content stringlengths 1k 24.2k | category stringclasses 6
values |
|---|---|
Shughuli hiyo imefanyika kwa lengo la kuonesha njia vijana kufikia malengo yao na kuinua jamii inayowazunguka. Bucha yake ipo katika stendi ya mabasi ya Ngerengere, Morogoro.Akizungumza wakati wa ukarabati wa bucha hiyo, Ofisa Mauzo wa Airtel, Aminata Keita alisema: “Airtel tunajali sana jamii yetu inayotuzunguka hivy... | uchumi |
MENEJA wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA) Kanda ya Kati, Stella Rutaguza ameonya kampuni zinazofanya biashara ya bima na kuzitaka kuacha tabia ya kutoza ada za bima chini ya kiwango kilichowekwa na Serikali.Rutaguza ametoa onyo hilo katika kikao kilichokutanisha TIRA na mameneja na wawakilishi wa kampuni, zinazofa... | kitaifa |
Katika mechi hiyo ya kirafiki ya kimataifa iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, Msuva alikuwa mwiba mchungu kwa Botswana na mabao yake hayo yaliipa Stars ushindi wa mabao 2-0.Kwa matokeo hayo, Stars imejiweka kwenye mazingira mazuri ya kukwea kwenye viwango vya Fifa. Msuva alianza kupeleka shangwe kwa mas... | michezo |
['Real Madrid inawafuatilia winga wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho, 19 na mshambuliaji wa Norway wa miaka 19- Erling Braut Haaland, anayechezea Red Bull Salzburg. (El Desmarque, via Mail)', 'Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anataka kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani na RB Leipzig Timo Werne... | michezo |
GOLIKIPA wa Azam FC, Razak Abalora amesema anaamini siku zote kuwa yeye ni mshindi licha ya kukosa penalti ya mwisho kwenye mchezo wa jana, huku kipa wa Simba Beno Kakolanya akisema alishajiwekea uhakika kwenye penalti tano, lazima aokoe mbili au moja.Makipa hao timu zao zilikutana juzi katika mchezo wa nusu fainali u... | michezo |
KOCHA wa timu ya soka ya taifa ya wanawake ya Tanzania Bara Kilimanjaro Queens, Bakari Shime amesema wanataka kuweka historia mpya katika michuano ya chalenji ya Afrika Mashariki na Kati kwa kuchukua kombe kwa mara ya tatu mfululizo.Michuano hiyo itakayoshirikisha nchi nane za Afrika Mashariki na Kati inatarajiwa kuti... | michezo |
WAZIRI wa Maji, Profesa Makame Mbarawa amesema mtandao wa ufisadi kwenye miradi ya maji una mizizi mirefu kuanzia ngazi za wilaya, halmashauri, mkoa hadi wizarani, jambo linalofanya miradi ya maji kutekelezwa kwa gharama kubwa.Aliyasema hayo Dar es Salaam wakati akishuhudia utiaji saini wa miradi sita ya maji kati ya ... | kitaifa |
AFC ni moja ya timu kongwe jijini Arusha na ni moja ya timu yenye historia kubwa mkoani humo, lakini ni moja ya timu yenye kucheza Ligi Daraja la Kwanza katika mazingira magumu sana baada ya wadau na mashabiki kusuasua kuichangia timu hiyo.Timu hiyo ya Arusha ni ya wanachana na wanachama wake hawazidi 100 na ni timu p... | michezo |
BODI ya Michezo ya Kubahatisha imesema katika kuhakikisha inadhibiti michezo hiyo imekamata mashine 500 za kamari zilizokuwa zimefungwa maeneo yasiyoruhusiwa na kuruhusu watoto chini ya miaka 18 kucheza michezo hiyo.Aidha, kuna kitengo maalumu cha malalamiko kwa mitandao ya simu inayosumbua watumiaji wa simu kwa kutum... | kitaifa |
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dk Adelhelm Meru aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kuwa hatua hiyo ni muhimu katika undelezaji wa eneo huru la bandari ya Mtwara. EPZA inaendeleza hekta 10 za eneo huru la bandari ya Mtwara.Hekta hizo ni kati ya jumla ya hekta 110 za eneo hilo huru l... | uchumi |
JUMUIYA ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) inatarajia kurejesha Tuzo ya Meya Bora, itakayodhaminiwa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN). Aidha, ALAT imeweka mkakati wa kujenga jengo la kitega uchumi baada ya kukamilisha ujenzi wa jengo la ofisi ndogo eneo la Tambukareli baada ya mwisho wa mwezi huu.Mratibu wa Tuz... | kitaifa |
UKITAZAMA kwa jicho la tatu, mwenendo wa mbio za marathon za kuwania ubingwa kwenye Ligi Kuu ya England (EPL) kati ya Manchester City na Liverpool, ilikuwa patashika ya nguo kuchanika, kwani City ilifanikiwa kubeba ubingwa huo kwa tofauti ya pointi moja dhidi ya mpinzani wake Liverpool.Mfano huo unaweza kuuleta Tanzan... | michezo |
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imemtaka mwandishi wa Kampuni ya Clouds Media, Abdi Chembeya kufika mahakamani hapo Mei 14, mwaka huu kutoa ushahidi katika kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema).Awali, Wakili wa Serikali, Patrick Mwita alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Hur... | kitaifa |
Hayo yalisema juzi jijini Dar es Salaam na Waziri wa Uchumi na Nishati wa Ujerumani, Matthias Machnig wakati ujumbe wa wafanyabiashara wa Ujerumani ulipokutana na Mtendaji Mkuu Ofisi ya Rais-Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Miradi (PDB) inayosimamia BRN, Omari Issa.“Ubunifu huu wa utekelezaji wa miradi kupitia BRN ni jam... | uchumi |
AZAM FC jana ilishindwa kutamba mbele ya Coastal Union baada ya kuachia pointi zote tatu kwa Wagosi hao kwa kukubali kipigo cha bao 1-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.Ushindi wa wenyeji Union ulipatikana kupitia bao pekee lililowekwa kimiani na mchezaji wake Haji U... | michezo |
MAMA wa binti wa miaka 17 aliyeeleza jinsi alivyofanyiwa ukatili na mwajiri wake ikiwa ni pamoja na kutumbukizwa mwiko katika sehemu zake za siri, amesema kwamba maagizo wa Polisi wa Chamwino kurejea Dar es salaam, kunafanya ufuatiliaji wa shauri la mwanae kuwa gumu.“Nimefika hapa na kupelekwa Polisi , lakini wanasema... | kitaifa |
Ushindi huo umefuta ubabe wa Lipuli iliyowasumbua katika mchezo wa raundi ya kwanza uliochezwa Dar es Salaam, ambapo walitoka sare ya bao 1-1 lakini pia, iliondoa ile dhana ya kutokufungwa kwenye Uwanja wa Samora.Mabao ya Yanga yalifungwa na Papy Kabamba Tshishimbi na Pius Buswita. Ushindi huo wa Yanga unafikisha juml... | michezo |
MAMLAKA ya hali ya Hewa nchini (TMA), imewatoa hofu wananchi kuhusu mvua zilizonyesha kuwa ni za kipindi kifupi zikiambatana na upepo kwa baadhi ya maeneo.Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisa Uhusiano wa TMA, Monica Mutoni, jana, mvua hizo zimenyesha kwa siku moja (jana) na kwamba upo uwezekano mkubwa wa kutoendelea kunyesh... | kitaifa |
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema ameridhishwa na kasi na viwango vya ujenzi wa mfumo wa Reli ya Kisasa (SGR) inayojengwa na Kampuni ya Yapi Merkezi ya Uturuki.Makonda ameyasema hayo alipotembelea mradi wa ujenzi wa reli hiyo ya kisasa kipande cha kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro chenye urefu wa ki... | kitaifa |
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mkongo Heritier Makambo amesema ameamini timu hiyo ni kubwa kuliko wachezaji kutokana na kile alichokishuhudia juzi kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro.Makambo aliyejiunga na timu hiyo msimu huu akitokea Lupopo ya DR Congo alisema tukio alilolishuhudia uwepo wa mashabiki wengi wakijitokeza kumuaga... | michezo |
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo, Ofisa Mkuu wa Biashara Airtel, Arindam Chakrabary alisema wanatoa mikopo ili mawakala wapate fursa ya kukuza biashara zao na kuongeza mitaji.Huduma hii ya mikopo kwa mawakala itawanufaisha mawakala zaidi ya 20,000 nchi nzima. Chakrabarty alikumbusha kuwa mwaka jana walizind... | uchumi |
JIMBO la Ruangwa mkoani Lindi linajiandaa kupata kiwanda cha kutengeneza betri za simu.Msaidizi wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye masuala ya jimbo, Fadhil Liwaka amesema, kiwanda hicho kitapata malighafi wilayani humo hivyo kushawishi uwekezaji wa viwanda vya simu.“Kwa hiyo ndio kusema kwamba kiwanda hiki cha kute... | uchumi |
['Ndoto ya Watanzania kuona raia wa kwanza wa taifa hilo kucheza kwenye makundi ya michuano ya Klabu Bingwa barani Ulaya (Champions League) inaweza isitimie hii leo. ', 'Mshambuliaji na nahodha wa Tanzania Mbwana Samatta kupitia klabu yake ya Genk ya Ubelgiji amefanikiwa kufuzu kutinga hatua ya makundi, lakini hii leo ... | michezo |
Hali hiyo inatokana na vyama vya msingi vya mazao ambavyo ndiyo mawakala wa ukusanyaji wa korosho kukosa sifa za kukopesheka na vyombo vya fedha.Ofisa Kilimo, Mifugo na Ushirika wa wilaya hiyo Chiza Marando, alimweleza mwandishi wa habari hii mjini Tunduru juzi kuwa, katika misimu miwili iliyopita wakulima wa wilaya h... | uchumi |
Imeelezwa kuwa watu hao huenda kinyume na taratibu za wachimbaji wadogo, katika kuchimba na kuuza madini hayo wakifanya hivyo kwa hila bila kutambuliwa rasmi.Kauli hiyo imetolewa na Kamishna wa Madini Tanzania, Paul Masanja, ambaye aliongeza kuwa utaratibu huo unaotumiwa na wawekezaji ni wa kienyeji na unalitia Taifa ... | uchumi |
NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye amesema serikali inalitambua deni la Sh milioni 241 ambalo Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) inadaiwa na Mamlaka ya Viwanja vye Ndege Zanzibar na kuahidi kulilipa. Nditiye aliyasema hayo wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Baraza la Wawakilish... | kitaifa |
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imesitisha usikilizwaji wa rufaa iliyokatwa na washitakiwa, Freeman Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko kupinga maamuzi ya Mahakama ya Kisutu ya kuwafutia dhamana.Washitakiwa hao walifikishwa katika Mahak... | kitaifa |
WAKATI Ligi Kuu Tanzania Bara ikisimama kwa wiki mbili kupisha mashindano ya kimataifa, uwepo wa ushindani mkali msimu huu tofauti na huko nyuma ni moja ya mambo yanayozungumzwa zaidi.Hadi sasa ligi hiyo ipo kwenye raundi ya 10 lakini utofauti uliopo kinara wa ligi hiyo Simba SC anayeongoza kwa pointi 22 amepishana kw... | michezo |
Huo utakuwa mchezo wa pili baada ya mwishoni mwa wiki iliyopita kucheza na Morocco na kushinda bao 1-0, ushindi ulioshuhudiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.Wapinzani wa Ngorongoro, Msumbiji juzi walicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Morocco kwenye Uwanja wa Uhuru na kuifunga bao 1-0.Hivyo, sio timu ya kubeza na ni ki... | michezo |
NAIBU Waziri wa Nishati, Subira Mgalu aliamsha shangwe za wananchi wa Kijiji cha Chiboli wilayani Chamwino, mkoani Dodoma baada ya kuwasha umeme katika kijiji hicho. Naibu Waziri huyo, aliwasha umeme katika zahanati ya kijiji hicho pamoja na kisima cha maji ambapo kijiji hicho kimepata umeme kupitia mradi wa Backbone ... | kitaifa |
KOCHA mkuu wa timu ya Soka ya taifa ya wanawake Tanzania Bara, Kilimanjaro Queens ,Bakari Shime amesema morali ya kikosi hicho ipo juu tayari kwa kuwakabili Sudan Kusini kwenye mchezo wao wa kwanza wa kundi A katika michuano ya kombe la Chalenji.Michuano hiyo inayofanyika chini ya usimamizi wa Baraza la vyama vya soka... | michezo |
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeingia mkataba wa mwaka mmoja na Ettiene Ndayiragije kuwa Kocha Mkuu wa Taifa Stars. Kabla ya uteuzi huo uliofanywa na Kamati ya Utendaji ya TFF, Ndayiragije alikuwa kocha wa muda wa Taifa Stars akisaidiwa na mzawa Suleman Matola na Juma Mgunda. Akizungumza jana Ofisa Hab... | michezo |
Alisema Benki hiyo iko kwenye mikakati ya kuanzisha mradi wa kunenepusha ng’ombe. “Tutawakopesha fedha kwa ajili ya kuuza minadani, mpango huu ulianza na mkoa wa Arusha na walifanya vizuri kwani mafanikio yalionekana” alisema Alisema jamii ya wafugaji ya kimasai wanamiliki mifugo mingi na kama benki waliona kuna umuhi... | uchumi |
Meneja wa Posta Mkoa wa Tanga, Rehema Marijni alitoa mwito huo jana wakati akielimisha wananchi waliotembelea banda la shirika hilo kwenye Maonesho ya Tatu ya Biashara Tanga yanayoendelea katika viwanja vya Mwahako.Alisema licha ya kufikiwa kwa maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasilianob (Tehama) ambayo yamesaba... | uchumi |
Trevelport ni kampuni ya kimataifa inayojihusisha kupatia mashirika ya ndege duniani mifumo ya ukataji wa tiketi.Mathew alisema kuna kodi nyingi sana zinazotozwa mashirika yanayotoa huduma za usafiri wa anga lakini mwisho wa siku mzigo wa kodi hizo anabebeshwa Mtanzania wa kawaida anapotaka kutumia huduma hizo kama ku... | uchumi |
Timu hiyo ilipata bao hilo dakika ya nne ya mchezo.Bao hilo ambalo liliongeza kasi ya ushambulizi kwa pande zote mbili liliwekwa kimiyani na mchezaji Hamad Mshamata na kuifanya timu yake kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao hilo.Kurudi katika kipindi cha pili miamba hiyo iliendelea kushambuliana kwa zamu huku kila upa... | michezo |
LICHA ya kuwafunga waajiri wake wazamani Yanga, Mshambuliaji wa Azam FC , Obrey Chirwa (pichani) ameonesha kutoridhika na hali hiyo na kudai kuwa anaitaka Yanga yenyewe iliyotimia akimaanisha ile ya wakubwa.Chirwa alifunga bao la tatu katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi juzi dhidi ya Yanga, mchezo ulioisha kwa mabingw... | kitaifa |
Nuh, ambaye mara zote amekuwa akiimba nyimbo za mapenzi, amesema nyimbo zote anazoimba huwa zinaendana na historia yake ya kweli kwenye mapenzi.Akizungumza kwenye mahojiano maalumu juzi, Nuh alisema kwamba sio pamoja na uwepo wa wimbo wa Jike Shupa lakini tayari ameimba wimbo mwingine unaitwa Upofu ambao unaendana na ... | michezo |
['Alexis Sanchez anakataa kuondoka Manchester United msimu huu, pamoja na kwamba kocha Ole Gunnar Solskjaer kutishia kumfanya kuwa mchezaji wa akiba ikiwa atasalia na timu hiyo. Roma inatafuta wachezaji wengine. (Sun)', 'Hatahivyo, timu ya Serie A, AC Milan, Juventus na Napoli bado wana mpango wa kumsajili mshambuliaji... | michezo |
VINARA wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara Yanga wamehamishia nguvu zao kwa maandalizi ya mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam (FA) dhidi ya Biashara United utakaochezwa wiki ijayo.Vijana hao wa Jangwani walitolewa mapema katika michuano ya wadhamini wao, portPesa na timu ya Kenya ya Kariobang Sharks kwa mabao 3-2 na sasa... | kitaifa |
UTALII ni sekta muhimu kwa ukuaji wa uchumi nchini Tanzania. Inachangia zaidi ya asilimia 17 ya pato la taifa. Katika mwaka wa fedha wa 2016/2017, sekta ya utalii ilichangia asilimia 17.5 ya pato la taifa huku ikiliingizia asilimia 25 ya fedha za kigeni.Katika kipindi hicho, ilichangia ajira 500,000 za moja kwa moja n... | kitaifa |
ATCL itakuwa ikitumia ndege yake aina ya Bombardier Dash - 8 yenye uwezo wa kubeba abiria 50 katika njia hiyo.Ikitokea Dar es Salaam kwenda Arusha, alikuwemo Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu na wakati wa kutoka Zanzibar kwenda Dar es Salaam, alipanda Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais (Utawala Bora) wa S... | uchumi |
['Miamba ya soka Uhispania klabu ya Barcelona imemsajili msahmbuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann kutoka klabu pinzani ya Atletico Madrid kwa kitita cha euro milioni 120. ', 'Mshambuliaji huyo mwenye miaka 28 alikuwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa kilichonyakua kombe la dunia mwaka jana. ', "Griezmann... | michezo |
MWANARIADHA Joshua Cheptegei amekuwa Mganda wa kwanza kuwa bingwa wa dunia wa mbio za nyika katika historia baada ya kumshinda Mganda mwenzake Jacob Kiplimo na bingwa mtetezi mara mbili Mkenya Geoffrey Kamworor kwa muda wa 10,240.Lakini pamoja na ahadi aliyopewa katika hafla iliyofanyika Kololo miaka miwili iliyopita,... | kitaifa |
WATU 13 kati ya 15 waliokufa papo hapo katika ajali iliyohusisha magari mawili baada ya kugongana uso kwa uso kwenye kitongoji cha Gokora, Kata ya Komaswa tarafa ya Inano Wilaya ya Tarime mkoani Mara, watazikwa pamoja eneo hilo la ajali baada ya miili yao kuharibika vibaya.Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ki... | kitaifa |
MKOA wa Kilimanjaro umetenga ekari 4,296 kwa ajili ya shughuli za uwekezaji, katika wilaya za Moshi na Siha na kuomba wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuchangamkia fursa hiyo.Aidha katika utekelezaji wa agizo la Serikali la uanzishwaji wa viwanda 100 kila mkoa, tayari mkoa huo umeanzisha viwanda vipya 74 kwa kipindi... | uchumi |
Hayo yamo kwenye taarifa iliyotolewa jana wakati benki hiyo ikisherehekea miaka mitatu ya utoaji wa huduma kwa wateja.Akizungumza na Wakurugenzi wa Bodi, Wafanyakazi na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kusherehekea mafanikio hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja alisema wamepata mafanikio... | uchumi |
RAIS John Magufuli amewapongeza wananchi wa Chato mkoani Geita kwa kuitikia mwito wa serikali wa kuongeza juhudi katika kazi za uzalishaji mali, hali iliyoiwezesha wilaya hiyo kupiga hatua kubwa za kimaendeleo.Rais Magufuli alitoa pongezi jana wakati akiwasalimu wananchi hao katika eneo la Njiapanda, muda mfupi baada ... | kitaifa |
Aliweka jiwe la msingi la viwanda hivyo jana akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza. Viwanda hivyo vinatengeneza steel wire, pipi, vifungashio aina ya viroba.“Nampongeza Lameck Airo, Mbunge wa Rorya na Mwenyekiti wa Kampuni ya Lakairo Investment kwa kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu y... | uchumi |
KOCHA Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema baada ya mshambuliaji wake Haritier Makambo kupata ofa katika klabu ya Horoya AC ya Guinea alimuomba amsindikize ili asitapeliwe.Zahera aliyerejea jana alfajiri na mchezaji huyo wakitokea Guinea aliweka wazi kuwa hakwenda huko kwa mapenzi yake mwenyewe bali mchezaji ndiye aliy... | michezo |
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) yenye jukumu la kukadiria, kukusanya na kuhasibu mapato ya serikali, ni miongoni mwa taasisi za umma zilizo mstari wa mbele kumuunga mkono Rais John Magufuli kwa vitendo katika kutekeleza azma ya serikali ya kuleta maendeleo.Serikali ya awamu ya tano katika kipindi cha miaka mitatu, im... | kitaifa |
WAZIRI wa Nishati, Dk Medard Kalemani amewataka watu kushiriki michezo ili kujenga afya bora zitakazowawezesha kufanya kazi kwa bidii na kuinua uchumi wa nchi.Hayo aliyasema mjini hapa wakati wa maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Kimataifa ya Olimpiki iliyofanyika wilayani Chato mkoani Geita na kushirikisha zaidi ya wa... | michezo |
WABUNGE wameonesha kukerwa na kutokamilika kwa mazungumzo na kampuni ya China inayotaka kuwekeza bandari ya Bagamoyo kwa takribani miaka saba sasa.Aidha wamesema mazungumzo hayo yaliyofanyika kwa miaka saba sasa huku nchi nyingine zikikamilisha miradi kama hiyo katika muda mfupi ni dalili kwamba kundi linalofanya mazu... | uchumi |
Katika mchezo huo ambao ulishuhudiwa na mashabiki wengi, Goms ilikuwa ya kwanza kupata bao mapema dakika ya tatu lililofungwa na Hamza Alaba.Lakini dakika ya saba Danis David aliisawazishia Itezi bao hilo na dakika ya 20 wakaongeza bao la pili lililofungwa na Salum Upuu na kufanya kipindi cha kwanza kumalizika kwa 2-1... | michezo |
['Nchini Uingereza mwezi Agosti ni wakati wa mapumziko na familia hutumia muda huo kujumuika pamoja baada ya shule kufungwa. ', 'Lakini kwa wachezaji wa ligi kuu ya England mambo ni tofauti, wachezaji wamerejea kazini huku kukiwa na hofu huenda wasipate kupumzika kwa karibu miezi 12.', 'Mchezaji wa Liverpool Sadio Man... | michezo |
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewasili jijini Cairo, Misri kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu ameongozana na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga na maofisa wengine wa serikali.Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, katika ziara hiyo, kiongozi huyo anatarajiwa kuwa na mazung... | kitaifa |
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameahidi kupokea kundi la watalii wasiopungua 300 wanaotarajiwa kuwasili nchini Machi, mwaka huu.Watalii hao ni kundi la kwanza miongoni mwa watalii 10,000 wanaotarajiwa kuwasili nchini mwaka huu chini ya mpango unaosimamiwa baina ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Bodi ya Utalii Tanzania (... | kitaifa |
MKUU wa Wilaya ya Longido mkoani Arusha, Frank Mwaisumbe amewataka wauza ardhi katika wilaya hiyo (madalali) wawili na kiongozi wa kijiji, kuripoti ofi sini kwake ili kuhojiwa baada ya kudaiwa kuwa wameuza ardhi mara mbili kinyume cha sheria na kuzua taharuki na mgogoro mkubwa wilayani humo.Alitoa agizo hilo baada ya ... | kitaifa |
WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Joseph Kakunda ameitaka Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) kuishauri vizuri serikali juu ya utendaji wa wakala ili azma ya kuboresha mazingira ya biashara na kufi kia uchumi wa kati unaotegemea viwanda itimie.Alisema hayo akizindua bodi hiyo Dar... | kitaifa |
JKT Queens imeendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya soka ya wanawake Tanzania Bara kwa kufikisha pointi 39 ikifuatiwa na Simba Queens yenye pointi 28.Baada ya zote kucheza michezo 13. JKT Queens bingwa mtetezi hawajapoteza mchezo wowote hadi sasa ligi ikiwa imefikisha mzunguko wa pili ikiwa imefunga ma... | michezo |
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amepokea treni ya kwanza ya mizigo kutoka Tanga ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa reli ya kutoka Tanga hadi Moshi huku akisisitiza kuwa ujenzi wa reli hiyo ni kwa kutumia fedha za ndani.Alipokea treni hiyo jana baada ya kuwasili saa 4:30 asubuhi kwenye stesheni ya Moshi na kukata utepe wa uzi... | kitaifa |
['Chelsea imetoa ofa ya kumsajili mshambuliaji wa Paris St-Germain na Uruguay Edinson Cavani, 32, kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu. (Times)', 'Babake Cavani amesema nyota huyo atajiunga na Atletico Madrid ikiwa klabu hiyo ya Uhispania itaafikiana na PSG. (Guardian)', 'Tottenham wanamlenga mshambuliaji wa Real Socied... | michezo |
WAZIRI wa Kilimo, Japhet Hasunga ametangaza neema kwa wakulima ya kununua mahindi baada ya kupatikana kwa soko kubwa kwenye nchi za kusini mwa Tanzania zinazohitaji tani milioni moja.Kutokana na hali hiyo, Wiki hii Wakala wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) na taasisi ambayo imep... | kitaifa |
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema, Tanzania haina shida ya sukari kwa sababu inayozalishwa ndani ya nchi ipo na inatosha.Majaliwa ameyasema hayo jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea mabanda kwenye Maonesho ya Nne ya Viwanda ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrik... | uchumi |
MKUU wa mkoa wa Dar es Salama ametangaza kuwa wasanii na wanamichezo watajengewa ukumbi mkubwa wa kisasa wa burudani na bwawa la kuogelea utakaogharimu Euro milioni 200 ambayo ni zaidi ya shilingi bilioni 500.RC Makonda amesema ukumbi huo utajengwa kwa ufadhili wa Kampuni ya Kifaransa, ambapo zinahitajika hekta 15 wak... | kitaifa |
KOCHA wa timu ya Yanga, Charles Mkwasa amesema ushindi walioupata kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Tanzania Prisons umewapa nguvu ya kujipanga kuikabili Biashara United katika mchezo utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.Mkwasa alitoa kauli hiyo juzi baada ya kikosi chake kuibuka na u... | michezo |
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe amesema serikali itaanzisha Wakala wa Viwanja vya Ndege nchini, ili kusimamia shughuli za viwanja zikiwemo za kudhibiti viwango vya mafuta ya ndege.Waziri Kamwelwe alisema hayo jijini hapa wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Baraza la Wafanyakazi (Mamlaka za Viwan... | kitaifa |
SHIRIKA la Makumbusho ya Taifa linatarajia kuanzisha mazungumzo rasmi ya jinsi gani Tanzania inaweza kunufaika na mikusanyo ya mjusi wa kale, aliyehifadhiwa katika makumbusho ya Berlin nchini Ujerumani.Kaimu Mkurugenzi wa Makumbusho, Mawazo Jamvi amesema hayo jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa mazungumzo hayo, yata... | kitaifa |
.Rais John Magufuli amesema bado kuna ukosefu wa maadili kwa baadhi ya watumishi wa idara ya mahakama nchini, hali ambayo haimfurahishi.Akihutubia jijini Dar es salaam katika kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria nchini, Rais Magufuli amesema kuwa ukosefu huo wa maadili miongoni mwa watumishi wa idara ya mahakama ... | kitaifa |
KATIKA toleo lililopita, kulikuwa na makala yaliyoelezea namna sekta ya kilimo inavyochochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Kupitia makala hayo, pamoja na masuala mengine yalieleza namna utekelezaji wa Sheria ya Utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji wa Mifugo Na. 12 ya Mwaka 2010 na Kanuni zake za Mwaka 2011 ulivyosaidi... | kitaifa |
BUNGE limeishauri serikali kuhakikisha fedha zote zinazoingia nchini kutekeleza miradi ya Ukimwi, zikaguliwe na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), licha ya fedha hizo kutoingia kwenye mfumo mkuu wa serikali.Akisoma taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi katika kipindi cha Januari ... | kitaifa |
WATANI wa jadi Simba na Yanga, kila mmoja anatafuta namna ya ‘kuchomoka’ kwenye mechi yao ya Ligi Kuu mwishoni mwa wiki hii kwa kila mmoja akipanga mbinu zake.Miamba hiyo inatarajiwa kumenyana Jumapili ya wiki hii kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam katika mechi yao ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu. Kocha Mkuu wa Si... | michezo |
WALIOKUWA wafanyakazi wa muda kwenye sekta mbalimbali zikiwamo za madini, ujenzi wa barabara, madaraja na nyinginezo wameanza kuwasilisha uthibitisho wao kwa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa ajili ya malipo ya mafao yao.Wafanyakazi hao ni miongoni mwa walioandamana hivi karibuni hadi ofisi za NSSF Ilala... | kitaifa |
WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Rais, Tawala na Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Dodoma na kamati ya ujenzi wa Hospitali ya Uhuru, kuhakikisha ujenzi unaanza wiki ijayo na kukamilika ndani ya miezi sita ijayo.Aidha, ametaka hospitali hiyo ijengwe na moja ya majeshi na kutaka utumike mch... | kitaifa |
KWA kauli moja Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imepokea maombi na kukubali kusamehewa adhabu ya kufukuzwa uanachama kutoka kwa waliokuwa wana CCM wanne, waliotenda makosa mbalimbali wakiwa wenyeviti wa chama hicho ngazi ya mikoa na wilaya.Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Bashir... | kitaifa |
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mbeya Mjini kimepata wanachama wapya 280, wakiwamo 30 waliohamia wakitokea vyama vingine vya siasa.Wanachama hao ambao walikuwa na nyadhifa mbalimbali ni pamoja na aliyekuwa mgombea Ubunge 2015 kupitia Chausta, Martha Komba. Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, Jacob Mwakasole aliongoza mapokezi ... | kitaifa |
ILE siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa ngumi hapa nchini hatimaye leo imefi ka, ambapo kutakuwa na pambano la ngumi la kukata na shoka litakalowakutanisha bondia wa ngumi za kulipwa wa Tanzania, Hassan Mwakinyo dhidi ya Arnel Tinampay wa Ufi lipino.Pambano hilo la uzani wa Super Walter lisilo la ubing... | michezo |
RIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2015/16, ilifichua udhaifu katika mradi wa bomba la usafirishaji gesi asilia kati ya Mtwara na Dar es Salaam, ilipobainisha kiwango kidogo cha matumizi ya gesi hiyo nchini.Katika ripoti yake hiyo, CAG alieleza kuwa bomba hilo lililojengwa na Kampu... | uchumi |
WADAU wa Muswada wa Sheria wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafi ri wa Ardhini (LATRA), wameshauri Jeshi la Polisi lisihusike na kukagua magari badala yake jukumu hilo liachiwe mikononi mwa mamlaka hiyo mpya ambayo ndiyo yenye mamlaka ya kutoa leseni za usafi ri na usafi rishaji.Akizungumza na gazeti hili jijini hapa jana, ... | kitaifa |
Promosheni ya Airtel Mkwanjika imekuwa ni promosheni ya kipekee inayowapatia wateja wanne wa Airtel kila siku kuchaguliwa kupitia droo inayoendeshwa chini ya usimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nafasi ya kuingia kwenye kisanduku kinachopeperusha pesa na kupewa dakika moja ya kujikusanyia pesa kisha kuondoka na... | uchumi |
WANAFUNZI wawili wa kitanzania wanatarajia kupeperusha bendera ya nchi katika mashindano ya kimataifa ya uimbaji kwa lugha ya Kichina yatakayofanyika Machi mwaka huu, jijini Beijing, China.Wanafunzi hao wanaiwakilisha nchi baada ya kuibuka vinara wa mashindano yaliyofanyika hapa ambayo yaliandaliwa na Chuo Kikuu cha D... | kitaifa |
WAKATI kikosi cha timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, kikiendelea kujifua vilivyo nchini Misri baada ya kupata mechi mbili za majaribio dhidi ya wenyeji Misri na Zimbabwe kabla ya kuingia rasmi kwenye fainali hizo ambazo wanatarajia kushiriki kwa mara ya pili tangu walipofanya hivyo miaka 39 iliyopita.Taifa Stars i... | michezo |
WIZARA ya Viwanda na Biashara imesema kati ya mwaka 2017 na 2018 Tanzania imeendelea kuwa na urari chanya katika mauzo ya bidhaa zake katika nchi za Afrika. Hayo yamo katika bajeti ya Wizara ya Viwanda na Biashara iliyosomwa bungeni jana na Waziri Joseph Kakunda wa wizara hiyo. Waziri Kakunda alisema Tanzania imeuza z... | kitaifa |
MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta amesema wanajipanga kuja na mikakati mitatu kuhakikisha wanasuka kikosi cha KMC kukifanya kiwe na ushindani kuelekea kwenye michuano ya kimataifa msimu huu.KMC wamepata nafasi ya kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika pamoja na Azam... | michezo |
WAKATI Serikali ya Kenya imelaani matamshi ya kibaguzi dhidi ya wafanyabiashara wa kigeni yaliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Starehe nchini humo, Charles Njagua maarufu kwa jina la Jaguar, mbunge huyo amekamatwa.Taarifa kutoka nchini humo zinasema kuwa mbunge huyo alikamatwa na vyombo vya dola kwa amri ya Mkurugenzi w... | kitaifa |
Taarifa kutoka Yanga zinasema kocha huyo aliondoka jana Dar es Salaam kwenda Morogoro, ambako timu hiyo imeweka kambi kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Simba.Zahera alikuwa kwenye benchi la ufundi la timu ya taifa ya Congo, The Leopard na amewahi kufundisha soka nchini Ufaransa.Ujio wa Zah... | michezo |
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara, Simba wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa CCM, Kirumba Mwanza.Mabao ya Simba yalifungwa na Haruna Niyonzima na Emmanuel Okwi.Ushindi huo unawafanya wekundu hao kufikisha pointi 63 ikiikaribia Azam FC inayoshika nafasi ya pili kwa... | michezo |
WATU wanne wamekufa baada ya magari mawili waliokuwa wakisafi ria kugongana katika eneo la Ubena, Zomozi lililopo upande wa Wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani.Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Francis Semwene alithibitisha kupokelewa kwa miili ya watu watatu ikiwemo ya mwanamke mmoja majira ya saa tano asubuhi j... | kitaifa |
Rais Kikwete alisema kuwa kiwango hicho kinaufanya uwekezaji wa China katika Tanzania kushika nafasi ya tano kwa thamani ya fedha, na kuwa uwekezaji huo utaiwezesha Tanzania kupata ajira 77,335 baada ya kukamilika kwa miradi yote kukamilika ambayo ujenzi wake unaendelea.Aidha, Rais Kikwete alisema uzuri wa uwekezaji h... | uchumi |
RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jakaya Kikwete amewataka wahitimu wa shahada za ualimu kujiandaa kisaikolojia kufundisha shule za msingi badala ya shule za sekondari kama yalivyo matarajio yao.Ameyasema hayo kwenye mahafali ya 10 ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Chuo Kikuu cha Dar es S... | kitaifa |
['Timu ya kandanda ya taifa Stars kutoka tanzania imeiondoa timu ya harambee Stars kutoka kenya katika mashindano ya CHAN 2020', 'Timu ya Kenya Harambee Stars ilidondoka katika michuano ya kufuzu kombe la CHAN 2020 baada ya kupoteza kwa Tanzania taifa Stars 4-1 kupitia mikwaju ya penalti katika uwanja wa Kasarani jijin... | michezo |
BENKI ya Dunia imeisifu Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli katika kupunguza umasikini na kujenga miundombinu imara ya kukuza uchumi wa Taifa. Mwakilishi wa Benki ya Dunia, Denis Biseko alitoa pongezi hizo jana, jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Matokeo ya Viashiria muhimu vya utafiti wa ... | kitaifa |
SERIKALI imewaagiza wadau wa ngumi za kulipwa nchini, kuheshimu Kamisheni Mpya ya Kusimamia Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) ili kuweza mchezo huo kupata maendeleo makubwa na kuwanufaisha mabondia.Mwito huo ulitolewa jana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe wakati wa mjadala wa mwi... | michezo |
NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angelina Mabula ametoa mwezi mmoja kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga kuhakikisha viwanja 150 vinaingizwa katika mfumo wa malipo ya kodi ya ardhi kwa njia ya kielektroniki.Dk Angelina ametoa agizo hilo alipofanya ziara katika Halmashauri ya Mkinga iliyoko mkoan... | kitaifa |
NAIBU Waziri wa Madini, Dotto Biteko amemwagiza Ofi sa Madini Mkazi wa Kanda ya Mirerani kuhakikisha anaufungua Mgodi wa Gem and Rock Venture na kuanza kufanya kazi mara moja, lakini kwa kufuata masharti ya leseni, kanuni, mipaka na sheria za uchimbaji na sio vinginevyo.Biteko alitoa agizo hilo juzi katika mji mdogo w... | kitaifa |
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kesho anatarajiwa kuzindua Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Pwani.Mkuu wa mkoa huo, mhandisi Evarist Ndikilo amesema mjini Kibaha kuwa, Waziri Mkuu atazindua mwongozo huo kwenye kongamano la uwekezaji mkoa wa Pwani.Kongamano hilo litafanyika sambamba na maonesho ya pili ya viwanda Mkoa wa Pwan... | uchumi |
Hyness ambaye ni mkulima na mama wa mtoto mmoja, alisema jana kuwa aliarifiwa juu ya ushindi wake akiwa shambani. Alisema anaamini Mungu amemuona na kwa ushindi huo, atabadilisha maisha yake kwa kiasi kikubwa.“Kwa muda mrefu nimekuwa nikihangaika na kazi za kilimo na kukumbana na changamoto nyingi kama vile ukosefu wa... | uchumi |
BARAZA la Mawaziri nchini hapa limetangaza kuongeza mishahara kwa walimu wa shule za msingi na sekondari kwa asilimia 10 katika shule za serikali na binafsi kuanzia Machi mwaka huu.Hatua hiyo imefikiwa na kikao cha mawaziri kilichoongozwa na rais wa nchi hiyo, Paul Kagame. Walimu nchini humo wamefurahishwa na ongezeko... | kitaifa |
MAMLAKA ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), imesema mchakato wa kubadilisha sheria ya uendeshaji mifuko ya hifadhi ya jamii, uliwashirikisha wadau wote muhimu, kabla ya kupitishwa na kuanza utekelezaji wake.Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumsihi wa Umma ya Mwaka 2018, ambayo ilisai... | kitaifa |
UONG OZ I wa Y anga umemshitaki mchezaji wa Si mba, James Kotei kwa Sh irikisho la So ka Tanzania (TFF) ikitaka achukuliwe hatua kwa utovu wa nidhamu.Kotei alimpiga ngumi beki wa Y anga, G adiel Michael wakati timu zao zilipokutana kwenye mechi ya L igi Kuu B ara mwishoni mwa wiki iliyopita. Marudio ya picha za video ... | michezo |
Subsets and Splits
No community queries yet
The top public SQL queries from the community will appear here once available.