushuru na bila kuhakikiwa ubora wake.Kutokana na sakata hilo, amebainisha kamwe serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Magufuli hai...
kitaifa
Hayo yalibainishwa Dar es Salaam jana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage alipofungua programu ya mafunzo maalumu ya wajasiriamali wanaoagiza nishati ya mafuta, yaliyoandaliwa na First National Bank (FNB).Mafunzo hayo yanahusu namna ambavyo wagizaji mafuta, wanaweza kupata dhamana za benki na kulipa ...
uchumi
WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeeleza sababu ya kutotekeleza sera ya wanafunzi kuishia darasa la sita na kusema ni busara iliyowajia upya ikionesha kuishia darasa la saba siyo vibaya.Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha, William Ole Nasha alisema hayo leo Jumatano wakati akijibu mas...
kitaifa
Kadhalika, serikali imetakiwa kudhibiti matumizi ya dola nchini, hatua ambayo itasaidia kuimarisha thamani ya Shilingi ambayo kushuka kwake kunasababisha bidhaa zinazoingia nchini kupanda bei.Akichangia Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2025/16, Mbunge wa Mwibara (CCM), Kangi Lugola, alisema kuachwa kwa nchi yetu ...
uchumi
UJENZI wa Stendi Kuu ya Mabasi mkoani Njombe imekamilika ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli alilolitoa Aprili 10, mwaka huu, alipofanya ziara ya kazi mkoani humo.Akiwa mkoani humo, aliagiza stendi hiyo ikamilike ifikapo Mei 10, mwaka huu yaani jana, badala ya Aprili 30, mwaka huu kama Naibu Waziri, Of...
kitaifa
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge ameuelekeza uongozi wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA), kuweka mikakati ya kumaliza msongamano hasa katika barabara ya kuelekea Dar es Salaam.Dk Mahenge alitoa agizo hilo jijini hapa jana wakati wa ziara ya kukagua miundombini ya barabara zinazozunguka Jiji...
kitaifa
MSHAMBULIAJI wa Simba, John Bocco, amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Aprili wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2018/2019.Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Cliford Ndimbo amesema Bocco ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda Emmanuel Okwi wa Simba na Heritier Makambo wa Yanga alioingia nao fainali.“Kwa ...
michezo
Hatua hiyo ni utekelezaji wa diplomasia ya uchumi inayomtaka kila balozi kutafuta masoko ya bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.Katika ziara yake katika kiwanda cha PCT juzi mjini hapa, Balozi huyo alisema, “nilikuja nchini na wafanyabiashara na wawekezaji 65, wametembelea sehemu mbalimbali za uwekezaji bara na visiwani...
uchumi
MLEZI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya mkoa wa Kusini Pemba, Makongoro Nyerere amewataka wanachama wa chama hicho kuimarisha mshikamano ambao utakifanya chama hicho kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu mwakani.Makongoro aliyasema hayo wakati alipozungumza na viongozi na wanachama wa CCM wilaya ya Mkoa...
kitaifa
Pia ametaka uongozi wa kampuni hiyo kushirikiana na vyombo vya habari, kutangaza mazao yanayozalishwa na mgodi huo, kuwezesha kuvutia wakopeshaji na wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.Aliyasema hayo leo wakati akizindua mkupuo wa kwanza wa uzalishaji wa dhahabu wenye uzito wa kilogramu 25 wenye thamani ya Sh bilioni 1...
uchumi
TANZANIA imepongezwa kutokana na uamuzi wa kuunda mabaraza ya kiswahili ambayo ni Bakita kwa Tanzania Bara na Bakiza kwa Zanzibar ambayo kimsingi yanasaidia katika masuala ya sera ya lugha ya Kiswahili.Pongezi hizo zilitolewa na Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki (EACK) Profesa Kenneth Simal...
kitaifa
Pia imepandisha kiwango cha ushuru wa huduma za mawasiliano kutoka asilimia 14.5 hadi asilimia 17 ambapo itaanza kulipwa kuanzia Januari mwakani.Hatua hiyo imefuatia Rais Jakaya Kikwete kutokusaini muswada huo wa sheria hivyo kusababisha kuletwa tena bungeni kwa hati ya dharura ambapo wabunge wote waliipitisha huku wa...
uchumi
VISIWA viwili vikubwa vya Zanzibar vya Unguja na Pemba na vingine vidogo vidogo takribani 20 vilikuwa na mvuto na historia ya kipekee tangu karne ya 11. Hivyo wageni wengi wakiwemo Waarabu, Wahindi, Wazungu n.k walifika Zanzibar kwa ajili ya biashara.Walipofika visiwani humo, wengi waliamua kutorudi kwao, wakaanza kuo...
kitaifa
['Manchester United huenda wakamnunua mshambuliaji wao wa zamani Muargentina Carlos Tevez,35, ambaye kwa sasa anachezea Boca Juniors. (Tuttosport)', 'Tottenham wamekubali kuiuzia Inter Milan kwa euro milioni 20 (£16.8m) kiungo wao wa kati Christian Eriksen, 27. (Sempreinter.com)', 'Hata hivyo, Barcelona wanataka kumsai...
michezo
MKAKATI wa kuhifadhi faru Tanzania utakaogharimu Sh bilioni 134.2 unakusudia katika kipindi cha miaka mitano kuongeza idadi ya faru weusi kutoka 161 waliopo mwaka huu hadi zaidi ya 205 ifi kapo 2023.Akizindua mkakati huo jijini Dodoma jana, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla alimtaka Katibu wa Wizara...
kitaifa
MWANAFUNZI aliyekuwa akisoma katika Shule ya Msingi Sintali, Kata ya Sintali wilayani Nkasi mkoani Rukwa, Exavery Mwananjela (5) amekufa baada ya kuanguka na kichwa chake kuzama kwenye chungu cha maharage yaliyokuwa yakichemka jikoni.Mtoto huyo alikuwa akisoma darasa la kwanza katika shule ya Msingi Sintali inasemekan...
kitaifa
MKUU wa Wilaya ya Chemba, Saimon Odunga amesema kesho watazindua utaratibu wa ugawaji wa vitambulisho vya wajasiriamali baada ya kupitisha vigezo ambavyo wanaona wanaweza kupata wajasiriamali.Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, Odunga alisema sifa ambazo zimewekwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekuwa n...
kitaifa
Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum alisema hayo jana wakati wa mkutano ulioandaliwa na Serikali na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa nchi za Ghuba kujadili uwekezaji nchini.Katika mkutano huo wa siku mbili uliohudhuriwa pia na wawekezaji kutoka nchi za Ujerumani, Marekani, maofisa wa serikali na wawekezaji wa ndani na nje...
uchumi
Mkurugenzi Mwendeshaji wa benki hiyo, Margreth Chacha, aliwaambia waandishi wa habari mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam kuwa katika kipindi cha chini ya miaka minne tangu benki hiyo ianzishwe, maelfu ya wajasiriamali wanawake na vijana wameshanufaika na mikopo ya kuendeleza biashara zao.“Mikopo yetu kwa wajasiria...
uchumi
AZAM FC imeendelea kusonga mbele mdogo mdogo katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya jana kuifunga Kagera Sugar kwa bao 1-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.Bao hilo pekee katika mchezo huo, lilifungwa na Donald Ngoma katika dakika ya 40, limeiwezesha Azam FC kufikisha pointi 30 na kuj...
michezo
RAIS wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dk Akinwumi Adesina ameipongeza Tanzania kwa ukuaji mzuri wa uchumi wa wastani wa asilimia 7 kwa mwaka na hivyo kuendelea kuwa miongoni mwa nchi zenye uchumi unaokua kwa kasi kubwa duniani.Dk Adesina alitoa pongezi hizo juzi usiku Ikulu jijini Dar es Salaam, baada ya kukuta...
kitaifa
['Kiungo wa Real Madrid, Dani Ceballos,22, karibuni kujiunga na Arsenal. (Mundo Deportivo)', 'Kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen,27, ni moja ya majina yaliyowekwa wazi na Atletico wakiwa wanatazamia kumsajili mchezaji huyo. (Evening Standard)', 'Mlinzi wa kushoto wa timu ya taifa ya England Danny ...
michezo
MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amewataka wafanyabiashara wadogo kulipia na kuchukua vitambulisho maalumu vilivyotolewa na serikali kwa ajili yao vinginevyo vitahesabika kuwa ni wafanyabiashara wakubwa wanaopaswa kulipia kodi.Hatua itasaidia kuwatambua na kuepusha usumbufu wakati wa kufanya shughuli zao za kujilet...
uchumi
MABINGWA wa Tanzania Bara msimu wa mwaka 2018/19, Simba jana walishindwa kukabidhiwa Kombe lao la Ligi Kuu Tanzania Bara licha ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuahidi kuwakabidhi.Mchezo huo ambao ulizikutanisha Simba na Biashara ya Musoma, ulichezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na ulianza saa 9:00 ...
michezo
MASUALA mbalimbali, yakiwemo tisa yaliyokuwa yamewekwa pembeni, katika mradi wa kusafi risha mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda mpaka Tanga nchini Tanzania, yatafi kiwa makubaliano baina ya pande hizo katika kikao, kitakachofanyika mwishoni mwa mwezi huu.Aidha, mkataba wa utekelezaji wa mradi, unatarajiwa kukamil...
kitaifa
KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema baada ya kushindwa kupata matokeo mazuri katika mechi mbili zilizopita, vita yao inahamia kwa Mtibwa Sugar na Ndanda wakiwa na matumaini ya kufanya vizuri.Katika mchezo wa juzi uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, wekundu hao wa Msimbazi walilazimishwa suluhu dh...
michezo
Akizungumza katika hafla ya utiaji saini mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Mizinga Melu alisema hiyo inahitimisha safari ya majadiliano na kampuni mama ya Star Oils, Mohammed Entrepries Tanzania Limited (METL) ya mkopo wa Sh bilioni 100."Star Oils ni kampuni dada ya METL ni moja ya ka...
uchumi
ILI kukabiliana na uharibifu wa mazingira, mdau wa mazingira ameanzisha kiwanda cha kutengeneza mkaa mbadala wilayani Bunda, ambao utauzwa kwa bei nafuu kwa watumiaji. Kiwanda hicho, Charcoal Investments kitasaidia kukabili uharibifu wa mazingira. Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Eliphas Mollel, mkazi wa wilayani Bunda al...
kitaifa
WANAFUNZI nchini wameshauriwa kujiamini na kutumia fursa ya masomo wanayopata huku wakisoma kwa bidii ili kujitambua na kuepukana na adha mbalimbali ikiwemo ukatili na manyanyaso.Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na kijana Brian Chandrabose, kutoka kampuni ya Fortune and Friends inayojishughulisha na kuandaa programu ...
kitaifa
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) kupitia mradi wa pamoja wa mashirika 16 limezikabidhi kwa halmashauri nne za mkoa Kigoma shilingi milioni 430 kwa ajili ya kukopesha  kwa vikundi vya wanawake kusaidia mkakati wa serikali wa kupambana na umasikini na kusaidia makundi maalum. Mchambuzi wa mipang...
kitaifa
TANZANIA imekuwa nchi ya kwanza barani Afrika kupata ngazi ya tatu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa mifumo bora ya udhibiti wa dawa kupitia Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA).Kwa hali hiyo, TFDA imeingia miongoni kwa asilimia 30 ya taasisi zote za udhibiti wa dawa duniani na imebakiza ngazi moja ya juu inayotolewa ...
kitaifa
KOCHA wa Rayon Sports Janvier Martinez Espinosa amewataka wachezaji wake kusahau matokeo yaliyopita dhidi ya Gasogi United na kufanya kweli katika mchezo wa leo wa uzinduzi wa Ligi Kuu ya Ewanda.Rayon Sports Jumamosi ililazimishwa suluhu dhidi ya Gasogi United na hivyo inataka matokeo katia mchezo wa leo. Mabingwa hao...
michezo
KOCHA Mkuu wa timu ya Soka ya Tanzania Bara,- Juma Mgunda amesema idadi ndogo ya wachezaji kwenye michuano ya kombe la Chalenji ni moja ya sababu iliyochangia kushindwa kufanya vizuri.Akizungumza jana baada ya kushuka Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere , Mgunda alisema alikuwa na kikosi chenye wachezaji 20...
michezo
Alikuwa mshambuliaji Mohammed Ibrahim Mo aliyeamsha shangwe, vifijo na nderemo za mashabiki wa Simba kwa bao la ushindi. Mo alifunga penalti ya tano kwa Simba na kuhitimisha upigaji penalti ulioiacha Yanga ikiishia kupata penalti nne.Pamoja na kuanza kupiga penalti huku Simba ikimalizia, Yanga ilikosa fursa ya kubeba ...
michezo
BAADA ya kucheza na Mashujaa juzi, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba leo watakuwa tena kwenye uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma kucheza na mabingwa wa Burundi Aigle Noir katika mchezo wa kirafi ki.Hiyo ni mechi ya pili kwa Simba kucheza kweny uwanja huo baada ya juzi kucheza na timu ya daraja la kwanza ya Mashu...
michezo
KAMPUNI ya Tanzania Breweries Limited kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Kitengo cha Dawati la Jinsia imeungana na mashirika yanayopinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na kutetea haki za binadamu, kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto.Maadhimisho hayo yalioanza wiki hii, huandaliw...
kitaifa
BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limelaani upungufu mkubwa katika usimamizi wa ukusanyaji na utupaji taka na kuzitaka serikali za mitaa zisimamie kikamilifu utupaji wa aina zote za taka.Pia baraza hilo limehimiza urejelezaji wa taka ngumu kwa manufaa ya taifa. Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dk Sa...
kitaifa
Aidha, serikali imeshauriwa kuangalia upya utaratibu wa kutoa misamaha ya kodi, hasa kwa kampuni kubwa zisizohitaji msamaha huo, kuwezesha kuongeza pato la Taifa kama Watanzania wanavyobanwa kulipa kodi katika mataifa ya nje waliomo.Hayo yalisemwa juzi na Mjumbe Kadari Singo, wakati akichangia mjadala wa Rasimu ya Kat...
uchumi
['Joao Felix sasa ndiye mchezaji ghali zaidi mwenye umri mdogo duniani baada ya kujiunga na Atletico Madrid kutoka Benfica kwa dau la £113m.', 'Pia ametajwa kuwa mchezaji mahiri zaidi kutoka Portugal baada ya Cristiano Ronaldo.', 'Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 alianza kuichezea Benfica mwanzoni mwa msimu wa 201...
michezo
SHIRIKA la Habari la China, Xinhua na Kampuni ya Magazeti ya Serikali Daily News, Habari Leo (TSN), zimeaidi kudumisha ushirikano ikiwa ni pamoja na kuendeleza programu ya lugha ya Kiswahili kwa Wachina.Hayo yalisemwa jana na Mhariri wa HabariLeo, Nicodemas Ikonko wakati akimkaribisha Mhariri Mkuu wa Shirika la Habari...
kitaifa
['Pazia la Ligi Kuu ya England, maarufu kama Ligi ya Primia msimu wa 2019/2020 linafunguliwa rasmi hii leo.', 'Msimu uliopita 2018/2019 ulikuwa ni moja ya misimu bora na wenye ushindani wa hali ya juu, mambo yatakuwaje kwenye msimu mpya. ', 'Mshindi wa Primia msimu uliopita Manchester City na mshindi wa Ligi ya Mabingw...
michezo
Hayo yameelezwa na Ofisa Masoko wa PSPF, Rahma Gemina Ngassa wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya Utumishi wa Umma katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Kaimu Katibu Mkuu ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi, Habu Mkwizu kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi.Anasema...
uchumi
Akipokea ndege hiyo, alisema kuwa kuna matumaini makubwa ya Shirika la Ndege la Taifa kufanya vizuri zaidi katika utoaji wa huduma za usafiri wa anga, ikizingatiwa kuwa shirika lina mkakati madhubuti wa upanuzi wa huduma zake ambao utekelezaji wake umeanza.“Ndege tuliyoipokea leo hii, ni sehemu ya ndege tatu tulizopan...
uchumi
Rai hiyo ilitolewa juzi na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sofia Simba wakati akizindua kampeni ya Wanawake na Uchumi inayoendeshwa na Kampuni ya kusaidia wanawake ya Angels Moment mjini hapa.“Wanawake nawaomba mbadilishe mfumo wa kufanya biashara, weka rekodi hata kama una Bajaj ujue kiasi gani kimein...
uchumi