content
stringlengths
1k
24.2k
category
stringclasses
6 values
NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu amesema wizara hiyo inatarajia kuja na mkakati maalumu wa kutangaza utalii ndani na nje ya nchi kwa kunadi maeneo ya vivutio vya utalii badala ya kuinadi nchi kwa ujumla na vivutio vyake.Pia amesema maeneo hayo yatakuwa yakinadiwa kwa mfumo wa vifurushi hali ita...
uchumi
WATAALAMU wa afya wameshauri wazazi kuacha kuwapa watoto wao vyakula vyenye sukari ili kupunguza ongezeko la ugonjwa wa kisukari kwa watoto wadogo.Vyakula ambavyo wazazi wanatakiwa kuepuka kuwapa watoto ni pamoja na chipsi, baga, soseji na vile vyenye mafuta mengi, sukari nyingi, ikiwemo vinywaji kama soda, juisi za v...
kitaifa
['Unai Emery amedokeza kuwa alikaribia kumsajili kiungo wa kati wa Liverpool na raia wa Brazil Fabinho, 26, alipojiunga na Arsenal kama kocha mkuu mwaka jana. (Evening Standard)', 'Manchester City imeongeza juhudi za kumsaka kiungo wa kati wa Napoli na Uhispania Fabian Ruiz, 23, na pia ilituma wataalamu wake kufuatili...
michezo
MADHARA ya mama mjamzito asiyekuwa na kinga au kupata chanjo ya ugonjwa wa rubella, husababisha kuzaa watoto wenye matatizo ya matundu kwenye moyo, fi go na hata kuwa na shida ya viungo.Dalili za ugonjwa wa rubella hazina tofauti na za ugonjwa wa surua, ambapo mtoto huanza kwa kupimwa kwanza surua kisha kupatiwa chanj...
kitaifa
MSHAMBULIAJI wa Azam FC, Obrey Chirwa amekuwa mchezaji wa tatu msimu huu kufunga mabao matatu katika mchezo mmoja, hat-trick, baada ya kufanya hivyo katika ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Alliance mchezo uliopigwa jana Uwanja wa Nyamagana, Mwanza.Chirwa alifunga mabao hayo dakika ya tano, 24 na 68 baada ya kazi nzuri il...
michezo
['Leicester imeanza mazungumzo na kocha Brendan Rodgers kuhusu mkataba mpya ili kuiwekea ukuta nia ya Arsenal kumnasa kocha huyo. (Telegraph)', 'Kocha wa zamani wa Tottenham Mauricio Pochettino hatakuwa kocha wa Bayern Munich.(Bild)', 'Kocha wa zamani wa Juventus Massimiliano Allegri amesema hatarejea kuwa meneja mpaka...
michezo
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imesitisha uteuzi wa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TIB Corporate, Frank Nyabundege na kumteua Fred Luvanda kushika nafasi hiyo kama Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na benki hiyo, kutenguliwa kwa Nyabundege kumezingatia Kifungu Namba 33(2...
kitaifa
BIASHARA ndani ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Afrika kwa ujumla, inatajwa kukua kwa kiwango cha chini ikiliganishwa na kanda nyingine ulimwenguni.Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwanda na Biashara katika Sekretarieti ya SADC, Calicious Tutalife amesema ikilinganishwa na kanda nyingine duniani, biashar...
uchumi
WAKATI mazoezi ya timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) yakiendelea kunoga, wapinzani wao Guinea ya Ikweta wanatarajiwa kutua nchini leo alfajiri tayari kwa pambano la kufuzu kwa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, Afcom 2021 nchini Cameroon.Kambi ya Taifa Stars ilikamilika juzi baada ya kutua kwa wachezaji wanao...
michezo
MKURUGENZI wa Mashtaka (DPP), Biswalo Mganga amemkabidhi Katibu Mkuu wa Hazina, Doto James madini ya dhahabu, madini ya vito na fedha za kigeni kwa pamoja zenye thamani zaidi ya Sh bilioni tisa zilizotaifi shwa kutokana na kesi za uhujumu uchumi. Mbali na kiwango hicho cha fedha, kiasi kingine cha madini ya Tanzanite ...
kitaifa
SAKATA la malumbano makali yaliyodumu kwa zaidi ya wiki mbili baada ya Spika wa Bunge, Job Ndugai, kudai Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad, amelidhalilisha Bunge kwa kuliita dhaifu, limechukua sura mpya baada ya CAG kukubali kuitikia mwito huo wa Spika.Katika hatua nyingine, Spi...
kitaifa
MCHEZO wa fainali Kombe la Shirikisho la Azam (FA) ulizozikutanisha timu ya Mtibwa Sugar na Singida United, uliingiza mapato ya uwanjani ya Sh milioni 20 mchezo uliopigwa mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini hapa.Mashabiki wa soka walifurika kushuhudia mtanange huo kutoka maeneo mbalimbali ya nda...
michezo
MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Loata ole Sanare, amewaonya wafanyabiashara wasio waaminifu katika mkoa huo kuacha kuingiza bidhaa kwa njia ya magendo ikiwamo vipodozi vilivyozuiwa kwa matumizi ya binadamu na kuonya watakaobainika watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria za nchi.Mkuu huyo wa mkoa alitoa onyo hilo wakati wa uto...
michezo
Mahadhi aliyesajiliwa Yanga akitokea Coastal Union ya Tanga ameandika ujumbe mrefu kwenye mtandao wake wa Instagram. “Assalam alykum ndugu zangu katika imani haja yangu kwenu ni kuomba radhi kwa mashabiki wangu wote na wapenzi wote wa mpira wa miguu duniani, nakiri kufanya makosa hapo nyuma na nimejifunza mengi kupiti...
michezo
Kocha wa muda wa timu ya taifa ya Marekani, Dave Sarachan alitangaza orodha ya wachezaji kwa ajili ya mechi ya kimataifa ya kirafiki Machi 27 itakayofanyika Cary, kaskazini mwa Carolina, ambayo itashirikisha wachezaji 17 kati ya 22 wenye umri wa miaka 24 au chini ya hapo.Weah, 18, anajiunga kwa mara ya kwanza katika k...
michezo
WAZIRI wa Nishati, Dk Medard Kalemani amekutana na Balozi wa Angola nchini Tanzania, Sandro De Oliveira na kufanya mazungumzo kuhusu ushirikiano katika utafi ti wa mafuta na gesi na ununuzi wa mafuta.Mazungumzo kuhusu ushirikiano huo, yalifanyika juzi mjini hapa na kuhudhuriwa na Kaimu Kamishna wa petroli na gesi, Mar...
uchumi
WAZIRI wa Kilimo, Japhet Hasunga amewataka Watanzania kuwekeza kwenye lishe kwani kuna uzalishaji mkubwa wa chakula na hakuna sababu za kuwepo kwa udumavu na hata utapiamlo.Hasunga alisema hayo mjini hapa jana wakati akifungua warsha ya wadau wa kilimo hifadhi.Alisema Tanzania ni wazalishaji wa mazao ambayo yamekuwa y...
kitaifa
KOCHA wa Simba, Mbelgiji Sven Ludwig Vandenbroeck amelalamikia bao la Yanga akidai kuwa lilifungwa wakati mchezaji wake akipatiwa matibabu nje ya uwanja.Alisema kuwa wakati mchezaji huyo akiomba kuingia uwanjani, mwamuzi hakumuona na goli likafungwa. Hatahivyo hakutoa lawama kwa mwamuzi Jonesia kwani alisema dakika zo...
michezo
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga amesema ujenzi wa viwanda umewezesha uchumi wa wilaya hiyo kukua kwa kasi kubwa na kukuza mapato ya halmashauri maradufu.Amesema ofisini kwake mjini Mkuranga kuwa, kwa kuzingatia hali ilivyokuwa kabla ya kuingia Serikali ya Awamu ya Tano na sasa, kuna mabadiliko makubwa, na k...
uchumi
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Dar as Salaam, Daniel Chongolo amezindua kampeni kuhamasisha wananchi wa wilaya hiyo kulipa kodi ya majengo na kodi ya mabango.Chongolo amesema kampeni hiyo itaenda sambamba na kampeni ya nyumba kwa nyumba ikilenga kuhakikisha wamiliki wote wanalipa kodi kwa wakati kukusanya Sh bilioni sab...
uchumi
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri amesema, baada ya Jukwaa la Fursa za Biashara Novemba 21 hadi 23 Tabora haitakuwa kama ilivyo sasa na ameziagiza halmashauri zote ziwe na miradi miwili mikubwa ya viwanda na kilimo.Mwanri amesema, mkoa umeziagiza halmashauri nane za mkoa huo ziwasilishe mipango yao na kwamba, waku...
uchumi
WANANCHI katika vijiji vya Kitongosima na Shinembo katika Wilaya ya Magu mkoani Mwanza, wamepongeza na kushukuru Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita) kwa kuwapa mafunzo wanayosema yamewazindua kimaisha.Walitoa pongezi hizo kwa nyakati tofauti katika vijiji vyao, ambavyo ni vya ...
kitaifa
WATU wanne wamefariki na wengine 42 wamejeruhiwa baada ya basi la abiria la Kampuni ya Fikosh, walilokuwa wakisafiria, kupata ajali baada ya kuacha njia na kupinduka.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Martin Otieno alisema ajali hiyo ni ya juzi katika eneo la Mnarani wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma. Alisema kuwa chanzo ...
kitaifa
RAIS wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Anthony Mtaka ameahidi kutoa Sh 500,000/- kwa kila mwanariadha atakayefikia viwango vya kushiriki Michezo ya Olimpiki itakayofanyika Tokyo, Japan 2020.Mtaka aliyasema hayo Dar es Salaam wakati akiwaaga wanariadha wanane wa Tanzania watakaoshiriki mbio za kimataifa za Nagai M...
michezo
ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA), Dickson Maimu na wenzake watano, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashitaka 100, ikiwemo ya utakatishaji fedha.Mbali na Maimu, washitakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 7/2019 ni Meneja Biashara w...
kitaifa
MFUKO wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) umetenga Sh bilioni 127.3 kwa ajili ya kufadhili miradi ya kilimo nchini Tanzania kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwakani. Rais wa IFAD, Gilbert Fossoun Houngbo aliyasema hayo Ikulu, Dar es Salaam jana alipofanya mazungumzo na Rais John Magufuli.Pamoja na kutenga f...
kitaifa
TIMU ya taifa ya Tanzania kwa wachezaji wenye umri wa chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes), imepangwa Kundi B katika mashindano ya Afrika Mashariki ya Cecafa 2019 yatakayofanyia Uganda, imeelezwa.Ngorongoro Heroes katika Kundi B imepangwa na Kenya na Zanzibar katika mashindano hayo yatakayofanyika Uganda kuanzia Sept...
michezo
SERIKALI ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo la Kimataifa (JICA) inakusudia kuipatia Tanzania mkopo nafuu na ruzuku wenye thamani ya zaidi ya dola milioni 345 za Marekani, sawa na takriban Sh bilioni 794, kwa ajili ya kutekeleza miradi mitatu ya maendeleo.Miradi hiyo ni ukarabati wa barabara ya Arusha hadi Holi...
kitaifa
UTAFITI umeonesha kuwa maambukizi mapya ya Ukimwi yameongezeka kwa kiwango kikubwa kwenye kundi la vijana wenye umri wa miaka 10 hadi 24 ambapo asilimia 40 kati ya asilimia 80 yako kwa wasichana wa umri wa miaka 15 hadi 19.Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa alisema h...
kitaifa
WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema madaktari wote waliosoma kwa fedha za serikali watapangiwa vituo vya kazi.Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dk Faustine Ndugulile alipokuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Nanyamba, Abdalah Chikota (CCM). Katika swali lake la...
kitaifa
SERIKALI itaibadilisha menejimenti ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kupata watendaji wanaotekeleza majukumu yake inavyostahili kwa kuwa kwa sasa wanakosa kuwa na mipango thabiti.Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe alisema hayo jana jijini Dar es Salaam baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa ny...
kitaifa
SIMBA leo inashuka dimbani kucheza nusu fainali dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Mashindano ya Kombe la Mapinduzi utakaochezwa Uwanja wa Amaan Unguja, Zanzibar kuanzia saa 2:15 usiku.Azam FC ambayo ni bingwa mtetezi inacheza na Simba ikiwa na kumbukumbu ya kuifunga katika fainali zilizopita kwa mabao 2-1 katika Uwanj...
michezo
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyopewa mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji imemuhukumu kifungo cha miaka miwili jela, Novat Kaberwa, baada ya kukiri kumuua bila kukusudia mke wake, Clara Munisi.Katika kesi hiyo, Kaberwa alikuwa akikabiliwa na shtaka la kumpiga mke wake baada ya kurudi nyumbani saa 3:00 usiku na ku...
kitaifa
TIMU ya Azam FC imelazimishwa suluhu ya bila kufungana na Mbao FC, kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza na kuendelea kujiweka katika mazingira magumu kwenye mbio za kuwania ubingwa.Matokeo hayo yamewafanya Azam kufikisha pointi 63 baada ya kucheza michezo 30 katika muen...
michezo
Pia alikutana na wawakilishi wa kampuni ya Price Waterhouse Coopers (PwC) wakiongozwa na David Tarimo kutoka Tanzania, John Gibbs (Kanda ya Afrika) na Anne Eriksson (Kanda ya Afrika Mashariki) na kuzungumza nao masuala ya nishati na gesi asilia, miundombinu na upatikanaji wa rasilimali fedha.Katika hatua nyingine Wazi...
uchumi
MBUNGE wa Arusha Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Godbless Lema amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kutotumia vyombo vya ulinzi na usalama ‘kumfinyafinya’ sana.Lema alitoa rai hiyo juzi wakati alipopewa nafasi na Gambo kusalimia wananchi wa Jiji la Arusha katika ufunguzi wa m...
kitaifa
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura na kumtaka kulipa fi dia ya Sh 100,998,121 kwa awamu tano.Hatua hiyo, imekuja baada ya upande wa mashitaka kumfutia Wambura mashitaka ya uhujumu uchumi na kumsomea mashitaka ya kujipatia fedha...
michezo
SEKTA za fedha zikiwamo benki na huduma nyingine za kifedha, wadau wa usafirishaji na wamiliki wa hoteli wametakiwa kuchangamkia fursa zitokanazo na mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika Agosti, mwaka huu. Mkutano huo utaanza Agost 5 hadi 18, mwaka huu na utaambatana na matu...
kitaifa
WAKAZI wa Dar es Salaam wapatao milioni 4.3 wanatarajiwa kumeza kingatiba dhidi ya magonjwa ya matende na mabusha pamoja na minyoo ya tumbo kuanzia Jumamosi ya wiki hii hadi Desemba 20.Aidha, imeelezwa kuwa mbu wa aina zote wakiwemo wale wanaoambukiza ugonjwa wa malaria wana uwezo wa kuambukiza ugonjwa wa matende na m...
kitaifa
['Klabu ya ligi ya Uchina Beijing Guoan wamepania kumsajili winga wa Real Madrid Gareth Bale. Klabu hiyo, ina mpango wa kumfanya winga huyo mwenye miaka 30 kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika ligi ya Uchina. (telegraph)', 'Manchester United, ambao awali walikuwa wakimnyemelea Bale wamejitoa katika mbio za kumsajili m...
michezo
TIMU za Simba na Mbao FC za Tanzania jana zilitakata baada ya kushinda mechi zao na kutinga nusu fainali za mashindano ya Kombe la SportPesa kwenye Uwanja wa Taifa katika muda tofauti.Mbao ndio ilikuwa ya kwanza kutinga nusu fainali na sasa itacheza dhidi ya Kariobang Ijumaa saa 10 jioni katika hatua hiyo baada ya kuw...
michezo
UKOMA ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea aina ya bakteria wa jamii ya “Mycobacterium”. Maambukizo ya wadudu hao hufanyika kwa njia ya hewa kwa mgonjwa kwenda kwa mtu mwingine.Ukoma ni jamii moja na ugonjwa wa Kifua Kikuu ambao pia huenezwa kwa njia ya hewa. Vimelea vya ukoma hushambulia mishipa ya neva na ngozi, wak...
kitaifa
WAZIRI mpya wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa (40) amesema amepokea kwa mikono miwili uteuzi huo na kuwa amejipanga kuitumikia nafasi hiyo kwa umakini na kuleta maendeleo makubwa yanayotakiwa.Bashungwa ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Kilimo kabla ya uteuzi wa jana asubuhi uliofanywa na Rais John Magufuli, alis...
kitaifa
Kwa mujibu wa Kamusi Kuu ya Kiswahili “mtu ni kiumbe mwenye utashi mkubwa kuliko viumbe wengine wote walioko duniani” na “binadamu ni kiumbe mwenye maumbile na sifa tofauti na wanyama wengine na hasa ya kuweza kutambua mema na mabaya”.Kimsingi, ufafanuzi hizi mbili zimetumia maelezo tofauti, lakini hazioneshi tofauti ...
kitaifa
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Magufuli imetoa kipaumbele kwenye matumizi ya tehama kuongeza uwazi, uwajibikaji na ufanisi katika utendaji kazi.Amewataka wananchi kutumia vizuri teknolojia hiyo ya habari na mawasiliano kwenye shughuli za uzalishaji mali na utoa...
kitaifa
Ametoa agizo hilo wakati akizungumza jana mjini hapa katika ufunguzi wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya SHIMUTTA.Amesema wafanyakazi wakishiriki mashindano hayo wataweza kuwasaidia katika matumizi yao kwa kupunguza gharama za matibabu pamoja na magonjwa yasiyoambukiza kwani watakuwa wamefanya mazoezi.Makamu wa Rais amba...
michezo
JUMLA ya Sh milioni 44.9 zimepatikana katika kipindi cha siku nne kuanzia Mei 6 hadi 9, mwaka huu, kutokana na ushuru na kodi mbalimbali zitokanazo na madini tangu serikali ilipoanzisha uratibu wa kufungua vituo vya kuuza na kununua madini mkoani Ruvuma.Takwimu hizo zilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mnde...
kitaifa
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Ilala inawashikilia watu watatu akiwamo mmiliki wa Kampuni ya Motrax, Chandulal Ladwa kwa tuhuma za kutoa rushwa ya Sh200,000.Mtuhumiwa huyo alitoa rushwa kwa wakili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Goodluck Mwangomango ili ampe upendeleo kwenye kikao cha kujad...
kitaifa
KUFUATIA kuwepo kwa taarifa zilizoenea za kusimamishwa kwa baadhi ya benki katika biashara ya kubadilisha fedha, Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imebainisha kuwa ilichokifanya ni kuzisimamisha ushiriki katika soko la jumla la fedha za kigeni na si kubadili fedha reja reja.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na benki hi...
kitaifa
WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo amechukizwa na kukemea utendaji kazi wa watendaji wa wilaya ya Kongwa wa kufanya kazi kwa maigizo.Pia, ameagiza Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Nelson Milanzi kujieleza kwa maandishi kwa kushindwa kuwa...
kitaifa
WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, imeanza operesheni maalum kubaini wamiliki hewa wa viwanja zaidi ya 9,000, vilivyoandikishwa kumilikiwa na watumishi wa wizara hiyo kwa njia isiyokuwa halali.Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ...
kitaifa
KATIBU Mkuu Kiongozi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Balozi John Kijazi amezindua vikundi kazi vya baraza hilo kwa lengo la kujenga na kuimarisha mahusiano kati ya sekta za umma na binafsi katika kuibua changamoto na kuzijadili kwa mustakabali wa maendeleo ya Tanzania....
kitaifa
SIMBA itacheza nusu fainali dhidi ya Azam FC katika mchezo wa mashindano ya Mapinduzi yanayochezwa visiwani Zanzibar kesho kutwa.Mchezo huo utachezwa katika Uwanja wa Amaan, Unguja baada ya jana kuifunga Zimamoto kwa mabao 3-1 katika Uwanja wa Gombani, Pemba. Azam FC ambaye ni bingwa mtetezi wa mashindano hayo, anakut...
michezo
SERIKALI imejizatiti kuongeza uwekezaji katika kilimo cha miwa ukienda sanjari na ujenzi wa viwanda vya sukari, kupunguza nakisi iliyopo.Akizungumza na Habarileo hivi karibuni, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amesema upo mkakati wa makusudi kuhakikisha viwanda vilivyopo vinaongeza uzalishaji wa sukari na kuongeza uwe...
uchumi
WAGONJWA 400 wa mabusha na matende wamefanyiwa upasuaji wa ugonjwa huo katika Wilaya za Kinondoni, Ilala na Temeke tangu kuanzishwa kwa kampeni hiyo, hatua iliyotokana na elimu mbalimbali inayoendelea kutolewa kwa wananchi.Hayo yalibainishwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam jana, Dk Grace Maghembe wakati wa sem...
kitaifa
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa kesho Jumatatu atakuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mashindano ya kitaifa ya Umoja wa Shule za Sekondari Tanzania (Umisseta) yatakayofanyika mjini Mtwara.Michezo hiyo itakayoshirikisha takribani washiriki 3,304 kutoka mikoa 26 ya Tanzania Bara na miwili Zanzibar, itafanyika hadi Juni 21 n...
michezo
LEO, Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea kwa michezo mitatu katika viwanja tofauti ukiwemo ule utakaowakutanisha mabingwa mara 27 wa ligi hiyo, Yanga SC ambao watawaalika Mbao FC katika Uwanja wa Taifa.Mara ya mwisho timu hizo kukutana ilikuwa Mei 22 mwaka jana katika uwanja huo huo ambapo Yanga walitoka na u...
michezo
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imeingia katika ushirikiano na kampuni ya Samsung Mobile pamoja na kampuni ya usambazaji ya Yellow box kuzindua ingizo jipya la simu za kisasa aina ya Samsung A series.Airtel na Samsung imeingia ubia huo huku ikizindua OFA maalumu kupitia Samsung A10 na A2 core inayolenga ...
kitaifa
MABONDIA Watanzania wametakiwa kujiaandaa vyema kabla ya kwenda kushiriki kwenye mashindano makubwa.Rai hiyo imetolewa baada ya mabondia wa Tanzania, Swedi Mohamed na Suleiman Said kupigwa kwa Knockout (KO) katika mapambano ya utangulizi kabla ya pambano la marudiano kati ya Andy Ruiz na Anthony Joshua lililofanyika n...
michezo
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi wa chuo hicho, Profesa Mathew Luhanga, katika hotuba yake iliyosomwa na Profesa Eliuter Mageni katika mahafali ya 48 ya chuo hicho mwishoni mwa wiki.Alisema kwamba ufugaji wa nyuki ni eneo linalokua kwa kasi hapa nchini hivyo chuo hicho kinajipanga kutoa mchango wa...
uchumi
CHAMA cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimevishauri vyuo vikuu nchini kuona umuhimu wa kufundisha masuala ya mazingira, madini na mafuta katika mitaala yao, ili kuijengea jamii uelewa mpana katika maeneo hayo.Rais wa TLS, Dk Rugemeleza Nshala alisema hayo Dar es Salaam jana na kuongeza kuwa kwa kufanya hivyo, itasaidia...
kitaifa
MBUNIFU wa teknolojia ya umwagiliaji wa shamba kwa kutumia simu janja, Ramadhani Bakari kutoka Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, amebuni mfumo wa umwagiliaji unaomwezesha mkulima kumwagilia kwa kutumia simu ya mkononi akiwa ndani au nje ya nchi.Bakari ambaye ni Mhitimu wa Stashahada ya Teknolojia ya Habari na Ma...
kitaifa
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imewakumbusha wananchi kudai risiti sahihi kila wanapofanya manunuzi ya bidhaa, la sivyo haitasita kuwatoza faini na hata kuwashitaki mahakamani.Meneja wa TRA Mkoa wa Mwanza, Ernest Dundee alisisitiza hilo alipozungumza na HabariLeo jijini hapa juzi kuhusu wajibu wa mnunuzi wa bidhaa k...
uchumi
OFISI ya Waziri Mkuu inayoshughulikia Sera, Bunge, Vijana, Kazi na Ajira mkoani Lindi imetoa mikopo yenye thamani ya Sh milioni 200 kwa vikundi vya uzalishaji mali vya vijana tujiajiri 53 kwa nyakati tofauti.Vijana hao wanatoka vikundi vya uzalishaji vilivyoko katika halmashauri sita za wilaya za Kilwa, Liwale, Nachin...
kitaifa
USHINDI wa Azam FC wa mabao 2-0 dhidi ya Lipuli katika mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa juzi, ni salamu kwa Yanga kuwa wako tayari kupambana kuelekea katika mchezo utakaowakutanisha kesho.Azam FC ilishinda mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kufuatia Uwanja wao wa Azam Complex, kuwa katika matenge...
michezo
Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mohamed Ahmada katika hafla ya uzinduzi wa mtandao wenye kasi wa 4G pamoja na huduma za kibenki kwa njia ya simu kutoka kampuni ya Zantel.Alisema pamoja na jitihada mbalimbali zinazofanywa na sekta za mawasiliano n...
uchumi
MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imesema haikusudii kuiondoa Kampuni ya Fastjet kufanya kazi zake nchini, badala yake inatakiwa kufuata masharti ya sheria za uendeshaji wa shughuli za usafiri wa anga ili kuepusha madhara, ikiwamo ajali.Kuhusu Mwenyekiti Mtendaji wa Fastjet, Lawrence Masha kujichagua kuwa Men...
kitaifa
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga amesema udanganyifu ni tatizo kubwa linalokabili mfuko huo na kwamba hadi sasa wameweza kuokoa Sh bilioni 4 ambazo zingeliwa na wajanja kwa udanganyifu. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga kwenye kikao cha mfuko huo na wahariri, kilichofanyika k...
kitaifa
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kuanzia saa 2:00 usiku.Ni mchezo mgumu na muhimu kwa timu zote kushinda kwani atakayepata matokeo mazuri ndiye atakayesonga mbele hatua ya nusu fainali. Azam Complex inapewa nafasi ya kusonga mbele kutokana na sababu zifuatazo.Mara nyingi inapocheza kwenye uwanja wa nyumbani hupata mato...
michezo
MCHUNGAJI wa Kanisa la Gospel Revival Center (GRC), lililopo Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam, Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ amewataka Watanzania kumpa muda Rais John Magufuli katika kazi yake ya kuliunganisha taifa na kuleta maendeleo na kwamba watahoji utendaji wake mara baada ya kutoka madarakani.Amesema kuwa...
kitaifa
Waziri Mwakyembe ametoa ojnyo hilo mjini Kigoma wakati anafunga mafunzo ya ngazi ya chini (Grass Root) ya ualimu wa mpira wa miguu kwa walimu kutoka shule za msingi na sekondari, ikiwa ni programu ya kuibua vipaji kuanzia ngazi za chini.Alisema amekuwa akipitia video zilizofungwa katika uwanja huo na kuona baadhi ya w...
michezo
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge amekuwa mbogo kwa watendaji wanaochelewesha ugawaji na usambazaji vitambulisho vya wajasiriamali katika maeneo yao mkoani humo. Dk Mahenge alisema hayo baada ya kutembelea halmashauri mbalimbali, kukagua namna vitambulisho hivyo vilivyotolewa kwa wajasiriamali na Rais John M...
kitaifa
SIMBA, leo inatarajiwa kukabidhiwa taji lake la Ubingwa wa Ligi Kuu Bara baada ya mechi dhidi ya Biashara United itakayofanyika kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam.Mechi hiyo ni ya 37 kwa Simba ambayo imeshatangaza ubingwa tangu wiki iliyopita ilipoifunga Singida United mabao 2-0 na kufikisha pointi 91 ambazo haziwez...
michezo
['Tunisia iliishinda Ghana kupitia mikwaju ya penlati na kutinga robo fainali michuano ya Afcon dhidi ya Madagascar.', 'Mlinda lango Farouk Ben Mustapha ndiye aliyekuwa shujaa baada ya kuingia na kuokoa mkwaju wa penalti wa Caleb Ekuban.', 'Tunisia ilikuwa imekaribia kushinda ilipofikia dakika ya 90 kabla ya beki wa z...
michezo
KOCHA wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Emanuel Amunike ametangaza kikosi cha wachezaji 25 kitakachocheza na Uganda katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon 2019) mchezo utakaochezwa Septemba 8 kwenye Uwanja wa Namboole Kampala, Uganda.Akizungumza jana, Amunike alisema timu hiyo it...
michezo
Aidha kampuni hiyo iliyopo chini ya Kampuni ya Toyota Tanzania Limited imeamua kupunguza bei ya pikipiki zake aina ya Yamaha kwa lengo la kuwavutia vijana wengi na kuunga mkono jitihada za serikali za kuongeza ajira kwa vijana kupitia biashara ya bodaboda ambayo imesaidia vijana wengi kujiajiri na kuepuka kujitumbukiz...
uchumi
MSIMU mpya wa Coke Studio Africa umezinduliwa rasmi Tanzania katika hafla iliyofanyika klabu ya burudani ya Lifepark Mwenge mwishoni mwa wiki iliyopita.Mkurungezi Mkuu wa Coca-Cola Kwanza, Basil Gadzios amekiri kufurahishwa na vipaji na uwezo wa wasanii Watanzania watakaoshiriki kwenye msimu huu mpya. Tanzania itawaki...
michezo
JIJI la Dodoma limetenga maeneo matatu kwa ajili ya kuwaweka wafanyabiashara wadogo wanaopanga biashara zao barabarani. Ofisa Masoko wa Jiji la Dodoma, James Yunu akizungumza na gazeti hili alisema maeneo hayo yaliyotengwa ni pamoja na pembeni ya soko la sabasaba ambalo ndio stendi kubwa ya mabasi yanayozunguka maeneo...
kitaifa
MARAIS Dk John Magufuli na Profesa Arthur Peter Mutharika wa Malawi wamekubaliana kwa pamoja kukuza uchumi wa nchi zao.Akiwa nchini humo, Rais Magufuli jana alifungua msimu wa soko la tumbaku na kusema nchi za Afrika zina haja ya kufanya mapinduzi kwenye sekta ya kilimo, kwa kuanzisha viwanda vya usindikaji vitakavyoo...
kitaifa
KAZI ya kutandaza mabomba ya gesi kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kwa Mkoa wa Lindi inatarajia kuanza mwisho wa mwezi huu.Hayo yamebainishwa bungeni na Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kuteuliwa, Salma Kikwete (CCM), aliyetaka kujua ni lini wananchi wa Lindi watafi...
kitaifa
HOMA ya ugonjwa wa dengue imeendelea kutikisa mikoa ya Dar es Salaam na Tanga ambapo mpaka sasa watu zaidi ya 2,900 wamethibitika kuugua ugonjwa huo, katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Mei mwaka huu.Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto jana, wagonjwa wawili walipote...
kitaifa
Wadau wengine ni Wakala wa usafirishaji mizigo bandarini (TAFFA), Wakala wa vipimo (WMA), Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Maliasili na Utalii, Kampuni ya Kuhudumia Kontena Bandarini (TICS) na Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (TA...
uchumi
SERIKALI imesema vyuo vya elimu ya juu nchini, havifanyi vizuri katika eneo la machapisho kwa kutokuwa nayo ya kutosha, jambo ambalo husababisha kushuka katika upangaji wa nafasi za vyuo vikuu kitaifa na kimataifa.Imeeleza katika eneo la taaluma, vyuo hivyo viko vizuri, lakini mara nyingi havishiki nafasi nzuri, huku ...
kitaifa
UCHAGUZI mdogo wa kujaza nafasi za uongozi Yanga umekuwa kizungumkuti baada ya Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kushindwa kutangaza tarehe ya kufanyika kwake.Awali, uchaguzi huo ulikuwa ufanyike Januari 13, mwaka huu, ukasogezwe mbele wagombea wakiwa katika hatua ya kujinadi kutokana na baadhi y...
michezo
SERIKALI kupitia Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imewaagiza maofisa elimu mikoa na wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kushughulikia nyongeza ya mishahara ya walimu waliopandishwa madaraja nchini ili waanze kulipwa stahiki zao kuanzia mwezi Agosti mwaka huu.Agizo hilo lilitolewa jana ...
kitaifa
WIZARA ya Miundombinu imeelekeza watoa huduma ya usafiri wa pikipiki maarufu bodaboda kutumia mfumo wa kisasa wa abiria kutolipa fedha taslimu Julai 1, mwaka huu.Hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya kuhakikisha matumizi ya fedha taslimu katika huduma zote yanakoma ifikapo mwaka 2024.Uamuzi wa kuanza na pikip...
uchumi
KUTOKANA na kuwepo kwa matendo ya unyanyasaji na ukatili kwa watoto Shirika lisilo la Kiserikali la Compassion International Tanzania limeiomba serikali ione uwezekano wa kuweka somo la ulinzi wa mtoto kwenye mitaala ya elimu.Hayo yalielezwa na Mkurugenzi wa Shirika hilo Tanzania, Agness Hotay wakati akitoa salamu kwa...
kitaifa
MKUU wa Mkoa wa Mara, Adam Malima ametoa siku tatu kwa viongozi wa Wilaya ya Tarime kubaini zilipo fedha za huduma zilizotolewa na Mgodi wa Acacia North Mara kwa miaka mitatu kiasi cha Sh bilioni 9.5.Malima alitoa agizo hilo kwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Charles Kabeho, maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (...
kitaifa
WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amesema ana hakika timu hiyo itarejea na ushindi kutoka Cape Verde.Stars ilisafiri alfajiri ya jana kwenda Praia kucheza na wenyeji wao Cape Verde kesho mechi ya kuwania kufuzu fainali za michuano ya Kombe la Mataifa Afrika iliyopangwa kufanyika Came...
michezo
KOCHA wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema amewajenga wachezaji wake kisaikolojia kukabiliana na mbinu za fi tina zinazotumiwa na timu nyingi za Kiarabu wakiwa kwao kujinufaisha kupata matokeo chanya.Aidha, Zahera alisema wataingia kwenye mchezo huo wakiwa na malengo mawili makubwa, kwanza kujilinda kuzuia wasifungwe na ku...
michezo
UTALII unachangia asilimia 25 ya pato la ndani Zanzibar na asilimia 80 ya fedha za kigeni, jambo ambalo wataalamu wanasema lisingewezekana bila kuwepo kwa matumizi bora ya teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama).Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, Dk Mzee Suleiman Mnde...
uchumi
MGOMBEA nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji katika klabu ya Yanga, Athanas Kazige amesema anataka kutumia fani yake kuiwezesha kiuchumi klabu hiyo. Uchaguzi wa Yanga umepangwa kufanyika Mei 5 na sasa wagombea wanajipigia kampeni ili kuwania nafasi wanazogombea.Akizungumza jana na gazeti hili Dar es Salaam, alisema ...
michezo
SERIKALI imesema hadi Desemba 31, mwaka huu, Watanzania wote wenye sifa za kupata vitambulisho vya Taifa watakamilisha usajili wa kuchukua alama za vidole, picha na saini ya kielektroniki, kazi inayoendelea kufanywa sasa.Sambamba na hilo, serikali imesema itanunua mashine mpya za uzalishaji wa vitambulisho vya taifa z...
kitaifa
YANGA imeendeleza wimbi la ushindi dhidi ya Tanzania Prisons ya Mbeya baad aya kuifunga 2-0 katika mchezo wa Kombe la FA, hatua ya 32 bora katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam jana. Hii ni mara ya pili kwa Yanga kuifunga Tanzania Prisons msimu huu, ambapo kwa mara ya kwanza waliifunga 1-0 na...
michezo
Akizungumzia mfumo huo alisema mfumo huo utatumika kutoa mizigo bandarini, katika viwanja vya ndege na mipakani na wenye kuhusisha wadau mbalimbali.“Awali Idara ya Forodha ilikuwa ikitumia mfumo wa asycuda kwa ajili ya kutolea mzigo ambapo umekuwa na changamoto nyingi zilizokuwa zikisababisha ucheleweshwaji wa kutoa m...
uchumi
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Bashiru Ally amekitangaza kijiji cha Nzali kuwa kituo cha uhamasishaji Mkoa wa Dodoma.Alisema hayo katika kijiji cha Nzali kata ya Chilonwa Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 42 tangu kuzaliwa kwa CCM na kubainisha kuwa maadhimisho h...
kitaifa
WAKATI nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kila moja ikionesha kuridhika na kuwa tayari kuiunga mkono Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika kampeni za kujiunga na jumuiya hiyo, wadau wengine wa maendeleo nao hawako nyuma.Wasomi, wachumi na wanadiplomasia ni miongoni mwa wanaoiunga mkono DRC kut...
kitaifa
MAMLAKA ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji (EPZA) imesema inaendelea kuvutia uwekezaji kwenye viwanda vinavyotumia teknolojia ya kisasa, ili kukuza na kuendeleza wajasiriamali waitumie kukuza uchumi.Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Uhamasishaji Uwekezaji wa EPZA, James Maziku alipozungumzia uwekezaji wa kiwanda cha kutenge...
uchumi
WIZARA ya Mifugo na Uvuvi imewaonya wafanyabiashara na wafugaji watakaojaribu kutorosha mazao ya mifugo zikiwemo ngozi kwa njia ya panya na kuikosesha serikali mapato, kuwa watachukuliwa hatua kali kisheria.Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa Elisante Ole Gabriel alitoa onyo hilo hivi karibuni wakati alipotembelea Kiw...
kitaifa
MABINGWA wa kihistoria wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara Yanga leo wana kazi ya kuhakikisha wanasaka ushindi dhidi ya Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa ligi utakaochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Huo utakuwa mchezo wa tatu wa ligi tangu kuanza kwa msimu huu wa mwaka 2019/20 Yanga ikicheza kwenye uwanja ...
michezo