content stringlengths 1k 24.2k | category stringclasses 6
values |
|---|---|
MKAZI wa Boko, Abubakar Hamisi (46) ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa mkataba wa mauziano ya kiwanja kati yake na aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Takukuru, Godfrey Gugai, uliandikwa Sh milioni 60 lakini walipewa Sh milioni 80 ili kupata ahuweni ya kodi.Hamisi ni shahidi wa 20 katika kesi ya utakatishaji fedha n... | kitaifa |
Kauli hiyo ameitoa wakati wa ufunguzi wa duka kubwa la kampuni hiyo mjini Dodoma baada ya kufanyiwa ukarabati mkubwa ili liweze kuwa la kisasa linalokidhi mahitaji ya mji mkuu.Mkuu huyo wa mkoa wa Dodoma pamoja na kuwapongeza kwa kuboresha utoaji wa huduma za mawasiliano kwa watumiaji nchini, amewataka wakazi wa Dodom... | uchumi |
WAENDESHA bodaboda nchini wametakiwa kutochukua sheria mkononi inapotokea watu wamesababisha ajali wakiendesha barabarani.Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuf Masauni alisema hayo mjini hapa jana wakati akijibu swali la Nyongeza la Mbunge wa Kuteuliwa, Salma Kikwete (CCM). Salma alitaka kujua serikali i... | kitaifa |
Alisema asilimia 81 ya mabomba yameshawasili eneo la mradi kutoka China. Idadi ya mabomba inayohitajika ni 440 hali ambayo alisema inamfariji kuwa mradi huo utakamilika kwa wakati. Aliongeza kuwa mabomba zaidi ya nusu (kilometa 265 ) yameshaunganishwa kati ya kilometa 542 ambazo ndio umbali wa Mtwara hadi Dar es Salaa... | uchumi |
WAKATI serikali ikiendelea na ujenzi wa reli ya kisasa kati ya Dar es Salaam na Mwanza yenye urefu wa kilometa 1,219 na pia kukarabati ile ya zamani maarufu kama `Reli ya Kati’, Shirika la Reli Tanzania (TRL), limetangaza kugeukia ujenzi wa reli za mijini, ikianza na Dar es Salaam na Dodoma.Lengo la reli hizo, limetaj... | kitaifa |
Mshambuliaji Elius Maguli anayekipiga klabu ya Dhofar inayoshiriki Ligi Kuu Oman ndiye aliyefunga bao hilo dakika ya 18 kwa shuti. Taifa Stars sasa itamenyana na Zambia katika mechi ya nusu fainali baada ya Zambia kuitoa Botswana juzi katika robo fainali nyingine.Baada ya kufungwa bao hilo, Afrika Kusini walibadilika ... | michezo |
Lulu aliye nje kwa dhamana atapanda kizimbani mahakamani hapo baada ya kusomewa maelezo ya awali karibu miaka miwili na nusu iliyopita. Msanii huyo anakabiliwa na kesi hiyo akidaiwa kumuua Kanumba bila kukusudia kinyume cha Kifungu cha 195 cha Kanuni za Adhabu.Inadaiwa Lulu alimuua Kanumba bila ya kukusudia Aprili 7, ... | michezo |
NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angeline Mabula ametengua uteuzi wa nafasi ya Ofi sa Ardhi Mteule wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Paul Misuzi na wakuu wa idara za ardhi wa Halmashauri ya Wilaya Kigoma na Halmashauri ya Manispaa Kigoma Ujiji.Hatua hiyo imekuja baada ya watendaji hao, kushindwa kuteke... | kitaifa |
IKIWA zimebaki siku tatu, kuanza kwa katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki, Jiji la Dar es Salaam limeweka mikakati mbalimbali kwa ajili ya kutekeleza agizo hilo katika mitaa mbalimbali.Aidha, uongozi wa mkoa, umeahidi kuwa kazi ya kutokomeza mifuko hiyo, haitakuwa ya nguvu wala usumbufu wowote na tayari vikosi kaz... | kitaifa |
WAKATI michuano ya soka ya Ligi ya Mabingwa Afrika Mashariki na Kati, (Kombe la Kagame) ikianza leo kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Baraza la vyama vya soka ukanda huo, Cecafa, Nicholaus Musonye amesema viongozi wa vyama wanachama wanahujumu.Akizungumza na waandishi wa habari jana M... | michezo |
SERIKALI imezitaka halmashauri zote zinazojenga hospitali za wilaya mkoani Lindi, zimalize kwa wakati uliopangwa bila kutoa sababu na kusababisha ujenzi wa hospitali hizo kuchelewa zaidi.Hayo yalibainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo mwishoni mwa wik... | kitaifa |
['Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars hii leo imeandikisha sare 1-1 na timu ya taifa ya Burundi Intamba Murugamba katika mechi za kufuzu kwa kombe la dunia nchini Qatar 2022.', 'Licha ya kutawala kipindi cha kwanza cha mchezo Tanzania ilishindwa kuona lango la wenyeji wao huku washambuliaji hodari Mbwana Samatta anay... | michezo |
AZAM FC jana ilikata tiketi ya nusu fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho la Azam baada ya kuifunga Kagera Sugar kwa bao 1-0 katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Kaitaba,Kagera.Katika mchezo huo bao pekee lililoifanya Azam kusonga mbele liliwekwa kimiani na Joseph Mahundi dakika ya 79 baada ya kuwatambuka mab... | michezo |
SAKATA la askari polisi wanane wanaodaiwa kujihusisha na kashfa ya utoroshaji dhahabu jijini Mwanza, limetua rasmi kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Robert Boaz.Askari hao ambao Januari 4, mwaka huu, waliwakamata watu waliotaka kutorosha kilo 323.6 za dhahabu yenye thamani ya zaidi ya Sh bil... | kitaifa |
AGIZO la Rais John Magufuli la kumtaka Msajili wa Hazina kuyabana mashirika ya umma ili kulipa gawio kwa serikali, hatimaye ofisi hiyo imevuka lengo kwa kukusanya Sh bilioni 633.39 hadi kufikia Juni mwaka huu, sawa na asilimia 106.Fedha hizo zinatokana na makusanyo ya mapato yasiyo ya kodi kutoka katika taasisi, mashi... | uchumi |
SERIKALI imetoa tahadhari kwa shule 108 za msingi, sekondari na za ufundi kwa kushindwa kukidhi matakwa ya wizara hiyo.Ripoti mpya ya Wizara ya Elimu inasema shule hizo zimebainika kutokidhi viwango vya usafi, matumizi mabaya ya ruzuku, kushindwa kutoa elimu na matumizi mabaya ya vifaa vya teknolojia ya mawasiliano.Ha... | kimataifa |
TANZANIA na Uganda zimeanzisha rasmi Jukwaa la Biashara baina ya nchi hizo, lengo likiwa kufungua milango zaidi ya biashara na uwekezaji kati ya nchi hizo mbili wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).Mbali ya Tanzania na Uganda, nchi nyingine wanachama wa EAC, jumuiya yenye wakazi zaidi ya milioni 170 ni Kenya... | kitaifa |
WAHADHIRI wa vyuo vya elimu ya juu wameunga mkono kauli ya Rais John Magufuli kwamba baadhi ya shahada zinazotolewa na vyuo vikuu sasa hazina hadhi bali wanafunzi wanamaliza vyuo ili kupata vyeti.Aidha wameshauri kufanyika kwa maboresho ya elimu na kuwe na msukumo wa kuwajali walimu kimaslahi lakini pia kuwaendeleza k... | kitaifa |
BAADA ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbao FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa, Yanga wametamba kuifunga Pyramids katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.Yanga watashuka dimba CCM Kirumba Jumapili kuikaribisha Pyramids ya Misri katika mchezo wa ply-off... | michezo |
KUPITIA Mfumo wa Mawasiliano ya Simu (TTMS) Serikali imepata zaidi ya Sh bilioni 93.6 fedha ambazo kama sio mfumo huo zingekuwa kwenye mifuko ya watu.Takwimu hizo zilitolewa Dar ea Salaam jana na Rais John Magufuli wakati akikabidhiwa rasmi mfumo huo ambao unasimamiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ili kuth... | kitaifa |
JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha linaendelea kumshikilia Mwenyekiti wa Kijiji cha Bangata, wilayani Arumeru, Michael Silamoi kwa tuhuma za kumshambulia hadi kumsababishia kifo mmoja wa wanakijiji wa kijiji hicho.Mbali na Mwenyekiti huyo, wengine wanaoshikiliwa ni askari mgambo wawili wa kijiji hicho waliofahamika kwa ma... | kitaifa |
KOCHA Msaidizi wa Taifa Stars Juma Mgunda amesema wanakwenda Sudan kupindua matokeo na kukata tiketi ya kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani zitakazofanyika Cameroon mwakani. Taifa Stars ikiwa kwenye nyumbani ilikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Sudan na kujiweka kwenye wakati mgumu wa kuf... | michezo |
RAIS mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk Jakaya Kikwete ambaye ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, amewataka wahitimu wa shahada za ualimu, kujiandaa kisaikolojia kufundisha shule za msingi, badala ya sekondari kama walivyotarajia.Alisema hayo juzi kwenye mahafali ya 10 ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Chuo Kikuu cha Dar es S... | kitaifa |
MABINGWA watetezi wa michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame), Azam FC watawakosa nyota watano katika michuano hiyo kutokana na sababu mbalimbali.Michuano hiyo inatarajiwa kuanza Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii na Azam imepangwa kundi A pamoja na timu za JKU ya Zanzibar, Kator FC ya Suda... | michezo |
TIMU ya soka ya vijana ya Tanzania imeiadhibu Zimbabwe kwa mabao 6-2 katika mchezo wa fainali za mashindano ya kwanza ya COPA Coca-Cola kwa vijana chini ya umri wa miaka 16 ya Mataifa ya Afrika na kutwaa ubingwa.Tanzania ilionesha kiwango cha juu na kuibuka mshindi katika mechi ya fainali iliyofanyika kwenye viwanja v... | michezo |
Miji hiyo ni Dar es Salaam, Mwanza, Kilimanjaro, Zanzibar na Mbeya na pia safari ya kimataifa kati ya Dar es Salaam na Johannesburg, Afrika Kusini.“Kwa mwaka mmoja sasa Fastjet imeona Watanzania wakisafiri kwa ajili ya mikutano ya kibiashara na kutembelea ndugu na jamaa hivyo kuepusha uchovu na muda mwingi wa kusafiri... | uchumi |
KAMPUNI ya teknolojia ya malipo ya kimataifa, Visa imetangaza ushirikiano wa mkakati na Halotel ili kuwezesha malipo ya Visa kwenye simu kwa kutuma codi ya QR kwa wateja wa Halotel nchini Tanzania. Huduma hiyo itakayotolewa mwanzoni mwa mwaka 2019 na hivyo kuwezesha wateja zaidi ya milioni moja wa HaloPesa kutumia Vis... | uchumi |
MWENYEKITI wa kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Ally Mchungahela ametangaza rasmi uchaguzi mkuu wa Klabu ya Yanga kwamba utafanyika Mei 5 mwaka huu.Uchaguzi huo umetangazwa kufanyika siku hiyo kutokana na agizo la Serikali kupitia Baraza la Michezo nchini (BMT), kuitaka TFF isimamie klab... | michezo |
['Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer yupo tayari kusubiri hadi msimu ujao w ajoto kushinikiza kiungo cha ushambilizi , huku mchezaji wa kiungo cha mbele wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, mwenye umri wa miaka 19, akisalia kuwa mchezaji anayemlenga pakuu. (Evening Standard)', 'Barcelona na Paris St-Germai... | michezo |
SIMBA sasa bado pointi tano tu kumfikia mpinzani wake mkubwa Yanga anayeongoza Ligi Kuu Soka ya Tanzania Bara baada ya jana kuifunga Biashara ya Mara kwa mabao 2-0.Ushindi kwenye mchezo huo uliochezwa mkoani Mara unaifanya Simba kufikisha pointi 69, pointi tano nyuma ya Yanga yenye pointi 74.Huo ni muendelezo wa mabin... | michezo |
Huduma hiyo ambayo inatolewa kwa kushirikiana na Kampuni ya AFB, imelenga kubadilisha maisha ya wafanyabiashara wadogo ambao wanahitaji mikopo kuimarisha mitaji yao.Huduma hiyo itakayojulikana kama “Airtel Money Timiza” ni sehemu ya juhudi za Airtel ya kuungana na Serikali katika kuwezesha wananchi na wateja wa Airtel... | uchumi |
WATU 26 wakiwemo Watanzania watatu wamekufa katika shambulio la bomu lililofanyika katika hoteli mjini Kismayo, Somalia.Mwandishi wa habari maarufu mwenye uraia wa Canada na Somalia, Hodan Nalayeh na mumewe, Farid, ni miongoni mwa waliokufa katika shambulio hilo linalosadikiwa kufanywa na kundi la wapiganaji wa al sha... | kitaifa |
SERIKALI haina mpango wa kuvibadili vyuo vya Maendeleo ya Wananchi kuwa VETA. Hayo yamebainishwa jana mjini hapa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Willam Ole Nasha wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Rufiji, Mohamed Mchengerwa (CCM). Mchengerwa alisema katika swali: “Serikali imerejesha vyuo vil... | kitaifa |
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge ameshauri wakuu wa mikoa nchini kuhamasisha matumizi ya mfumo wa anwani za makazi na postikodi.Pia ameiomba Ofisi ya Rais Tamisemi na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) kuwezesha suala la anuani ya makazi kufanikiwa. Hayo yamo katika hotuba yake... | kitaifa |
Maswi alitoa agizo hilo mjini Mbeya jana, wakati akizungumza na wafanyakazi wa Idara ya Madini mkoani Mbeya, ambako alipatiwa taarifa na Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), kuhusu kampuni kubwa tatu zinazogoma kulipa maduhuli stahiki kwa Serikali, kwa madai ya kuwa na hati ya msamaha wa kodi katika baadhi ya ... | uchumi |
WATU watano wa familia moja wamekufa papo hapo baada ya kupigwa na radi ambayo pia iliwajeruhi watu watatu wa Kijiji cha Isongwa, Kata ya Mkole, Wilaya ya Sikonge, Tabora.Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Kamishina Msaidizi wa Polisi Emanuel Nley ilisema mvua kubwa iliyonyesha juzi usiku ikia... | kitaifa |
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema, Mbunge wa Kigoma Mjini, Kabwe Zitto anampa taabu sana na ameomba ushauri amfanye nini.Ndugai amesema jijini Dar es Salaam kuwa, Zitto anampa taabu kwa sababu chama cha ACT Wazalendo kina Mbunge mmoja tu kwenye Bunge la Tanzania hivyo akimfukuza chama hicho kitakosa uwaki... | kitaifa |
MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan, amewataka wawekezaji, wafanyabiashara, taasisi za fedha na wajasiriamali kuwa na uthubutu na kuchangamkia fursa, zinazoibuliwa Lindi ili kuujenga mkoa huo, ambao ni kati ya mikoa yenye utajiri uliojifi cha.Pia, amewataka Watanzania na wawekezaji, kuchangamkia fursa zinazoibuliwa ka... | uchumi |
MAZIKO ya aliyekuwa mmiliki wa timu ya Pallson ya Mbuguni wilayani Arumeru mkoani Arusha, Thomas Mollel maarufu Askofu yanatarajiwa kufanyika Jumatatu, nyumbani kwake Mbuguni.`Askofu’ ambaye ni mfanyabiashara maarufu wa madini ya tanzanite na mmiliki wa migodi hiyo iliyoko wilayani Simanjiro mkoani Manyara, alifariki ... | michezo |
UJENZI wa reli ya kisasa unaoendelea katika maeneo mbalimbali kati ya Dar es Salaam- Morogoro na Dodoma, umetajwa kuviachia neema kubwa viwanda vya ndani kutokana na malighafi yenye thamani ya mabilioni kununuliwa nchini.Kwa sasa viwanda vya saruji na nondo, ndivyo vinavyoonekana kunufaika zaidi kutokana na mahitaji m... | kitaifa |
Besson anayeiwakilisha Kampuni ya GDF Suez ya Ufaransa, alitembelea wizara kufahamu fursa za uwekezaji zilizo katika sekta ya nishati na madini.“Kampuni unayoiwakilisha ni kubwa, yenye teknolojia ya kisasa na inafanya uwekezaji mkubwa duniani hivyo kama mna nia ya kuwekeza katika uendelezaji wa vitalu vya gesi mnaweza... | uchumi |
RAIS John Magufuli amedokeza kisa kilichosababisha kusimamishwa kazi kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), James Mataragio ambaye ameamuru arudishwe katika nafasi yake.Akizungumza jana katika hafla ya makabidhiano ya dhahabu za Tanzania zilizokamatwa Kenya, iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Sal... | kitaifa |
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba amesisitiza kuwa zuio la mifuko ya plastiki, litakuwa la kisheria na hivyo hakutakuwa na msalie mtume.Akizungumza Dar es Salaam jana, January alisisitiza kuwa marufuku ya mifuko hiyo, lengo lake ni kulinda afya za wananchi na mazingira. “... | kitaifa |
WADAU wa usalama barabarani wakiwemo wabunge wameiomba serikali kuangalia upya sheria ya usalama barabarani ya mwaka Sheria ya mwaka 1973 na kubadilisha vipengele ambavyo vimekuwa vikwazo katika kupunguza madhara ya ajali.Akizungumza jijini hapa jana katika mkutano ulioshirikisha wadau, wakiwamo waandishi wa habari ka... | kitaifa |
TIMU sita za netiboli zitacheza Ligi Daraja la Kwanza baada ya kufanya vizuri katika mashindano yaliyomalizika juzi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Bandari mjini Mtwara.Mashindano hayo ya Daraja la Pili yalishirikisha jumla ya timu nane, huku mbili zikishuka daraja wakati zingine nne zikipigwa faini ya Sh 500,000 baada... | michezo |
JUMLA ya makontena 34 yenye seti za meza na viti 22,000 vimewasili bandarini Zanzibar na vinatarajiwa kuanza kusambazwa katika shule za Unguja na Pemba.Mwenyekiti wa kamati ya madawati kitaifa, Waziri Haroun Ali Suleiman amesema madawati hayo yamewasili kutoka China ambapo yametengenezwa na Kampuni ya Guangzhou Everpr... | kitaifa |
KUTOKANA na ufanisi wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) katika uagizaji wa mbolea kwa pamoja, sasa Bodi ya Sukari imeomba ushirika na wakala huo katika uagizaji sukari.Aidha, PBPA imepanga kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) kuweka utaratibu wa flowmeter katika mabomba yatokayo ba... | uchumi |
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa badhi ya wakazi wa mjini Sumbawanga wanalazimika kutumia pumba za mpunga kupikia chakula baada ya mkaa kupanda kwa kasi.Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mwandishi wa gazeti hili jana mjini hapa, baadhi ya wakazi hao wamekiri kushindwa kununua mkaa huo kwa bei ya kat... | uchumi |
SERIKALI itaendelea kuchukua hatua za kinidhamu na kisheria kwa watumishi wa umma watakaofanya ubadhirifu katika miradi ambayo serikali imeweka fedha nyingi kwa maendeleo.Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William ole Nasha ameyasema hayo alipozungumza na watendaji wa serikali ya mkoa wa Morogoro baada ya k... | kitaifa |
NAHODHA wa timu ya Soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Mbwana Samatta leo anatarajia kuichezea kwa mara ya kwanza Aston Villa tangu akuposajiliwa kutoka Genk ya Ubelgi.Aston Villa inashuka dimbani kumenyana na Leicester City katika mchezo wa nusu fainali ya pili ya Kombe la Carabao utakaofanyika kwenye Uwanja wa Villa Park... | michezo |
Wataalamu hao wakiongozwa na Paolo Mauro, walisema katika taarifa yao jana kwa vyombo vya habari, kuwa hata ukuaji wa uchumi nchini bado ni imara.“Kutokana na mwendelezo mzuri wa sera ya fedha na wa bei za vyakula katika kanda, mfumuko wa bei unatarajiwa kushuka zaidi katikati ya mwaka huu hadi kufikia lengo la muda w... | uchumi |
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Lephy Gembe alitoa mwito huo kwenye mazungumzo yake na Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Robert Paschal alipomtembelea ofisini kwake.Gembe alisema benki hiyo ina wajibu wa kutoa elimu ya kina kuhusu kilimo cha kisasa kwa kutilia mkazo miundombinu muhimu ya kilimo kama vile skimu za... | uchumi |
RAIS John Magufuli amewaagiza wafanyabiashara kulipa kodi kwa wakati, kutotoa rushwa na kuripoti wanapoomba rushwa. Akizungumza na wafanyabiasha Ikulu jana, Rais Magufuli aliwapongeza wafanyabiashara hao kufika katika mkutano huo kwa gharama zao na pia kutoa michango yao kwa lengo la kuboresha huduma za serikali lakin... | kitaifa |
KIKOSI cha vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga leo asubuhi kinatarajiwa kuondoka na msafara wa wachezaji 20 kwenda Iringa kukabiliana na Lipuli katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, bila ya baadhi ya wachezaji wake nyota.Mchezo huo utafanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora keshokutwa. Katika msafara huo ... | michezo |
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla amesema kuwa Rais ameridhia hifadhi tatu mpya kuingizwa katika orodha ya Hifadhi za Taifa.Alibainisha hayo jana wakati akihitimisha na kujibu hoja mbalimbali za wabunge waliochangia katika hotuba yake ya makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2019/2020.“... | kitaifa |
KOCHA wa mabingwa wa soka wa Tanzania Bara Simba, Patrick Aussems bado ubingwa uko wazi kati yao na wapinzani wao wakubwa Yanga. Simba inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 45 baada ya kucheza mechi 18 wakiwa nyuma ya Azam wanayoshika nafasi ya pili kwa pointi sita.Yanga inaendelea kuongo... | michezo |
WASOMI wamesema kauli ya ‘maagizo kutoka juu’ iliyokuwa ikitumiwa na baadhi ya watumishi wa umma, ililenga kuwashughulikia wananchi kama wahalifu.Kauli hiyo ambayo imekuwa ikutumiwa na baadhi ya watumishi wa umma, imezua gumzo nchini baada ya Rais John Magufuli kupitia ujumbe wake wa Mwaka Mpya kwa taifa, kuwataka wat... | kitaifa |
['Mshambuliaji wa Liverpool Divock Origi ametia saini kandarasi ya muda mrefu na Liverpool. ', 'Raia huyo wa Ubelgiji, mwenye umri wa miaka 24, alijiunga na Liverpool kutoka Lille 2014 kwa mkataba wa miaka mitano kabla ya kuhudumu misimu miwili kwa mkopo. ', 'Lakini alirudi na matokeo mazuri akifunga mara mbili dhidi ... | michezo |
SHIRIKA la Ndege Tanzania (ATCL) ni moja ya sekta zilizonufaika na Mkutano wa 39 wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliomalizika jana jijini Dar es Salaam.Aidha, shirika hilo limeazimia kumaliza changamoto za ucheleweshaji wa safari, uahirishaji wa safari na utoaji wa taarifa kwa abiria pindi kun... | uchumi |
NAIBU Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (pichani) amezitaka kampuni zinazotakiwa kulipa fi dia katika maeneo ya uchimbaji kufanya hivyo kwa wakati ili kuondoa migongano na wananchi.Nyongo alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga (CCM) aliyetaka kujua lini serikali itawalipa fidia wananch... | kitaifa |
KATIKA mchezo wa jana, kati ya Simba na Yanga kulishuhudia matukio matano kabla ya mchezo huo kuanza, Yanga kugoma kuingia kushuka katika basi lao.-Yanga walifika Uwanja wa Taifa saa 9:25 alasiri, lakini wachezaji wao walikaa ndani ya gari kwa takriani dakika 20, huku baadhi ya makomandoo wakiwafukuza waandishi wa hab... | michezo |
MKURUGENZI wa Jiji la Arusha, Dk Maulid Madeni amesema wakuu wa idara jijini humo, wamekosea kugawa vitambulisho vya wafanyabiashara ndogo kwa kuwafuata wafanyabiashara hao ndani ya masoko, badala ya nje ya masoko.Madeni ameyasema hayo jana katika baraza la madiwani la Jiji la Arusha ambapo baadhi ya madiwani wa jiji ... | kitaifa |
['Nyota wa soka Cristiano Ronaldo hatakabiliwa na shtaka lolote baada ya kutuhumiwa na madai ya unyanyasaji wa kingono, waendesha mashtaka wa Marekani wamesema.', 'Kathryn Mayorga, 34, alidai kuwa mchezaji huyo wa klabu ya Juventus alimbaka katika hoteli moja mjini Las Vegas mwaka 2009.', 'Iliripotiwa kuwa Bi Mayorga a... | michezo |
JESHI la Polisi mkoani Katavi linawasaka askari wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) kwa tuhuma za kuwapiga risasi na kuwajeruhi vibaya watu watano, wanne kati yao wakiwa ndugu wa familia moja ambao ni wakazi wa kijiji cha Ikongwe kilichopo katika wilaya ya Mpanda .Watu hao wamelazwa Hospitali Teule ya mkoa wa Katavi i... | kitaifa |
.Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa vyama vya siasa nchini havijazuliliwa kufanya shughuli zake za kisiasa kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.Akijibu maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu Bungeni jijini Dodoma, Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa utaratibu uliopo sasa unaoonekana kama kuvinyima nafasi vyama vya ... | kitaifa |
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amekemea tabia ya baadhi ya halmashauri kuuza viwanja kwa bei jambo ambalo amesema itakuwa vigumu masikini kumilika ardhi iliyopangwa.Lukuvi aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wataalamu wa ardhi nchini wapatao 800 ambao wamekutana jijini hapa kwa kwa ... | kitaifa |
RAIS John Magufuli ametoboa siri ya kumkabidhi Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, kamusi na vitabu vya kusoma na kujifunza lugha ya Kiswahili viliyoandikwa na walimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwa hatua hiyo itasaidia kukuza lugha hiyo kwa kasi.Marais hao wawili walikutana juzi na kufanya mazungumzo katika ... | kitaifa |
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk Agness Kijazi ameibuka kidedea kwa kuchaguliwa kuwa Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) kwa kipindi cha miaka minne 2019-2022.Dk Kijazi ambaye ni mwakilishi wa kudumu Tanzania katika Shirika hilo anakuwa mwanamke wa kwanza na mju... | kitaifa |
OFISI ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imekiri kuwepo kwa changamoto nyingi baada ya serikali kuanzisha mfumo wa elimu bila malipo kwa shule za msingi.Akijibu swali la mbunge wa Handeni, Omar Kigoda (CCM), Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tamisemi, Mwita Waitara amesema serikali imejipanga kutatua ... | kitaifa |
WIZARA ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi ya Zanzibar imesema njia pekee ya wakulima kupiga hatua kubwa ya uzalishaji wa mpunga ni kutumia kilimo cha umwagiliaji.Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, Rashid Ali Juma alisema kilimo cha umwagiliaji ndio mkombozi wa wakulima ambao kwa sasa wanaweza kulima muda... | kitaifa |
CHAMA cha Wakulima wa Zabibu na Masoko Mpunguzi (UWAZAMAM) jijini hapa, kimeipongeza serikali kwa kupunguza tozo ya ushuru wa mchuzi wa zabibu kutoka Sh 3,315 hadi 450, kikisema hatua hiyo itainua uchumi wa mkoa na wakulima wa zao hilo.Hata hivyo, Uwazamam kimewaomba wanunuzi wa mchuzi huo, kuongeza bei kutoka Sh 1,54... | uchumi |
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewaweka kitimoto wakuu wa idara mbalimbali zilizopo katika halmashauri za wilaya na jiji hilo kwa kuwataka kujiandaa na uhamisho kwenda mikoani endapo idara zao zitabainika kukwamisha miradi mbalimbali.Akizungumza katika kikao cha dharura cha Baraza la Madiwani la Halmasha... | kitaifa |
WATU wawili wameuawa katika matukio tofauti wilayani Muleba mkoani Kagera kwa imani za kishirikina na kujichukulia sheria mkononi akiwemo mtoto aliyenyofolewa sehemu zake za siri. Kamanda wa polisi Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi amethibitisha kutokea kwa matukio hayo na kwamba mtu mmoja anashikiliwa na polisi, mkoan... | kitaifa |
WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo ameuagiza uongozi wa manispaa ya Morogoro na mkandarasi wa ujenzi wa majengo ya Shule ya Sekondari Mji Mpya mkoani hapa kukamilisha ujenzi huo Agosti 30, mwaka huu ili wanafunzi waanze kusoma.Waziri huyo alitoa agizo hilo hi... | kitaifa |
LEO ni tarehe 28 Desemba, zimebaki siku tatu tu kabla ya kukamilisha mwaka 2019 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2020, tunamuomba Mwenyezi Mungu atujaalie kuumaliza mwaka huu na kuingia mwaka mpya salama.Wakati mwaka 2019 unaelekea ukingoni kuna matukio mengi ya kukumbukwa ambayo yametokea katika anga la michezo na burud... | michezo |
Akifunga mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uelewa wajasiriamali wakubwa na wakati juu ya mpango wa serikali wa kuishirikisha sekta binafsi katika miradi mikubwa kupitia PPP Dar es Salaam jana, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Profesa Adolf Mkenda, aliwaeleza washiriki kuwa, kuna sheria inayoongoza ubia kati ya s... | uchumi |
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea na semina kwa wajasiriamali wadogo katika Wilaya ya Lushoto kuhusu utekelezaji wa viwango vya kitaifa kwa bidhaa zinazozalishwa na zinazosindikwa.Pia wajasiriamali hao wamepatiwa elimu ya namna ya kupata alama ya ubora kwenye bidhaa wanazozalisha bure bila gharama yoyote.S... | uchumi |
Alisema shirika litaendelea kugawa faida inayopatikana kutokana na zao hilo kwa kusaidia maendeleo ya jamii kwa kila hali inaporuhusu na fursa inapopatikana ili kujenga imani ya wananchi kuipenda ZSTC na kulipenda zao la karafuu ambapo ndio zao kuu la uchumi Zanzibar.Bai aliyasema hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mwendesh... | uchumi |
KATIBU Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Dk Stergomena Tax (pichani) amesema Tanzania ni nchi pekee katika jumuiya hiyo, iliyofanikiwa kufi kia kigezo kilichowekwa na jumuiya cha kufi kia ukuaji wa uchumi wa asilimia saba.Dk Tax amesema SADC imejiwekea vigezo vya uchumi mpana wa kufikia asilim... | uchumi |
WAKAZI wawili wa Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma, Patrick Chirwa maarufu kwa jina la Boy (42), mkazi wa Lizaboni na Ramadhani Nivya (41), mkazi wa Ruhuwiko wamehukumiwa kwenda jela miaka 15 wote wawili katika kesi ya uhujumu uchumi baada ya kupatikana na betri mbili zinazotumika kuchaji betri zinazotumika kwenye nde... | kitaifa |
WAKATI michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara ikiendelea kupamba moto, huku tukishuhudia mtifuano mkubwa wa mbio za marathon kwa mafahali wawili Simba na Yanga, kila mmoja wao akijinasibu kushinda michezo iliyobaki kuhakikisha anatwaa taji hilo msimu huu.Lakini vita nyingine ni kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho la Aza... | kitaifa |
SIMBA jana ilikuwa uwanjani Dar es Salaam ikimenyana na African Lyon kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara katika harakati zake za kutetea taji lake. Katika mechi hiyo Simba ilishinda 2-1.Lakini wakati mabingwa hao watetezi wakipigania taji hilo, kuna kila dalili uongozi wa klabu hiyo kuachana na kocha wake msaidizi Mrundi Ma... | michezo |
Jiji la Dodoma litaweza kujitegemea kimapato ifi kapo mwaka 2021.“Jiji la Dodoma ifikapo mwaka 2021 jiji hilo litakuwa likijitegemea kwa mapato ya ndani,” amesema Mkurugenzi wa jiji hilo, Godwin Kunambi.Amesema kwa kuwa Dodoma inatekeleza ahadi ya serikali kuhamishia makao makuu ya nchi mkoani humo, halmashauri inatek... | uchumi |
Ofisa Mwandamizi Mkuu Elimu wa TRA, Hamis Lupenja alisema hayo wakati wa semina ya waandishi wa habari iliyofanyika jijini hapa mwishoni mwa wiki.“Vituo vya mafuta hawatoi risiti za TRA licha ya baadhi yao kuwa mashine za EFD’s, katika kukabiliana na hilo utaratibu wa kufunga kifaa cha kodi ndani ya pampu ili kuondoa ... | uchumi |
TANZANIA imepanda kwa nafasi sita katika ubora wa viwango vya Fifa vilivyotolewa jana. Kwa mujibu wa viwango hivyo vilivyo kwenye tovuti rasmi ya Fifa, Tanzania imepaa kutoka nafasi ya 137 iliyokuwa mwezi uliopita mpaka nafasi ya 131.Kupanda kwenye viwango hivyo kumetokana na timu ya taifa, Taifa Stars kufuzu fainali ... | michezo |
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ndiye anayetarajia kukabidhi bendera ya taifa na kuiaga rasmi timu hiyo.Alisema kuwa msafara wa timu hiyo, ambao utaongozwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini, Dk... | michezo |
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kutoa uamuzi katika kesi ya utakatishaji fedha inayowakabili aliyekuwa Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na wenzake kama wana kesi ya kujibu au la.Hatua hiyo imekuja baada ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, kusema bado hajamaliza kuandika uamuzi wa kesi hiyo. Septemba 2, m... | michezo |
WABUNGE nchini wamemmwagia sifa Rais John Magufuli kwa kufi kiria Taifa hili litakuaje miaka 50 ijayo na kuwataka Watanzania wasijifi kirie wao binafsi, bali Taifa na hatima yake.Aidha, wabunge hao wamesema uwezo wa kufikiri wa Rais Magufuli ni mkubwa kwa kubuni miradi ya kimkakati, ambayo inaiweka nchi katika ramani ... | kitaifa |
Lipuli ilikuwa ya kwanza kupata bao la lililofungwa na Adam Salamba dakika ya 32 na Simba wakisawazisha dakika ya 66 likifungwa na Laudit Mavugo.Simba itaendelea kuwa kileleni mwa msimamo ikifikisha pointi 59 katika michezo 25 iliyocheza huku mahasimu wao Yanga wanaotarajiwa kucheza leo wakiendelea kuwa katika nafasi ... | michezo |
Hayo yalisemwa na Ntibenda wakati alipowahutubia wafanyakazi katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani kimkoa yaliyofanyika jana Viwanja vya Shehe Amri Abeid jijini Arusha. Aliwasihi wafanyakazi kutumia vyema vyama vya wafanyakazi mahali pa kazi ili walete maendeleo kati ya waajiri pamoja na wafanyakazi wenyew... | uchumi |
JESHI la Polisi Wilaya ya Igunga mkoani Tabora limefanikiwa kuwakamata baadhi ya vijana wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu, ikiwemo wizi wa kutumia funguo za bandia kwa kufungua milango ya wananchi wanapokuwa wamelala nyakati za usiku.Hayo yalisemwa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Igunga, Ally Mkalipa alipokuwa akizung... | kitaifa |
IKIWA imesalia siku moja kabla ya Yanga kuumana na wapinzani wao, Township Rollers katika kuwania kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, timu hiyo imejinasibu kuwa ipo tayari kupambana kuhakikisha inapata matokeo na kusonga mbele kulingana na maandalizi waliyokuwa nayo.Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera ameeleza kuwa ... | michezo |
Tuzo Mapunda SIMBA imeanza vyema msimu huu baada ya kuifunga Azam mabao 4-2 katika mechi ya Ngao ya Jamii iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana.Mechi hiyo inayoashiria kufungua pazia la Ligi Kuu Bara hushirikisha bingwa wa Ligi Kuu (Simba na bingwa wa Kombe la FA (Azam).Simba sasa inatwaa ubingwa huo ... | michezo |
Naibu Kamishna wa Forodha, Patrick Kisaka ametaja mali hizo kuwa ni mifuko 40 ya sukari kutoka Brazil, ndoo 20 za mafuta ya kupikia kutoka Mashariki ya Mbali na katoni 70 za vigae, ambavyo maofisa wa TRA kwa kushirikiana na askari wa doria, walivikamata Januari 8 katika bandari hiyo.Akizungumza na waandishi wa habari ... | uchumi |
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Kigoma kimesema tofauti ya kiitikadi iliyopo baina ya vyama vya siasa mkoani humo na nchini kwa jumla isiwe sababu ya kuleta utengano na kuvuruga ushirikiano walio nao Watanzania tangu nchi ipate uhuru.Mwenyekiti wa Chadema Mkoa, Ally Kisala alitoa kauli hiyo katika ... | kitaifa |
Hatua hiyo imeelezewa kuwa ni sehemu ya mkakati wa benki hiyo kuhakikisha inawarahisishia wateja wake upatikanaji wa huduma zake kupitia teknolojia ya mawasiliano.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati wa kuzindua kituo hicho, Meneja Mwandamizi Huduma kwa wateja wa Exim, Frank... | uchumi |
['Mchezaji wa kiungo cha kati wa Ufaransa Paul Pogba, mwenye umri wa miaka 26, bado ana hamu kubwa ya kutaka kuondoka Manchester United kuelekea Real Madrid msimu huu wa joto. (Marca) ', 'Beki wa kati wa England Harry Maguire, mwenye miaka 26, amekataa pendekezo la thamani ya £278,000 kwa wiki kutoka Manchester City ba... | michezo |
BAADA ya kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa Gor Mahia FC katika mchezo wa makundi wa michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, mashabiki na wanachama wa Yanga wameutaka uongozi kufanya uamuzi mgumu kwa kusafisha upya kikosi.Kipigo hicho cha ugenini kimemtoa hadharani mchezaji wa zamani wa Yanga, Abeid Mziba akieleza kutori... | michezo |
Msaada huo ni kwa ajili ya kuwatambua na kuwasaidia wafanyabiashara, wanaofuata sheria ili wafanye biashara zao kiurahisi.Pia, mamlaka hizo zimetakiwa kupambana na wafanyabiashara wasiofuata sheria kwa kuwaelimisha juu ya kutumia njia sahihi za kufanya biashara ndani na nje ya nchi .Akizungumza Dar es Salaam jana, Mku... | uchumi |
KOCHA wa Yanga, Mwinyi Zahera amemvua kitambaa cha unahodha mlinzi Kelvin Yondani na kumkabidhi mshambuliaji Ibrahim Ajibu kutokana na utovu wa nidhamu baada ya kuchelewa kuripoti kambini.“Nilitoa siku tano za mapumziko baada ya mechi na Mbeya City lakini yeye kama nahodha hakuripoti kambini baada ya siku hizo na haja... | michezo |
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.