content
stringlengths
1k
24.2k
category
stringclasses
6 values
WACHIMBAJI wadogo wa dhahabu katika mgodi mpya wa Ndurutu, Kijiji cha Kilama Kata ya Iyogwe wilayani Gairo, mkoa wa Morogoro wamepata neema kwani hadi Juni 30, mwaka huu.Jumla ya gramu 255. 23 za dhahabu zilinunuliwa katika soko la madini la Morogoro mjini na kupatikana jumla ya Sh milioni 25.3 na Serikali ikiwa imeku...
uchumi
LIGI Kuu ya wanawake Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea leo kwa michezo minne katika viwanja vinne tofauti.Vinara wa ligi hiyo Alliance Girls yenye pointi 13 wataikaribisha Baobab ya Dodoma yenye pointi moja katika mchezo utakaochezwa Uwanja wa Nyamagana, Mwanza. Panama Queens yenye pointi tatu itacheza na bingwa mte...
michezo
MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma wa PSSSF, umeanza kufanya uhakiki wa wastaafu na wategemezi wa mfuko huo kuanzia sasa hadi mwezi Machi, mwaka huu Tanzania Bara na Visiwani.Ili kuweza kufanikisha kazi hiyo, uongozi wa mfuko huo umetaja vigezo vitakavyotumika ili kutambua uhalali wa wastaafu hao...
kitaifa
Kahawa hiyo iliuzwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2013 hadi Aprili 30 mwaka huu. Meneja Mkuu wa Tanica, Leonidas Nshansha alisema hayo alipozungumza na mwandishi wa habari hizi.Alisema malengo ya kampuni hiyo tangu Mei Mosi mwaka jana yalikuwa ni kuzalisha tani 255 za kahawa ya unga na tani 270 za kahawa ya kukaan...
uchumi
NAIBU Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema serikali imetenga Sh bilioni 88 kulipa wakandarasi mbalimbali nchini wanaotekeleza miradi ya maji.Aliyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Rita Kabati (CCM) aliyetaka kujua serikali ina mkakati gani kuhakikisha inawalipa wakandarasi wanaoidai ambao wengi ...
kitaifa
TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Geita katika kipindi Oktoba hadi Desemba, mwaka jana, imeokoa zaidi ya Sh milioni 16 za taasisi mbalimbali ikiwamo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)ambazo zingehujumiwa.Taasisi hiyo imepokea malalamiko ya rushwa 48 kutoka kwa wananchi ambapo malalamiko 10 kati ...
kitaifa
['Chelsea wanavutiwa kumsajili winga wa Crystal Palace na Ivory Coast Wilfried Zaha mwezi huu lakini hawako tayari kufikia dau la pauni milioni 80 lililotajwa na klabu hiyo. (Express)', 'Manchester City wanawania kumsajili winga wa Wolves Mhispania Adama Traore, 23. (Calcio Mercato, via Manchester Evening News)', 'Wak...
michezo
Hayo yalisemwa Mke wa Mbunge wa Mkuranga, Naima Malima wakati wa kuwapokea wageni kutoka India, ambao ni Chama cha Wanawake Waliojiajiri (SEWA) waliotembelea kikundi cha Kiwalani Women Group.Naima alisema imefika wakati sasa kwa vikundi hivyo, kutafuta masoko mbalimbali yakiwemo ya Kimataifa.“Ni vema mtumie fursa za u...
uchumi
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe, ametoa miezi mitatu kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kutopeleka magari ya Serikali kwenye karakana binafsi kwani Wakala unajitosheleza kwa kuwa na wataalamu na vifaa vya kutosha.Kamwelwe, amesisitiza kwa Wakala huo kuhakikisha unatengeneza magari kwa bei...
kitaifa
VIJANA wawili wa Kitanzania, Zakaria Sheha Ally na Shamsi Mwalimu Said wamechukua nafasi ya kwanza na ya tatu kwenye fainali za 27 za tuzo ya kimataifa ya kuhifadhi Kurani tukufu.Zakaria Sheha Ally (16) kutoka Tanzania Bara na Shamsi Mwalimu Said (19) kutoka Zanzibar wameibuka na kitita cha Dola za Marekani 5,000 na d...
kitaifa
KIKOSI cha Klabu ya Yanga SC, kimeondoka jana kwa ndege kwenda mkoani Shinyanga kuwakabili Mwadui FC kesho, kwenye Uwanja wa CCM, Kambarage katika muendelezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.Timu hiyo imeondoka siku moja baada ya kuwasili kutoka mkoani Lindi, ambako ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo FC inayoshirik...
michezo
['Kuna uwezekano Manchester United ikashuka daraja msimu huu, kwa mujibu wa kocha wa zamani wa England, Sam Allardyce. (Talksport)', 'Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer atafutwa kazi endapo timu yake itafungwa na Norwich mwishoni mwa mwezi, ripoti zinaeleza. (Sun)', 'Hata hivyo, vyanzo vingine vinaarifu k...
michezo
Rais John Magufuli amewataka wanafunzi na wahadhiri wa vyuo vikuu vya Teknolojia Mbeya (MUST), Mzumbe na Saint Augustine (SAUT) kutekeleza majukumu yao kwa haki na kutumia muda ipasavyo.Akizungumza wananchi na Jumuiya ya wanataaluma wa vyuo hicho, Rais amesema wanafunzi wanapoteza muda wao mwingi kwa mambo ambayo haya...
kitaifa
Mkurugenzi Mkuu wa ATCl, Ladislaus Matindi amesema wamejipanga vizuri ili kujitanua kibiashara na kurudi katika mfumo wa kimataifa wa Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Ndege (IATA).Amesema ATCL iliondolewa katika mfumo wa kimataifa wa utoaji wa huduma na ununuzi wa tiketi kwa kukabiliwa na madeni makubwa.Kwa mujibu w...
uchumi
SERIKALI kwa sasa iko katika hatua ya kuchambua na kupitia upya muundo wa kifedha na kiuchumi, utakaotumika kwenye mikataba ya uchimbaji na utafutaji wa gesi ili kuweza kuinufaisha nchi.Aidha, serikali imebainisha kuwa imejiandaa na haina wasiwasi kwenye malipo ya Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Rufiji.Akijibu hoja wakati...
uchumi
UONGOZI wa timu ya soka ya Yanga umesema hauna mpango wa kubadilisha kikosi chake katika mchezo wao na Azam FC ambao utachezwa leo usiku kuanzia saa 2:15 wa Kombe la Mapinduzi Timu hizo zinakutana leo katika dimba la Amaan, Azam inashuka ikiwa na pointi moja baada ya mchezo wake wa kwanza kutoka sare na Jamhuri na Yan...
michezo
KAMPENI ya kuwastiri Watoto wa kike kupata nguo za ndani (chupi na sidiria), imezinduliwa jana jijini Dar es Salaam kwa lengo la kusaidia watoto 1,000 wa mkoani Lindi na Arusha hususani wilayani Karatu.Kampeni hiyo ya siku 40 inaendeshwa na mradi wa Girls in Action Initiative iliopo chini ya Kampuni ya Christom Soluti...
kitaifa
NYUMBA 336 katika vijiji vya Kipeta na Kilyamatundu Kata ya Kipenta katika Bonde la Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga, zimebomoka na zingine kuezuliwa paa na kuta baada ya mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo mkali kunyesha kwa takribani dakika 45.Aidha, mkazi wa kijiji cha Kipeta, Elizabeth Manamba (85) amepoteza m...
kitaifa
Hayo yalisemwa Mjini hapa jana na Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda wakati wa uzinduzi wa kikundi cha Vicoba cha watumishi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Makao Makuu.Alisema wananchi wanatakiwa kuchangamkia fursa kwa kujiunga kwenye vikundi vya kuweka na kukopa kwani mfumo huo umeonesha mafanikio makubwa katika mikoa m...
uchumi
BAADA ya kupoteza pointi nne kwenye michezo miwili iliyopita vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wameapa kufi a uwanjani kusaka pointi tatu muhimu kwenye mechi dhidi ya African Lyon itakayopigwa leo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.Mchezo huo wa 30 kwa Yanga ambayo inaongoza ligi hiyo kwa pointi 68 baada ya kuc...
michezo
Waziri huyo anaongoza ujumbe wa maofisa mbalimbali wa Serikali katika kukagua barabara kuu hususani mizani kutoka jijini Dar es Salaam-Tunduma hadi Mji wa Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).Barabara hiyo inatumiwa na magari ya mizigo ya wafanyabiashara wa DRC kutoka Bandari ya Dar es Salaam, hivyo kwa ...
uchumi
Promosheni ya “Airtel MKWANJIKA” itawawezesha wateja wote wanaojiunga na kifurushi chochote cha yatosha au kuongeza muda wa maongezi wa kiwango chochote kwenye simu zao kuingia kwenye droo na kupata nafasi ya kujishindia.Kila siku wateja watakaoongeza salio wataingizwa kwenye droo ya “Airtel MKWANJIKA” ambapo washindi...
uchumi
Nchemba aliyasema hayo mwishoni mwa wiki bungeni mjini hapa wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge zilizotolewa katika mjadala wa hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Tamisemi kwa mwaka wa fedha 2015/16.Akijibu hoja hizo, ambazo nyingi zilitolewa na wabunge wa vyama vya upinzani wakisema serikali haijafanya ...
uchumi
Akiwa kwenye mabaki ya iliyokuwa nyumba yao miaka takribani tisa iliyopita, bado ni mahala anapoishi na kupata usingizi wake. Lakini Salah Jaar mwenye umri wa miaka 32 sasa, hayuko peke yake.Pembeni mwake kuna nusu dazani ya paka ambao huchangia kumpa faraja kwamba bado kuna uhai wa watu na viumbe wengine katika mji h...
michezo
MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amesitisha likizo zote za watendaji wakuu wa mkoa na wilaya ili wasimamie ujenzi wa madarasa mapya kwenye shule za sekondari.Mndeme ametoa agizo hilo wakati wa kikao na viongozi na watendaji wa taasisi za umma na binafsi na kuwataja viongozi ambao hawapaswi kwenda likizo hadi vy...
kitaifa
['Real Madrid itataka kumsaini kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen mwezi Januari.(Marca)', 'Real Madrid pia wanaisaka saini ya mshambuliaji wa Red Bull Salzburg, 19 raia wa Norway Erling Haaland, ambaye amehusishwa na uhamisho wa kuelekea Manchester United. (AS)', 'Beki wa kulia wa Tottenham na Ivory Coast Se...
michezo
KUMEKUWA na ongezeko la mashauri ya migogoro ya ndoa katika kipindi cha miezi tisa kuanzia Julai, mwaka 2018 hadi Machi, mwaka huu, ambapo jumla ya mashauri 16,832 yameripotiwa ikilinganishwa na mashauri 13,282 katika kipindi cha mwaka 2017/18 ambayo ni sawa na asilimia 34.5.Mkurugenzi wa Idara ya Watoto, Idara Kuu ya...
kitaifa
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro Premium Lager imezindua shindano la uchoraji nchi nzima linalojulikana kama ‘Jiachie na Kili Canvas Competition 2020’ linalotarajiwa kufanyika Januari 22, Golden Tulip, Dar es Salaaam.Akizungumza jana Dar es Salaam, Meneja wa bia ya Kilimanjaro, Pamela Kikuli, a...
michezo
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amechaguliwa bila kupingwa kuwa Rais wa Baraza la vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) katika uchaguzi mkuu uliofanyika mjini Kampala, Uganda jana. Uchaguzi huo ulifanyika baada ya viongozi waliokuwepo kumaliza muda wao tangu mwezi uliopita.Karia ata...
michezo
MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA) kupitia Bandari ya Mtwara itakuwa na uwezo wa kuhudumia tani zaidi ya milioni moja za mizigo kwa mwaka kutoka tani 400,000 za sasa, mara ujenzi wa gati namba mbili utakapokamilika mwishoni mwa mwaka huu.Bandari hiyo ambayo imeelezwa kuwa lango kuu la biashara au uchumi kwa ...
uchumi
SERIKALI imeamua kuendesha mnada wa wazi mtandaoni katika msimu wa mauzo ya zao la korosho kwa mwaka huu ili kuwe na uwazi, usawa na kupata bei nzuri. Aidha, katika msimu wa mauzo uliopita ambao serikali ilichukua jukumu la kununua korosho zote zilizovunwa, mpaka sasa serikali imebaki ikidaiwa na wakulima Sh bilioni 5...
uchumi
Gawio hilo lilitolewa Jumamosi jijini Dar es Salaam wakati wa semina ya wahariri wa vyombo vya habari nchini, iliyoandaliwa na NSSF.Akikabidhi hundi ya fedha kwa Mkurugenzi Mtendaji wa NSSF Dk Ramadhani Dau, Kaimu Mkurugenzi wa Katani Ltd, Juma Shamte alisema katika kipindi cha Mwaka 2006/2013 , NSSF imeshatoa kiasi c...
uchumi
FAINALI za kumsaka mshindi wa Bongo Star Search 2019, zilizofanyika juzi katika ukumbi wa Next Door Arena, Dar es Salaam, Meshack Fukuta kutoka Mbeya aliibuka mshindi.Mshindi wa pili alikuwa Leonard Sunday na ushindi wa tatu ulikwenda kwa Frank Charles, wa nne, Patricia Zephania na wa tano, Patrick Alsina. Kabla ya Ja...
michezo
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Josephat Kandege ameagiza vitengo vya ukaguzi wa ndani katika ofi si za mikoa na halmashauri kuhakikisha inabainisha na kudhibiti mianya ya ubadhirifu kwenye mifumo ya kukusanyia mapato na usimamizi wa fedha.Pia amesema wizara yake imeomba kibali cha aji...
kitaifa
MSHIKEMSHIKE wa Ligi Kuu Tanzania Bara unatarajiwa kuendelea tena leo katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kwa kuwakutanisha mabingwa watetezi wa ligi hiyo Simba SC dhidi ya Mwadui FC.Simba itamalizia hasira zake kwa Mwadui baada ya kufungwa 5-0 na Al Ahly ya Misri katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika uliofan...
michezo
Wafanyabiashara hao zaidi ya 500 wakiwa wamekusanyika katika eneo la Masuka mjini hapa, kutaka kufanya maandamano kwenda kuonana na mkuu wa mkoa ofisini kwake kumuelezea kero hizo ili zipatiwe ufumbuzi, ambapo maduka mengi yalionekana kufungwa.Baadhi ya wafanyabiashara waliozungumza na waandishi wa habari, kabla ya ku...
uchumi
WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa amewataka wamiliki wa viwanda kushirikiana na serikali ili kuhakikisha soko la bidhaa mbalimbali wanazozizalisha linakuwa kubwa kwenye nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) pamoja na Jumuiya ya Afrika Mshariki (EAC).Bashungwa amesema hayo alipokutana na...
uchumi
WATU wa kada mbali mbali wameunga mkono hatua ya Rais John Magufuli ya kuwaalika watu wa kada mbalimbali kukaa nao pamoja ili kujua changamoto zinazowakabili na kuzitatua kwa pamoja.Walisema ili nchi iweze kusonga mbele, inahitajika michango ya pamoja kutoka sekta mbalimbali ya nchi, kitu ambacho Rais Magufuli amekuwa...
kitaifa
MKOA wa Ruvuma umetakiwa kuweka mazingira wezeshi ya kuwavutia wawekezaji kuchangamkia fursa za uwekezaji na kuufanya mkoa huo kuwa moja ya maeneo yenye viwanda vingi nchini.Akiwasilisha mada wakati wa uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji mkoani humo mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwek...
uchumi
NAHODHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na mshambuliaji wa klabu ya Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta, amefurahishwa na mbinu za Kaimu Kocha Mkuu wa timu hiyo, Etienne Ndayiragije na kueleza zinawasaidia kuwa na ari ya kupambana uwanjani na kuahidi kufanya makubwa chini yake.Samatta aliyasema hayo alipokuwa k...
michezo
KAULI ya Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mwanaasha Tumbo kuwa Idara ya Ardhi katika Halmashauri ya Wilaya hiyo haina mtendaji wa sekta ya ardhi anayeweza kuvaa viatu vya ukuu wa idara iwapo anayeshikilia nafasi hiyo, Salehe Kang’e ataondolewa, imemwokoa mkuu huyo wa idara kutumbuliwa.Kauli hiyo ilikuja baada ya Naibu Waziri...
kitaifa
Hayo yalibainishwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa CMSA, Nasanda Massama, wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa kampuni ya Soko la Bidhaa (TMX), iliyozinduliwa na Rais Jakaya Kikwete Dar es Salaam, hivi karibuni.Alisema kwa upande wa kampuni za ndani masoko hayo ya mitaji mchango wake umeongezeka kutoka asilimia sita, mwaka...
uchumi
KAMATI ya Bunge ya Kudumu ya Viwanda, Biashara na Mazingira imeipongeza Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC Plc) kwa kuwa mstari wa mbele katika utekelezaji wa malengo ya ubinafsishaji na kuendeleza azma ya serikali ya viwanda.Pongezi hizo zimetolewa wakati wa ziara ya kamati hiyo iliyoratibiwa na Shirikisho la Viwanda Ta...
uchumi
BONDIA machachari nchini, Hassan Mwakinyo ameiomba Serikali isapoti mchezo wa ngumi ili utumike katika kulitangaza taifa nje ya mipaka yake.Mwakinyo ambaye ni balozi wa Kampuni ya Sportpesa ameyasema hayo mapema leo jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya mwelekeo wa ngumi za ku...
michezo
Kwa mara ya kwanza Tanzania itakuwa na kiwanda cha kuchenjua na kusafisha dhahabu kinachotarajiwa kuanza kazi Oktoba mwaka huu.Hayo yameelezwa jijini Dodoma na Waziri wa Madini, Doto Biteko baada ya kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda kitakachochenjua na kusafisha dhahabu kwa asilimia 99.9.Amesema ...
uchumi
MABONDIA Francis Cheka na Abdallah Pazi ‘Dullah Mbabe’ kila mmoja amejigamba kuonesha ubabe wake katika pambano litakalofanyika keshokutwa katika ukumbi wa Sabasaba PTA, Dar es Salaam. Dullah Mbabe mwenye umri wa miaka 24, amecheza michezo 28 mpaka sasa, kashinda mapambano 22 ambapo 21 kati ya hayo ameshinda kwa KO, a...
michezo
BUNGE limeridhia kubadilisha hadhi mapori ya akiba ya Biharamulo, Burigi, Kimisi, Ibanda na Rumanyika-Orugundu katika ukanda wa Kaskazini- Magharibi kuwa Hifadhi za Taifa ambako kutasaidia kuimarisha ulinzi, kujenga mazingira bora na kukuza Pato la Taifa.Pia serikali ipo katika kampeni ya kuchora upya ramani na vivuti...
kitaifa
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko wataendelea kusota gerezani hadi Januari 3, mwakani kesi yao ya uchochezi inayowakabili na wenzao saba, itakapotajwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.Sababu ya washitakiwa hao kusota rumande ni kutoka...
kitaifa
Simba juzi iliingia mkataba wa miaka miwili na Okwi, ambaye ataanza kuichezea tena timu hiyo msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, utakapoanza Agosti mwaka huu.Akizungumza na gazeti hili, Kaburu alisema baada ya kuinasa saini ya Okwi, sasa usajili wao umekamilika kwa asilimia 90 na wamebakiza asilimia 10, ili kufun...
michezo
WADAU wa kilimo cha alizeti mkoani Dodoma, wameiomba serikali kuandaa mafunzo maalumu kwa maofi sa ugani, hatua itakayowaongezea uwezo wataalamu hao katika kutoa elimu stahiki kwa wakulima wa zao hilo.Ombi hilo lilitolewa na wadau hao wakati wa kikao cha wajumbe wa Bodi ya Taasisi ya Kuendeleza Mifumo ya Masoko ya Kil...
kitaifa
KIPA Juma Kaseja amesema juhudi zake ndizo zilizomfanya aitwe kwenye kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars. Kaseja alikuwa kipa namba moja ‘Tanzania one’ kwa muda mrefu kabla ya kuachwa kujumuishwa kwenye kikosi cha Stars miaka sita iliyopita.Mwishoni mwa wiki iliyopita, kocha wa muda wa Taifa Stars, Etiene Ndayiragij...
michezo
MWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG), Profesa Adelardus Kilangi amesema hawezi kufungua shauri lolote mahakamani la kuomba ufafanuzi wa kikatiba kuhusu mgogoro uliopo kati ya Bunge na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad uliodumu kwa takribani miezi minne sasa.Baadhi ya wananchi walio...
kitaifa
['Barcelona ingelimsaini mshambuliaji wa Tottenham Lucas Moura, 27, msimu huu lakini ilishindwa kufikia bei yake ya £45m. (Mundo Deportivo)', 'Juventus itawauza mshambuliaji Mario Mandzukic, 33, na kiungo wa kati Emre Can, 25, dirisha la uhamisho wa wachezaji litakapofunguliwa mwezi Januari. (Goal)', 'Atletico Madrid b...
michezo
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wassira alisema hayo katika hotuba yake iliyosomwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Sophia Kaduma, wakati akifungua warsha ya wadau wa kilimo, kujadili mpango mkakati wa Tadb, Dar es Salaam jana.Kwa mujibu wa Wassira, benki hiyo itaweza kutoa mikopo ya bei nafuu endapo itas...
uchumi
WAZIRI wa Madini, Dotto Biteko ameitaka kampuni inayochimba madini ya urani katika mto Mkuju wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma, Uranium One kutosita kuwasiliana naye pindi wanapokutana na changamoto katika utekelezaji wa mradi wao.Aliyasema hayo katika kikao chake na watendaji wa kampuni hiyo kilichofanyika ofisini kwak...
uchumi
KAMPUNI ya Magazeti ya Serikali (TSN) inayochapisha magazeti ya HabariLeo, Daily News na SpotiLeo, imetoa washindi watano katika Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2018, zinazotolewa kila mwaka na Baraza la Habari nchini (MCT).Tuzo hizo ambazo zinafanyika kwa mara ya 10, zimekuwa zikishirikisha waan...
kitaifa
MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya Mendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Japhet Justine ametoa mwito kwa vyama vya ushirika katika zao la korosho, kuwekeza kwenye viwanda vya kubangua korosho ili kuongeza thamani na kupata bei nzuri sokoni.Ametoa mwito huo alipofanya ziara ya Operesheni ya Korosho wilayani Tunduru mkoani R...
kitaifa
HUKU takwimu zikionesha kuongezeka kwa ukatili wa watoto hapa nchini, Mbunge Salma Kikwete ameshauri kuwepo kwa kampeni kwa lengo la kuepusha vitendo hivyo vinavyoathiri kundi hilo kimwili, kiakili na kihisia. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kwa kushirikiana na Jeshi la ...
kitaifa
MAOFISA Madini nchini wametakiwa kutobagua migodi midogo kwa kuelekeza nguvu kwenye migodi mikubwa tu huku wakisisitizwa kutatua migogoro kwenye maeneo yao ya kazi na kuelezwa kuwa, watakaobainika wakibagua migodi hiyo na kutotatua migogoro wataondolewa kwenye nafasi zao.Hayo yalibainishwa na Naibu Waziri wa Madini, S...
kitaifa
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Johnson Mfinanga wakati aliitaja baadhi ya mikakati iliyoundwa juu ya msingi wa serikali ya awamu ya nne katika kuboresha zaidi huduma za kampuni hiyo.“Ni katika kipindi hiki cha awamu ya nne chini ya Rais Kikwete ndio tuliweza kuanzisha safari zetu za kwenda ...
uchumi
MESUT Ozil ni mchezaji muhimu sana kwenye kikosi cha Arsenal na hakuna wa kumlinganisha naye kwa wachezaji wanaocheza nafasi yake kwenye kikosi cha washika bunduki hao.Bado anaonekana kutoendana sana na mfumo wa kocha Unai Emery, lakini hakuna namna zaidi ya kocha huyo wa zamani kujitahidi kupata kile ambacho Ozil ana...
michezo
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Meneja Mawasiliano wa kampuni hiyo, Emma Oriyo alisema programu hiyo ya mafunzo ni ya miaka minne mfululizo na awamu ya kwanza inaanza mwezi huu na kukamilika Machi 3 mwaka ujao.Emma alisema programu imelenga kuwanufaisha wauzaji wadogo wa bidhaa zao nchi nzima ambapo awamu ya kwanz...
uchumi
WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema gharama za matibabu nchini hazijabadilika badala yake, zimezidi kupungua ili wananchi wamudu na kupata hduuma bora za afya.Kwa mujibu wa taarifa ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Idara Kuu ya Afya, kumekuwapo na taarifa za upotoshaji umma juu ya ...
kitaifa
['Klabu ya Arsenal imefanya mazungumzo na meneja wa zamani wa Uhispania na Barcelona, Luis Enrique kuhusu mpango kuchukua nafasi ya Unai Emery. (El Confidencial, kupitia Metro)', 'Klabu ya Tottenham wapo tayari kutoa ofa ya pauni 50m kwa Memphis Depay mshambuliaji wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 25, ambaye alihamia Kl...
michezo
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kuanzia Julai Mosi mwaka huu Serikali itaanza kutekeleza utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kuboresha Mfumo wa Udhibiti wa Biashara nchini (Blue print) kwa lengo la kurahisisha mazingira ya kufanya biashara.Alisema hayo jana wakati akiahirisha mkutano wa 15 wa Bunge, jijini Dodoma na kuo...
kitaifa
BAADA ya kusimama kwa siku kadhaa kupisha mechi za kimataifa, Ligi Kuu Tanzania Bara inarejea tena mwishoni mwa wiki hii huku kila timu ikiwa na moto wa kutaka kushinda. Ligi ilisimama kuipisha timu ya taifa, Taifa Stars iliyocheza na Uganda mechi ya kuwania kufuzu fainali za kombe la Mataifa Afrika, Afcon 2019, mechi...
michezo
MWIGIZAJI maarufu nchini Wema Sepetu ameachiwa huru kuendelea na shughuli zake za filamu baada ya Bodi ya Filamu kujiridhisha kuwa ametekeleza adhabu waliyompa kwa asilimia 75.Wema alifungiwa tangu Oktoba mwaka jana kujihusisha na filamu kwa muda usiojulikana, baada ya kusambaa kwa picha yake kwenye mitandao ya kijami...
michezo
MKURUGENZI wa Mashitaka (DDP), Biswago Mganga amesema serikali imetaifisha rasmi mali za Wakili maarufu jijini Arusha, Median Mwale zenye thamani ya Sh bilioni 1.2 kutokana na makosa ya kutakatisha fedha haramu.Mganga amesema, mali hizo zilizotokana na zao la utakatishaji fedha haramu baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Ar...
kitaifa
HOSPITALI ya Benjamin Mkapa (BMH) ya jijini Dodoma leo inazindua kitengo kitakachotibu magonjwa yanayohusiana na mfumo wa njia ya mkojo na pia kitashughulikia upasuaji wa tezi dume.Katika taarifa iliyotolewa na Kitendo cha Mawasiliano na Uhusiano katika Hospitali ya Benjamini Mkapa inaonesha kwamba kitengo hicho kitak...
kitaifa
KAMISHNA Jenerali wa Idara ya Uhamiaji, Anna Makakala amepewa salamu za heshima kutoka kwa mataifa mbalimbali kwa kuindoa Tanzania kuwa uchochoro wa vitendo vya rushwa na kupitisha dawa za kulevya kwenda Ulaya.Nchi zilizotoa pongeza na kumpa heshima kwa kutambua mchango wa Kamishna Makakala ni China, Marekani, India, ...
kitaifa
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo ametoa siku 68 kwa halmashauri nne kurejesha fedha za Mradi wa Elimu (Equip) zilizotumika kinyume cha utaratibu.Pia ameagiza ndani ya siku saba Mweka Hazina wa Manispaa ya Iringa, Saad Ishabairo kuchunguzwa na ikibidi ashushwe cheo mara...
kitaifa
Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya benki hiyo mjini Morogoro jana, Herman Kessy kwenye mkutano mkuu wa kwanza wa wanahisa wa benki hiyo.Aidha, aliwaambia wajumbe wa mkutano huo kuwa, benki hiyo pia itaanzisha uwakala wa benki ambayo itashirikiana na mawakala wa sehemu mbalimbali na ili kuhakikisha ...
uchumi
FOMU za kushiriki mbio za Ngorongoro Race 2019, ambazo zinatarajia kufanyika Aprili 20 zitaanza kutolewa Ijumaa mjini Karatu, imeelezwa.Mratibu wa mbio hizo, Meta Petro alisema juzi tayari baadhi ya wanariadha nyota wamethibitisha kushiriki mbio hizo za kilometa 21, akiwemo Alphonce Simbu ambaye hivi karibuni alifikia...
michezo
WATU sita wanaosadikiwa kuwa majambazi, wakiwemo raia wa Burundi, wameuawa katika majibizano ya risasi na kikosi kazi maalumu cha kupambana na ujambazi katika maeneo ya Ubungo UFI, Dar es Salaam.Watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na silaha tatu aina ya AK 47, risasi 217, magazini nane, mabomu manane ya kutupa kwa mkono...
kitaifa
Pongezi hizo zilitolewa na Mkuu wa Mkoa huo, Joel Bendera, katika hotuba yake kwenye sherehe ya TCCIA kutimiza miaka 25 iliyofanyika hivi karibuni mjini hapa.Mbali na kutoa pongezi hizo alitumia fursa hiyo kuipongeza kwa kuwezesha kumaliza tatizo la mashine za kielectroniki (EFDs), ambao ni mfumo mpya wa kutoa risiti....
uchumi
KOCHA mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema, kilichowafanya wapoteze mchezo wao mbele ya Lipuli FC ni wapinzani wao hao kuwazidi uwezo hivyo mbinu zao zote walizozitumia hazikufanya kazi.Yanga walifungwa mabao 2-0 na Lipuli katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam, FA, uliopigwa katika Uwanja wa Sam...
michezo
WAPINZANI wa Simba kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, TP Mazembe wanatarajiwa kuwasili leo mchana tayari kwa mchezo wa hatua ya robo fainali unaotarajiwa kupigwa mwishoni mwa wiki hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Kuelekea kwenye mchezo huo, Ofisa Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara alisema kikosi cha timu yao kipo kw...
michezo
KOCHA Emmanuel Amunike ameita kikosi cha Taifa Stars kwa ajili ya mchezo wa mwisho dhidi ya timu ya taifa ya Uganda, The Cranes na hakumjumuisha hata mchezaji mmoja wa Mtibwa Sugar.Mchezo huo wa kundi L utapigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Machi 24 ni muhimu kwa Taifa Stars kufuzu kwa fainali za Mataifa ya A...
michezo
JUKWAA la Fursa za Biashara na Uwekezaji mkoani Tabora linamalizika leo baada ya kufanyika kwa siku tatu mfululizo. Limekuwa ni jukwaa la kwanza kati ya saba yaliyokwishafanyika, kuhudhuriwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na mawaziri wengine watatu kwa mpigo.Ni jukwaa ambalo pia lilitia fora kwa kuhudhuriwa na...
kitaifa
KOCHA wa Azam FC Ettiene Ndayiragije amesema mchezo wa leo wa fainali Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati Kombe la Kagame ni wa kisasi.Akizungumzia mchezo huo jana kupitia sauti iliyotumwa na Msemaji wa klabu hiyo Jaffar Maganga, Ndayiragije alisema kwa kuwa mchezo wa kwanza wa makundi walipoteza 1-0 dhidi ya KCCA, ...
michezo
KIKOSI cha mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba jana kilifi ka salama mjini Rustenburg, Afrika Kusini kwa ajili ya kambi ya wiki mbili.Msafara wa wachezaji 22 na viongozi wa benchi la ufundi la timu hiyo uliondoka jana asubuhi na ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania. Simba ipo kwenye maandalizi ya kuanza msimu mpya ...
kitaifa
['Mwaka 1969, mataifa ya El Salvador na Honduras yalipigana kwa siku nne na kuacha maelfu wakipoteza maisha na maelfu wengine wakipoteza makazi- umwagaji huo wa damu baado unakumbukwa kama Vita vya Mpira wa Miguu. ', 'Matokeo yalikuwa 2-2 baada ya dakika 90 katika uga wa Azteca jijini Mexico City. Huu ulikuwa ni mchez...
michezo
Mkurugenzi Mkuu wa Fastjet nchini, Nico Bezuidenhout amesema mwishoni mwa wiki kuwa, makubaliano hayo yatakuza biashara ya Fastjet kwa kutanua wigo wa kuuza tiketi duniani.Amesema wateja wataweza kufanya maandalizi ya safari, kununua tiketi na kuona mfumo wa safari za Fastjet kirahisi na kutumia huduma zao."Kwa kuwa h...
uchumi
MAOFISA Tarafa nchini wametakiwa kusimamia kwa karibu miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao ya kazi vinginevyo, atakayeshindwa kufanya hivyo atadhihirisha kuwa hamudu kazi hiyo. Rais John Magufuli amewataka viongozi hao kutambua mipaka ya kazi yao huku akiasa Maofisa Tarafa kugeuzwa wasaidizi wa Makatib...
kitaifa
KUTOKANA na kusambaa kwa taarifa kwa njia ya video fupi kwenye mitandao ya kijamii, ikieleza uwepo wa viashiria vya vitendo vya ugaidi nchini, serikali imewatoa hofu wananchi na kuwataka kuipuuza taarifa hiyo.Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali,...
kitaifa
Rais John Magufuli amesema, Tanzania na Afrika Kusini zinaongoza kwa kufanya biashara ndani ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).Amesema jijini Dar es Salaam kuwa, mwaka jana biashara baina ya nchi hizo ilikuwa na thamani ya Dola za Marekani bilioni 1.18 kutoka Dola za Marekani bilioni 1.11 mwaka 2017.Amey...
uchumi
WATU 18 akiwemo mkuu wa shule ya Shule ya Sekondari Tumaini Lutheran Seminary iliyopo wilayani Malinyi, Mkoa wa Morogoro, baadhi ya walimu, wasimamizi wa mitihani na baadhi ya wanafunzi wamefi kishwa katika mahakama ya Wilaya ya Ulanga wakikabiliwa na makosa yanayohusu udanganyifu wa mitihani ya kidato cha nne.Kamanda...
kitaifa
WANANCHI wa Kenya wanatumia fedha nyingi katika kugharamia sherehe za harusi nchini humo. Kwa mwaka jana pekee, inakadiriwa zimetumika zaidi ya Shilingi za Kenya bilioni 15, sawa na Shilingi za Tanzania bilioni 300.Hayo ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa jijini humu na Kampuni ya Samantha Bridal, inayojihusisha na sh...
kitaifa
MWALIMU wa Shule ya Msingi Forest katika Manispaa ya Morogoro mkoani Morogoro, Pendo Manyama (29) na wanawe wawili wamekufa baada ya mtungi wa gesi iliyokuwa imevuja, kujaa ndani ya chumba na kulipuka.Moto huo ulilipuka mama huyo alipoingia ndani na jiko la mkaa. Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Wilbroad Mutafungwa alisema ...
kitaifa
UBALOZI wa Thailand nchini umeanza mikakati ya kutenga maeneo mbalimbali kwa ajili ya kilimo cha mpunga na kujenga viwanda kwa ajili ya kuchakata zao hilo.Huu ni uzalishaji wa kisasa ambao utashuhudia Uganda ikizalisha mpunga maradufu kutokana na uwepo wa ardhi yenye kufaa kwa kilimo hicho. Akizungumza katika siku ya ...
kitaifa
YANGA inatarajiwa kuwa ugenini Nairobi kesho kumenyana na Gor Mahia ya Kenya katika mechi ya makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika. Tayari wawakilishi hao wa Tanzania wameshawasili Nairobi kwa ajili ya mechi hiyo, wakitamba kufanya vizuri licha ya kuacha nyota wake kadhaa wanaodaiwa kugoma kutokana na kuto...
michezo
NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye ameliagiza Baraza la Wafanyakazi wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), kuimarisha kitengo cha biashara na kufanya uchunguzi wa hujuma mbalimbali dhidi ya kampuni hiyo.Akifungua kikao cha tatu cha Baraza la Wafanyakazi la ATCL, Nditiye alisema hivi karib...
kitaifa
MTOTO anayesumbuliwa na kitovu chenye ukubwa usio wa kawaida, ameruhusiwa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa amelazwa baada ya wataalamu kumchunguza na kuelekeza utunzaji wake ikisubiriwa umri sahihi wa kuweza kumfanyia upasuaji.Habib Kassim mwenye umri wa miezi minane kutoka Nzega mkoani Tabora aliku...
kitaifa
RAIS wa Shirikisho la Soka la Afrika (Caf), Ahmad Ahmad amekamatwa jana asubuhi jijini Paris, Ufaransa akituhumiwa kwa rushwa, kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo mbalimbali.Gazeti la kila wiki la Afrika la Jeune Afrique lilidai kuwa rais huyo wa Caf alikuwa akiishi jijini Paris katika hoteli moja wakati akihudhuria M...
michezo
[' Siku ya Jumanne mashabiki wa mojawapo wa timu kongwe Tanzania watakusanyika katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam kusherehekea "Simba Day".', 'Ni katika kuidhinisha wiki ya Simba au kwa umaarufu "Simba Week" na inahusisha mechi ya kirafiki dhidi ya Power Dynamos ya Zambia pamoja na mechi za timu za wanawake w...
michezo
['Kevin de Bruyne amekuwa kiungo muhimu wa Manchester City msimu huu, akitengeza nafasi chungu nzima zaidi ya mchezaji mwengine yeyote mbali na kuongoza jedwali miongoni mwa wachezaji waliotoa pasi nyingi zilizosababisha magoli. ', 'Ni ndoto ya mshambuliaji yeyote yule, kucheza mbele ya De Bruyne kutokana na pasi zake...
michezo
MKUU wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Ayoub Mohamed Mahmoud amewataka maofisa ardhi na mipango miji mkoani humo kutoa elimu kwa umma juu ya hifadhi na matumizi bora ya ardhi, kama njia moja ya kuepusha migogoro.Aliyasema hayo Fuoni Kipungani baada ya kuirudisha serikalini eneo la ekari tatu lililokuwa likitumiwa na ...
kitaifa
Ripoti iliyotolewa hivi karibuni na TPA ya kati ya Julai 2013 na Machi 2014 kuhusu utekelezaji wa mkakati huo, imeonesha pamekuwa na maendeleo makubwa na kuongezeka kwa ufanisi katika Bandari ya Dar es Salaam, ikilinganishwa na kabla ya Julai mwaka jana.Pamoja na mambo mengine, mkakati wa Matokeo Makubwa Sasa unalenga...
uchumi
IDADI ya watu waliopoteza maisha kutokana na mvua za masika zinazoendelea kunyesha mkoani Rukwa, imeongezeka na kufi kia watano huku idadi ya watu ambao hawana makazi ikifi kia 2,205.Pia mvua hiyo pia imeharibu nyumba 441, shule mbili na makanisa mawili. Aidha wakazi 165 kutoka Kijiji cha Mshete wilayani Nkasi kujikut...
kitaifa
KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Bara ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Zuberi Katwila amesema anaamini kikosi chake leo kitashinda dhidi ya Sudan. Timu hiyo leo inakutana na Sudan mjini Gulu, Uganda katika mechi ya nusu fainali za michuano ya kombe la Chalenji kwa vijana wa umri huo.Tanzania Bara ilifuzu nus...
michezo